Kinana using'atuke kabla ya kujibu haya

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,897
Vyombo vya habari vimeripoti kwa uzito wake habari ya kung'atuka kwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abrahiman Kinana .

Ikumbukwe kuwa Kanali mstaafu ndugu Abrahiman Kinana anaondoka kwenye Siasa huku akiacha umma wa watanzania na Chama chake CCM bila majibu ya kile alichokiita nataka "Mabadiliko Makubwa ndani ya CCM".

Akihitimisha ziara yake jijini Mwanza 29 /06/2015 baada ya kuzunguka Mikoa 26 ya Tanzania Bara alitoa hoja kumi (12) ambazo anapaswa kuzitolea ufafanuzi kabla ya kung'atuka.

Hoja za Kinana zilikuwa kama ifuatavyo :

Mosi , Kinana alisema namnukuu , Mawaziri wa Kikwete wamekuwa wazururaji , wavivu na kila siku wako nchi za nje ,hakuna waziri hata mmoja aliwahi kufanya ziara ya siku kumi Mkoa wowote hapa nchini.

Pili , Serikali ya CCM sio Serikali sikivu kwa wananchi wake .

Tatu , Wabuge wa CCM wamekuwa wa hovyo sana kwa kuunga mkono hoja dhaifu Bungeni kila siku.

Nne , Bunge lisipitishe tena sheria za hovyo zinazowakandamiza Wananchi , Bunge lijalo ( yaani la 11) iwe mwisho.

Tano , CCM in dhaifu haijaweza na haiwezi kuisimamia Serikali , Nataka Marekebiso makubwa ndani ya CCM.

Sita , Serikali ya CCM imekuwa na utitiriri wa kodi nyingi sana zinazoumiza wananchi.

Saba , Kikao changu cha kwanza nitafanya na Wabunge na Nitavunja Party coucas ya CCM hawajafanya kitu kwa miaka mitano iliyopita (2010 - 2015).

Nane , Serikali ya CCM kwa muda wote wa miaka mitano imewatesa wafanyabiashara wadogowadogo ( Wamachinga).

Tisa , Serikali ya CCM kwa miaka mitano imewaambia Watanzania tuko mbioni kuleta Maendeleo , hizo mbio za Serikali zitaisha lini... alisikika Kinana akihoji Serikali ya Chama chake chini ya Kanali mwenzake mstaafu Rais Kikwete.

Kumi , Jeshi la Polisi chini ya CCM limewanyanyasa Vijana wa Bodaboda na nataka hayo yakome.

Kumi na moja , Serikali ya CCM imekosa uadilifu , ni Serikali inayolinda wezi na wala rushwa.

Kumi na mbili , Serikali ya CCM ni Serikali isiyojali muda tazameni jinsi ambavyo Nchi ni Maskini .

Baada ya tuhuma hizo nzito ambazo wabobezi na wachambuzi wa maswala ya kisiasa walisema ameivua nguo CCM , yeye akiwa kama Katibu Mkuu alimalizia hotuba yake kwa kusema hivi ...... Naishukuru Serikali ya CCM kwa kuleta Maendeleo kwa kuwa sasa hivi kila Mtanzania ana Simu ya mkononi tumejenga minara ya kutosha kila mahali , nitajitahidi CCM iwe na Nguvu ya kuisimamia Serikali .

KINANA TOKA HADHARANI.

Kinana atoke hadharani hata kama atatumia mwanya wa Mkutano Mkuu maalum wa CCM July 23 ambapo Rais Magufuli anaenda kurithishwa Uenyekiti wa CCM Mjini Dodoma kujibu hoja hizi :-

1. Ni nini tofauti ya Mawaziri wazururaji na wavivu wa JK na Magufuli wanaokimbizina na Camera za waandishi kila uchao kwa kisingizio cha kuchapa kazi kumbe ni geresha tuuu ili wasitumbuliwe ? Je hawa wa sasa wanafanya ziara zenye tija Mikoani?

2. Je Serikali ya CCM imeshakuwa sikivu kwa wananchi mpaka sasa ? Maana kilio cha maisha magumu kimetamalaki kona zote za Nchi.

3. Je mpaka sasa Wabunge wa CCM si hovyo ? hasa yaliyojiri kwenye hili Bunge la Bajeti 2016/2017 lilomalizika hivi karibuni?

4. Je Bunge la 11 Chini ya wabubge wako wa CCM halijapitisha sheria za hovyo zinazowakandamiza Wananchi?

5. Je CCM sasa sio dhaifu ? inaweza kuisimamia Serikali? Kwa nini unang'atuka kabla ya kufanya ulichokiita " Marekebisho Makubwa ndani ya CCM?

6. Je utitiri wa kodi umepungua ndani ya utawala huu wa Magufuli au umeamua ung'atuke huku ongezeko za VAT likiizamisha Nchi kwenye ufukara?

7. Je umewahi kukaa na Wabunge wako ? Kama umewahi kukaa nao , uamuzi wa kuvunja Party Coucas umeota mbawa?

8 . Je Serikali ya CCM imeacha kuwatesa wafanya biashara wadogo na wakubwa?

9. Je Mbio za Serikali hii ya awamu ya Tano kuleta maendeleo ni haya maigizo ya kiini macho ya madawati tena tunayochangishana sisi wananchi?

10. Je Manyanyaso ya Vijana wa bodaboda yanayofanywa na Jeshi la Polisi yamekoma ?

11. Je uadilifu wa Serikali ya CCM umerejea? kama umerejea mbona baadhi ya mikataba kama ya Lugumi haipaswi kuguswa? Hapo wezi na wala rushwa hawalindwi na Serikali ya CCM?

12. Je Serikali ya CCM imeanza kujali muda? Kama inajali kwa nini Rais Magufuli (kama tasisi ya Urais) imetumia miezi 8 kuunda Serikali? umaskini uliousema utaondokaje wakati Serikali yako haikomboi wakati?

Kila la kheri Mzee Kinana , Mmekula Nchi mmetuacha Vijana tunatoka jasho kusaka Maisha Bora ambayo tunapapasa kila kukicha bila mafanikio.

Leonce J Marto
 
Tunaitengeza nchi irudi kwenye mstari wewe unaturudisha nyuma, yaliyopita si ndwele tugange yajayo.
Sasa ni nafasi ya Magufuli, Kikwete kamaliza Muda wake.
 
CCM ipo madarakani kwa sababu ya uoga na unafiki uliotukuka.
Huyo Kinana leo hii ukimuuliza atakanusha na ataanza kuisifia serikali ya CCM kana kwamba imeshafanya mabadiliko aliyokuwa anayapigia chapuo.
Ndio maana hatupigi hatua kwa unafiki wao.
 
Tanzania inahitaji mabadiliko ya kimfumo na sio hii ya 'one man show' ambayo hata hivyo hayajawahi kuleta mabadiliko chanya.
 
1. Kwa nini Mbowe uliuza chama chetu??
2.Kwa nin uliripotiwa unatorosha mabilioni ya fedha nje ya nchi Mara tu baada ya kuuza chama??
3.Ni kwa nini chadema imepanga makaburini na haina ofisi kwa miaka 20??
4.Lini utaitisha uchaguzi wa mwenyekiti mpya ili tumkabidhi uenyekiti jembe Lowasa??

5. Ni kwa nini chadema hatupeleki maandamano Moshi??

Mbowe jitokeze uyajibu hayo na mioyo ya sisi chadema asilia itasuuzika.
 
Ile ya sheria kandamizi, aliomba kura mjini Tabora, akiahidi atahakikisha wabunge wake wanaziondoa.
Lakini ngojeni tusubili,!!
 
Haya maswali ni kabambe kweli kweli.Kinana hawezi kuyajibu.Na si yeye tu;hata wakusanyike viongozi wa chama waandamizi wastaafu na waliopo,wajumbe wote wa CC na Halmashauri Kuu;hakuna mwenye 'moral authority' ya kujibu hizo hoja.
 
Vyombo vya habari vimeripoti kwa uzito wake habari ya kung'atuka kwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abrahiman Kinana .

Ikumbukwe kuwa Kanali mstaafu ndugu Abrahiman Kinana anaondoka kwenye Siasa huku akiacha umma wa watanzania na Chama chake CCM bila majibu ya kile alichokiita nataka "Mabadiliko Makubwa ndani ya CCM".

Akihitimisha ziara yake jijini Mwanza 29 /06/2015 baada ya kuzunguka Mikoa 26 ya Tanzania Bara alitoa hoja kumi (12) ambazo anapaswa kuzitolea ufafanuzi kabla ya kung'atuka.

Hoja za Kinana zilikuwa kama ifuatavyo :

Mosi , Kinana alisema namnukuu , Mawaziri wa Kikwete wamekuwa wazururaji , wavivu na kila siku wako nchi za nje ,hakuna waziri hata mmoja aliwahi kufanya ziara ya siku kumi Mkoa wowote hapa nchini.

Pili , Serikali ya CCM sio Serikali sikivu kwa wananchi wake .

Tatu , Wabuge wa CCM wamekuwa wa hovyo sana kwa kuunga mkono hoja dhaifu Bungeni kila siku.

Nne , Bunge lisipitishe tena sheria za hovyo zinazowakandamiza Wananchi , Bunge lijalo ( yaani la 11) iwe mwisho.

Tano , CCM in dhaifu haijaweza na haiwezi kuisimamia Serikali , Nataka Marekebiso makubwa ndani ya CCM.

Sita , Serikali ya CCM imekuwa na utitiriri wa kodi nyingi sana zinazoumiza wananchi.

Saba , Kikao changu cha kwanza nitafanya na Wabunge na Nitavunja Party coucas ya CCM hawajafanya kitu kwa miaka mitano iliyopita (2010 - 2015).

Nane , Serikali ya CCM kwa muda wote wa miaka mitano imewatesa wafanyabiashara wadogowadogo ( Wamachinga).

Tisa , Serikali ya CCM kwa miaka mitano imewaambia Watanzania tuko mbioni kuleta Maendeleo , hizo mbio za Serikali zitaisha lini... alisikika Kinana akihoji Serikali ya Chama chake chini ya Kanali mwenzake mstaafu Rais Kikwete.

Kumi , Jeshi la Polisi chini ya CCM limewanyanyasa Vijana wa Bodaboda na nataka hayo yakome.

Kumi na moja , Serikali ya CCM imekosa uadilifu , ni Serikali inayolinda wezi na wala rushwa.

Kumi na mbili , Serikali ya CCM ni Serikali isiyojali muda tazameni jinsi ambavyo Nchi ni Maskini .

Baada ya tuhuma hizo nzito ambazo wabobezi na wachambuzi wa maswala ya kisiasa walisema ameivua nguo CCM , yeye akiwa kama Katibu Mkuu alimalizia hotuba yake kwa kusema hivi ...... Naishukuru Serikali ya CCM kwa kuleta Maendeleo kwa kuwa sasa hivi kila Mtanzania ana Simu ya mkononi tumejenga minara ya kutosha kila mahali , nitajitahidi CCM iwe na Nguvu ya kuisimamia Serikali .

KINANA TOKA HADHARANI.

Kinana atoke hadharani hata kama atatumia mwanya wa Mkutano Mkuu maalum wa CCM July 23 ambapo Rais Magufuli anaenda kurithishwa Uenyekiti wa CCM Mjini Dodoma kujibu hoja hizi :-

1. Ni nini tofauti ya Mawaziri wazururaji na wavivu wa JK na Magufuli wanaokimbizina na Camera za waandishi kila uchao kwa kisingizio cha kuchapa kazi kumbe ni geresha tuuu ili wasitumbuliwe ? Je hawa wa sasa wanafanya ziara zenye tija Mikoani?

2. Je Serikali ya CCM imeshakuwa sikivu kwa wananchi mpaka sasa ? Maana kilio cha maisha magumu kimetamalaki kona zote za Nchi.

3. Je mpaka sasa Wabunge wa CCM si hovyo ? hasa yaliyojiri kwenye hili Bunge la Bajeti 2016/2017 lilomalizika hivi karibuni?

4. Je Bunge la 11 Chini ya wabubge wako wa CCM halijapitisha sheria za hovyo zinazowakandamiza Wananchi?

5. Je CCM sasa sio dhaifu ? inaweza kuisimamia Serikali? Kwa nini unang'atuka kabla ya kufanya ulichokiita " Marekebisho Makubwa ndani ya CCM?

6. Je utitiri wa kodi umepungua ndani ya utawala huu wa Magufuli au umeamua ung'atuke huku ongezeko za VAT likiizamisha Nchi kwenye ufukara?

7. Je umewahi kukaa na Wabunge wako ? Kama umewahi kukaa nao , uamuzi wa kuvunja Party Coucas umeota mbawa?

8 . Je Serikali ya CCM imeacha kuwatesa wafanya biashara wadogo na wakubwa?

9. Je Mbio za Serikali hii ya awamu ya Tano kuleta maendeleo ni haya maigizo ya kiini macho ya madawati tena tunayochangishana sisi wananchi?

10. Je Manyanyaso ya Vijana wa bodaboda yanayofanywa na Jeshi la Polisi yamekoma ?

11. Je uadilifu wa Serikali ya CCM umerejea? kama umerejea mbona baadhi ya mikataba kama ya Lugumi haipaswi kuguswa? Hapo wezi na wala rushwa hawalindwi na Serikali ya CCM?

12. Je Serikali ya CCM imeanza kujali muda? Kama inajali kwa nini Rais Magufuli (kama tasisi ya Urais) imetumia miezi 8 kuunda Serikali? umaskini uliousema utaondokaje wakati Serikali yako haikomboi wakati?

Kila la kheri Mzee Kinana , Mmekula Nchi mmetuacha Vijana tunatoka jasho kusaka Maisha Bora ambayo tunapapasa kila kukicha bila mafanikio.

Leonce J Marto

Tathmini yangu ya haraka zaidi ya 66% ya alichosema Kinana kimefanyiwa kazi
1. Safari za nje zimesitishwa mpaka kibali maalumu
2. Wateule wote wa Raisi wamepewa maelekezo ya kutatua kero za wananchi
3. ???
4. Sheria zilizopitishwa za kuimarisha makusanyo ya mapato ya serikali kamwe huwezi kuziita ni sheria mbovu
5. ??
6.??
7.??
8. Kusimamia utawala wa sheria si kunyanyasa raia. Kila mtu mtu atakiwa kutii sheria bila shuruti
9. Utawala wa sasa una mipando endelevu ya kuleta maendeleo; ndio maana umeweze kutenga 40% ya mapato yote kwa shughuli za maendeleo.
10. Soma namba 8.
11. Utawala wa sasa unapambana na ubadhilivu ndio maana hata sheria ya kuunda mahakama ya mafisadi imetungwa na kupitishwa
12. Tupeana muda Serikali chini ya Raisi wa sasa majibu yataonekana. Umaskini utaondoka kwa kila mtu kukubali kulipa kodi stahiki.

HAYO NI TATHMINI YANGU NA MIMI SI MWANACHAMA WA CHAMA CHOCHOTE ISIPOKUWA SI MVIVU WA KUFUATILIA MASUALA YA KITAIFA
 
chama chochote hakiwezi kufanya vizuri bila ya kuwa na katiba nzuri nchi hii katiba ina matege nandio maana kila miaka chaguzi zinakuja watu wanapewa sera zilezile na wana wachagua viongozi wa bovu jambo la msingi ni CCM kufungua milango ya masikio kuona wapinzani wanasema nini zuri libebwe na lifanyiwe kazi vilevile wapinzani wakubari mazuri yanayo fanywa na CCM tusonge mbele ila siasa za mashindano ya kutujazia tuhuma fulani kafanya hivi yule vile ni upumbavu na inadhihilisha tulivyokuwa na wanasiasa dhaifu na wasio na nia njema na nchi
 
CCM ipo madarakani kwa sababu ya uoga na unafiki uliotukuka.
Huyo Kinana leo hii ukimuuliza atakanusha na ataanza kuisifia serikali ya CCM kana kwamba imeshafanya mabadiliko aliyokuwa anayapigia chapuo.
Ndio maana hatupigi hatua kwa unafiki wao.
MAKOSA YA CCM HAYAWEZI KUHALALISHA WAPINZANI WENYE VYAMA DHAIFU KUPEWA NCHI. HATUWEZI KUWEKA REHANI NCHI YETU PERIOD!
 
Back
Top Bottom