Inatia kichefuchefu kuona viongozi hao hao wameishiwa hoja zinazolenga changamoto za maisha ya mtanzania badala yake wamekalia vijembe.
Nilishangaa kusikia Nape anatumia propaganda rahisi kuwa Slaa bado ana kadi ya CCM. So what? Nape au hajui au anapotosha makusudi, kwa kuwa katiba ya CCM inatamka wazi kuwa mtu anapojiunga tu na chama kingine uanachama wake CCM unakoma kwa mujibu wa katiba.
Wananchi wanapowaona majukwaani, wanawazia mambo yanayowakabili na wana matumaini kuwa ninyi mna habari njema: shughuli zao za kiuchumi, bei za bidhaa zao, ajira, pato, shule za watoto, kodi, gharama za matibabu, usalama wao na mali zao n.k. Badala yake wanaambulia mipasho, porojo, upotoshaji n.k.
Pathetic.