Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,896
Vyombo vya habari vimeripoti kwa uzito wake habari ya kung'atuka kwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abrahiman Kinana .
Ikumbukwe kuwa Kanali mstaafu ndugu Abrahiman Kinana anaondoka kwenye Siasa huku akiacha umma wa watanzania na Chama chake CCM bila majibu ya kile alichokiita nataka "Mabadiliko Makubwa ndani ya CCM".
Akihitimisha ziara yake jijini Mwanza 29 /06/2015 baada ya kuzunguka Mikoa 26 ya Tanzania Bara alitoa hoja kumi (12) ambazo anapaswa kuzitolea ufafanuzi kabla ya kung'atuka.
Hoja za Kinana zilikuwa kama ifuatavyo :
Mosi , Kinana alisema namnukuu , Mawaziri wa Kikwete wamekuwa wazururaji , wavivu na kila siku wako nchi za nje ,hakuna waziri hata mmoja aliwahi kufanya ziara ya siku kumi Mkoa wowote hapa nchini.
Pili , Serikali ya CCM sio Serikali sikivu kwa wananchi wake .
Tatu , Wabuge wa CCM wamekuwa wa hovyo sana kwa kuunga mkono hoja dhaifu Bungeni kila siku.
Nne , Bunge lisipitishe tena sheria za hovyo zinazowakandamiza Wananchi , Bunge lijalo ( yaani la 11) iwe mwisho.
Tano , CCM in dhaifu haijaweza na haiwezi kuisimamia Serikali , Nataka Marekebiso makubwa ndani ya CCM.
Sita , Serikali ya CCM imekuwa na utitiriri wa kodi nyingi sana zinazoumiza wananchi.
Saba , Kikao changu cha kwanza nitafanya na Wabunge na Nitavunja Party coucas ya CCM hawajafanya kitu kwa miaka mitano iliyopita (2010 - 2015).
Nane , Serikali ya CCM kwa muda wote wa miaka mitano imewatesa wafanyabiashara wadogowadogo ( Wamachinga).
Tisa , Serikali ya CCM kwa miaka mitano imewaambia Watanzania tuko mbioni kuleta Maendeleo , hizo mbio za Serikali zitaisha lini... alisikika Kinana akihoji Serikali ya Chama chake chini ya Kanali mwenzake mstaafu Rais Kikwete.
Kumi , Jeshi la Polisi chini ya CCM limewanyanyasa Vijana wa Bodaboda na nataka hayo yakome.
Kumi na moja , Serikali ya CCM imekosa uadilifu , ni Serikali inayolinda wezi na wala rushwa.
Kumi na mbili , Serikali ya CCM ni Serikali isiyojali muda tazameni jinsi ambavyo Nchi ni Maskini .
Baada ya tuhuma hizo nzito ambazo wabobezi na wachambuzi wa maswala ya kisiasa walisema ameivua nguo CCM , yeye akiwa kama Katibu Mkuu alimalizia hotuba yake kwa kusema hivi ...... Naishukuru Serikali ya CCM kwa kuleta Maendeleo kwa kuwa sasa hivi kila Mtanzania ana Simu ya mkononi tumejenga minara ya kutosha kila mahali , nitajitahidi CCM iwe na Nguvu ya kuisimamia Serikali .
KINANA TOKA HADHARANI.
Kinana atoke hadharani hata kama atatumia mwanya wa Mkutano Mkuu maalum wa CCM July 23 ambapo Rais Magufuli anaenda kurithishwa Uenyekiti wa CCM Mjini Dodoma kujibu hoja hizi :-
1. Ni nini tofauti ya Mawaziri wazururaji na wavivu wa JK na Magufuli wanaokimbizina na Camera za waandishi kila uchao kwa kisingizio cha kuchapa kazi kumbe ni geresha tuuu ili wasitumbuliwe ? Je hawa wa sasa wanafanya ziara zenye tija Mikoani?
2. Je Serikali ya CCM imeshakuwa sikivu kwa wananchi mpaka sasa ? Maana kilio cha maisha magumu kimetamalaki kona zote za Nchi.
3. Je mpaka sasa Wabunge wa CCM si hovyo ? hasa yaliyojiri kwenye hili Bunge la Bajeti 2016/2017 lilomalizika hivi karibuni?
4. Je Bunge la 11 Chini ya wabubge wako wa CCM halijapitisha sheria za hovyo zinazowakandamiza Wananchi?
5. Je CCM sasa sio dhaifu ? inaweza kuisimamia Serikali? Kwa nini unang'atuka kabla ya kufanya ulichokiita " Marekebisho Makubwa ndani ya CCM?
6. Je utitiri wa kodi umepungua ndani ya utawala huu wa Magufuli au umeamua ung'atuke huku ongezeko za VAT likiizamisha Nchi kwenye ufukara?
7. Je umewahi kukaa na Wabunge wako ? Kama umewahi kukaa nao , uamuzi wa kuvunja Party Coucas umeota mbawa?
8 . Je Serikali ya CCM imeacha kuwatesa wafanya biashara wadogo na wakubwa?
9. Je Mbio za Serikali hii ya awamu ya Tano kuleta maendeleo ni haya maigizo ya kiini macho ya madawati tena tunayochangishana sisi wananchi?
10. Je Manyanyaso ya Vijana wa bodaboda yanayofanywa na Jeshi la Polisi yamekoma ?
11. Je uadilifu wa Serikali ya CCM umerejea? kama umerejea mbona baadhi ya mikataba kama ya Lugumi haipaswi kuguswa? Hapo wezi na wala rushwa hawalindwi na Serikali ya CCM?
12. Je Serikali ya CCM imeanza kujali muda? Kama inajali kwa nini Rais Magufuli (kama tasisi ya Urais) imetumia miezi 8 kuunda Serikali? umaskini uliousema utaondokaje wakati Serikali yako haikomboi wakati?
Kila la kheri Mzee Kinana , Mmekula Nchi mmetuacha Vijana tunatoka jasho kusaka Maisha Bora ambayo tunapapasa kila kukicha bila mafanikio.
Leonce J Marto