VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,136
- 17,871
CCM,kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2015,tulikuwa kwenye hali ngumu. Watanzania kwa mamia yao walikatishwa nayo tamaa na kuichukia vya kutosha na kutisha. Hata mipango ya kujivua gamba ilikwama. CCM ilikuwa njiapanda
Wakatafutwa 'Wasanii wabobezi' wawili wa kisiasa: Kanali Mstaafu na Katibu Mkuu wa chama Abdulrahman Kinana na Kada Nape Nnauye. Hawa wakaandaliwa scenes za kuzicheza na kuonesha hadharani.
Wawili hao wakazunguka takribani Tanzania nzima kukipa chama uhai mpya na kukifanya kipendwe. Maigizo yao yakapigwa picha na kurekodiwa. Kuanzia kula kwa mama ntilie,kujenga madarasa,kuvuka kwa mitumbwi na kadhalika,kote kukaoneshwa kwa watanzania wapenda maigizo
Hatimaye,CCM ikakubalika upya na kwa kishindo kilichozaa ushindi mwaka 2015. Sanaa ikaweka mambo sawa. Sasa kuna juhudi za makusudi za kukisawajisha tena chama. Wapo watu wanawakera makada kwa matendo na maneno yao. Watu hao hasa wapo Serikalini
CCM inabomoka na kuchukiwa kidogokidogo. Tunarejea kulekule. Nawashauri Wasanii wetu wa kisiasa akina Kinana na Nape wasikubali tena kwenda kwenye maigizo ya maagizo. Waacheni wanaobomoa wakajenge wenyewe.
Mwafaaaa!
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam