Uhuru wa kujieleza ni Gololi mpya kwa Watanzania. Watanzania ni wale wale tu

RNA

JF-Expert Member
Mar 27, 2013
1,584
2,683
Miaka ya nyuma sana nchi yetu ilikuwa na vitu vya thamani sana kama madini ambavyo vilikuwa vinapatikana kwa Urahisi sana bila kutumia nguvu sana kama ilivyo sasa.

Inasemekana watu wa Mataifa ya nje walikuwa wakija wanashangaa kuona watu wanachezea dhahabu huku wenyewe wanaitafuta sana, hivyo wakawa wanawaletea vitu vinavyopendeza kwa muonekano kama Gololi na kubadilishana na Dhahabu.

Hichi ndicho kinachotokea sasa Watanzania wanapenda porojo sana hasa kwa sasa za mitandoni, ukitaka umfurahishe mpe uhuru aandike au aseme chochote halafu aangaliwe bila hatua yoyote.

Yaani kwa sasa watu makanisani,magazetini ,mitandaoni wanakashfu serikali ,wanatukana viongozi, wanaandika lugha za kuudhi/kebehi dhidi viongozi na mara nyingine kuudhiana wao kwa wao lakini wanaacha tu na Hicho ndio kinachoonekana Sasa hivi tunaenda sawa na kusahau ugumu wa Maisha uliopo mtaani na Mali/fedha zetu zinazopotea.

Lakini ndio siasa unafanya kile wananchi wanachohitaji ili ukubarike sema watanzania tunanunulika kirahisi sana.

Sehemu nyingine watu wanalilia Maendeleo sisi tunalilia uhuru wa kumtukana au kumchafua kiongozi au umkere pascal Mayalla wa JF unalala kwa Amani ukipata huo Uhuru.

Tutaendelea Kuwa Maskini wa kutupwa kama Watanzania wale wa kupokea Gololi ni hawa hawa Kupewa uhuru wa kujieleza na kuona washapata kila kitu.
 
Nakumbuka Baba w Taifa aliwahi kutoa Mfano ambao ulichukuliwa kama kichekesho cha Almasi na Kipande Cha Chupa.
 
Hii ni fursa kwako

Wakati wanspiga porojo wewe fany kazi zalisha n.k

Baadae watakuja kwako kuja kununua mazao si utakuwa umepata faida?
 
  • Thanks
Reactions: RNA
Back
Top Bottom