Kinana: Tujilaumu kwa Katiba ya Zanzibar

tpaul

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2008
Posts
27,780
Reaction score
29,231
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana amesema hoja zilizoshawishi marekebisho ya kumi ya Katiba ya Zanzibar hazikuwa na mashiko ya kujenga utaifa, badala yake zilikuwa na sababu za kuleta mpasuko usiokuwa na tija kwa Watanzania.

Akizungumza katika mahojiano na gazeti hili, Kinana alisema marekebisho hayo yaliyoitambua Zanzibar kuwa nchi, ni makosa ambayo pande zote mbili za Muungano zinatakiwa kuyajutia kwa kukosa umakini na kuhisi kuwa ongezeko la mambo ni kuzikandamiza.

Kwa mujibu wa marekebisho hayo, Zanzibar ilitambuliwa kuwa nchi na kumpokonya mamlaka ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika ugawaji wa mikoa na wilaya kisiwani humo, na kumpa mamlaka hayo Rais wa Zanzibar.

Alifafanua kuwa baada ya kuvunjika kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki mwaka 1977, sehemu zote mbili za Muungano hazikuona ukweli ni upi mpaka kufikia muundo ulioleta mgogoro wa kikatiba mpaka sasa.

Alisema sababu nyingine ya kufanya marekebisho hayo ni pamoja na msukumo wa kisiasa kutoka kwa vyama vya upinzani.

Kinana alionya kuhusu mgawanyiko, akisema: "Ni vyema tukakumbuka athari za Uzanzibari na Uzanzibara zilizoelezwa na Mwalimu Julius Nyerere." alisema.

Azidi kumpinga Warioba

Kinana aliendelea kupingana na mapendekezo ya muundo wa Serikali tatu ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyoongozwa na Jaji Joseph Warioba, akisisitiza kuwa waziri huyo mkuu wa zamani anatakiwa kutoa ufafanuzi kuhusu hoja zilizofichika.

Hata hivyo, Jaji Warioba alipohojiwa na gazeti hili kuhusu madai hayo alisema: "Nisingependa kuzungumzia tena suala hilo kwa sababu nilishaeleza kila kitu bungeni.'Issa

Ponda na wenzake 49 wana kesi ya kujibu kwa mashtaka yote matano yanayowakabili.

Mods, samahani msinipige ban: Source: Mwananchi, Alhamisi,Aprili3 2014

:yield:
 
Suala sio kujilaumu, Swala hapo ni kuwashtaki wote waliosababisha kuvunjwa kwa Katiba ya JMT. Sasa mambo ya kutuimbia mashairi huu sio wakati wa mashairi ya siasa za ubabaishaji.
 
Hana lolote huyo mtu, akaeneze tu sera danganya za CCM.
 
Katiba ya Zanzibar: CCM imeshikwa pabaya! JK amewaponza, halafu bado anawataka muendelee kung'ang'ania serikali mbili, kwa kura ya wazi! Ni unafiki wa hali ya juu sana!
 
poacher mkubwa huyu ame compile kiasi kikubwa cha fedha due to his illegal activities!!!!!
 
Lakini aliyesababisha Katiba ya Zanzibar kubadilishwa na kuweka kipengele cha kutambuliwa rasimi kama nchi ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda alipokuja na hoja ya kusema Zanzibar si nchi akijibu maswali Bungeni. Kitendo hicho kiliwaudhi sana wa Zanzibar na kuamua kurekebisha Katiba yao. Waziri wa Katiba na Sheria wa Zanzibar ameapa kamwe Katiba yao haitaondoa kipengele hicho, na atakaye isaliti Zanzibar atashughulikiwa peupe na sasa wanachotaka ni Serikali tatu.
 
Nkasi. Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana amesema hoja zilizoshawishi marekebisho ya kumi ya Katiba ya Zanzibar hazikuwa na mashiko ya kujenga utaifa, badala yake zilikuwa na sababu za kuleta mpasuko usiokuwa na tija kwa Watanzania.

Akizungumza katika mahojiano na gazeti hili, Kinana alisema marekebisho hayo yaliyoitambua Zanzibar kuwa nchi, ni makosa ambayo pande zote mbili za Muungano zinatakiwa kuyajutia kwa kukosa umakini na kuhisi kuwa ongezeko la mambo ni kuzikandamiza.

Kwa mujibu wa marekebisho hayo, Zanzibar ilitambuliwa kuwa nchi na kumpokonya mamlaka ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika ugawaji wa mikoa na wilaya kisiwani humo, na kumpa mamlaka hayo Rais wa Zanzibar.

Alifafanua kuwa baada ya kuvunjika kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki mwaka 1977, sehemu zote mbili za Muungano hazikuona ukweli ni upi mpaka kufikia muundo ulioleta mgogoro wa kikatiba mpaka sasa.

Alisema sababu nyingine ya kufanya marekebisho hayo ni pamoja na msukumo wa kisiasa kutoka kwa vyama vya upinzani.

Kinana alionya kuhusu mgawanyiko, akisema: "Ni vyema tukakumbuka athari za Uzanzibari na Uzanzibara zilizoelezwa na Mwalimu Julius Nyerere." alisema.

Azidi kumpinga Warioba

Kinana aliendelea kupingana na mapendekezo ya muundo wa Serikali tatu ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyoongozwa na Jaji Joseph Warioba, akisisitiza kuwa waziri huyo mkuu wa zamani anatakiwa kutoa ufafanuzi kuhusu hoja zilizofichika.

Hata hivyo, Jaji Warioba alipohojiwa na gazeti hili kuhusu madai hayo alisema: "Nisingependa kuzungumzia tena suala hilo kwa sababu nilishaeleza kila kitu bungeni.'Issa

Ponda na wenzake 49 wana kesi ya kujibu kwa mashtaka yote matano yanayowakabili.

Source:
Mwananchi
 
Inabidi mara nyingine tuwaulize hawa akina Kinana. Je yeye alionana na tume ya marekebisho ya Katiba na akatoa maoni yake? Kama ndivyo, basi tumechoshwa na maneno yao ya kila siku na kumlaumu Jaji Warioba. Kama alitoa maoni ya muundo wa serikali mbili, ajielewe kuwa walio wengi walitaka serikali tatu. Zanzibar ilipokuwa inaandika Katiba yake na hadi kuipitisha, akina Kinana walikuwepo ndani ya CCM na walikaa kimya pasipo kukosoa. Kutokuwajibika kwenu ndiko kulikozaa nia ya walio wengi kudai Tanganyika.
 
Huyu Kinana anaonngea as if sio CCM walioifanyia marekebisho katiba ya Zanzibar. Halafu huu wimbo wa kusingizia kila kitu UPINZANI ni ngojera iliyokosa mashiko. Kinana atwambie mwaka 1984 wakati wanaifanyia marekebisho makubwa katiba ya Zanzibar huo UPINZANI ulikuwepo?. If my brain still serves me well, unlike Kinana kumbukumbu zinaniambia kwamba UPINZANI Tanzania uliruhusiwa 1992.
 
Kinana analinda Ruzuku ya wabunge wa zenji na Tanganyika akichanganya na pesa za kubembeleza muungano anapata cha juu kingi sana, Hana jipya zaidi ya kutetea masilahi tu.
 
Huyu Kinana anaonngea as if sio CCM walioifanyia marekebisho katiba ya Zanzibar. Halafu huu wimbo wa kusingizia kila kitu UPINZANI ni ngojera iliyokosa mashiko. Kinana atwambie mwaka 1984 wakati wanaifanyia marekebisho makubwa katiba ya Zanzibar huo UPINZANI ulikuwepo?. If my brain still serves me well, unlike Kinana kumbukumbu zinaniambia kwamba UPINZANI Tanzania uliruhusiwa 1992.
Chama Tawala Zanzibar ni CCM na m/kiti na katibu Mkuu ni Mmoja tu , Hakuna kinachofanyika Zanzibar pasipo CCM kujua hata mwaka 2010 walilidhia mabadiliko ya katiba ya Zanzibar . Kwani Mfumo huu wa sasa unawanufaisha kupitia Kero wanaitumia vizuri kujinufaisha na kuchelewesha Tanganyika kujikomboa toka Koloni la Zanzibar .
 
mwenye cv ya kinana atuwekee hapa ili tujuwe thinking base yake ni ya namna gani
 
Nchi yetu inaenda mrama kutokana na uwezo mdogo wa kufikiri kwa viongozi wetu. Wakijitahidi kufikiria, fikra zao zinaishia matumboni mwao.nikimaanisha maslahi binafsi. Hawaangalii kabisa mstakabali wa taifa letu kwa miaka mingi ijayo. Hakika tutaangamia kwa viongozi wetu wengi kukosa maarifa.
 
mwenye cv ya kinana atuwekee hapa ili tujuwe thinking base yake ni ya namna gani

hii hapa
images.jpeg
 
kumuondoa rais wa Zanzibar kama makamo wa rais wa muungano sio kosa kosa kusema Zanzibar nchi tokeni povu tu imekula kwenu majangili wakubwa
 
Back
Top Bottom