Kinana: Msipuuze kila hoja ya wapinzani!

Kinana: Msipuuze kila hoja ya wapinzani!

Ng'wamapalala

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2011
Posts
6,811
Reaction score
6,507
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abdulrahman Kinana amewataka viongozi na wananchama wa chama hicho kubadilika na kuachana na tabia ya kubeza kila hoja na malalamiko yanayotolewa na wapinzani kwa niaba ya wananchi.

Katibu mkuu huyo ametoa kauli hiyo katika mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Ruaha wilayani Kilosa ikiwa ni mkutano wake wa kwanza mara baada ya kuanza ziara yake ya siku saba mkoani Morogoro kwa lengo la kusikiliza kero za wananchi na kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM.

Kinana amesema kuwa hoja zinazotolewa na wapinzani lazima zipimwe na kufanyiwa kazi badala ya kubezwa, akisisitiza kuwa tabia ya kubeza kila hoja ya wapinzani imechangia viongozi wengi kushindwa kuwajibika kwa wananchi.

Baada ya kuwahutubiwa wananchi katibu mkuu huyo akatoa nafasi kwa wananchi kuelezea kero zao na akalazimika kujibu baadhi ya hoja hizo ambapo kwa upande wa kero za wakulima wa miwa amehadi kufikisha tatizo hilo kwenye kamati kuu ya CCM, CC .

Awali katibu mwenezi wa CCM taifa Nape Moses Nauye katika utangulizi wake amewapongeza wananchi kwa ushiriki wao katika kutoa maoni ya katiba na uundwaji wa mabaraza ya katiba.

Kwa hisani ya Wavuti.
 

Attachments

  • image.jpg
    image.jpg
    27 KB · Views: 215
  • image.jpg
    image.jpg
    42 KB · Views: 243
  • image.jpg
    image.jpg
    60.9 KB · Views: 205
  • image.jpg
    image.jpg
    27.1 KB · Views: 181
  • image.jpg
    image.jpg
    36.3 KB · Views: 172
  • image.jpg
    image.jpg
    33.7 KB · Views: 193
  • image.jpg
    image.jpg
    69.8 KB · Views: 165
  • image.jpg
    image.jpg
    46.1 KB · Views: 1,176
  • image.jpg
    image.jpg
    44.3 KB · Views: 170
  • image.jpg
    image.jpg
    53.9 KB · Views: 160
  • image.jpg
    image.jpg
    45.5 KB · Views: 154
  • image.jpg
    image.jpg
    47.4 KB · Views: 151
  • image.jpg
    image.jpg
    40.2 KB · Views: 138
  • image.jpg
    image.jpg
    56.5 KB · Views: 150
  • image.jpg
    image.jpg
    50.7 KB · Views: 156
  • image.jpg
    image.jpg
    59.6 KB · Views: 151
  • image.jpg
    image.jpg
    40.9 KB · Views: 146
  • image.jpg
    image.jpg
    60.8 KB · Views: 154
  • image.jpg
    image.jpg
    57.8 KB · Views: 152
Siasa ni kushindana kwa hoja zenye ukweli. Wananchi lazima wauziwe hoja ambazo hazijachakachuliwa.

Vyama lazima viuze ilani zake za uchaguzi na siyo porojo na kile chama ambacho kimekabidhiwa nchi, lazima kitekeleze ilani yake kwa wananchi.

Nchi niya kila mwananchi, kwa maana kuwa kila mwananchi anahitaji kusikilizwa hata kama anachokisema hukipendi kukisikia.

Demokrasia ni pamoja na kukubali kutokubaliana.
 
Al shabab kaiba sana na kuua Ndovu wetu! hapo utaona jinsi CCM wanvoyweza kuwa ni genge la wezi
 
Katibu Mkuu wa CCM Abraham Kinana, amewaasa wana CCM, na Wananchi kwa Ujumla kua wasiwe wanawabeza Wapinzani wanapolalamikia serikali kwani ni haki yao na badala yake Serikali iwasikilize na Kufanyia Mawazo yao kazi badala ya Kuwabeza, kitu ambacho kinasababisha wananchi kuichukia na kukosa Imani na Serikali yao!

Source: Radio free Afrika.
 
Basi aache kwanza kuvuna tembo, maana hilo ni moja ya malalamiko ya wapinzani!
 
Amechelewa tayari kwani wenzake hawapo tayari kusikia jambo lolote toka kwa wapinzani na wakalifanyia kazi,kwao hata kama wakichukua jambo toka kwa wapinzani hulisema kuwa ni lao.
Asubiri anguko lake na la chama chake 2015.
 
Je, anapingana na boss wake aliyesema vyama vya msimu??

si bure inawezekana eneo hilo wapinzani wana nguvu kwa hiyo hakuwa na uchaguzi zaidi ya kusema ukweli.
 
Basi aache kwanza kuvuna tembo, maana hilo ni moja ya malalamiko ya wapinzani!
Mkuu aache tena wakati huko alipo ndio kwenye ile mbuga ya milima ya Udzungwa pamoja na Selous. Watu wa TANAPA kwenye hizo mbuga inabidi wawe makini sana na idadi ya tembo. Usishangae wakapungua baada ya ziara ya huyu jamaa.

Alianzia Kigoma kule Gombe, na sasa yuko huku....
 
Je, anapingana na boss wake aliyesema vyama vya msimu??

si bure inawezekana eneo hilo wapinzani wana nguvu kwa hiyo hakuwa na uchaguzi zaidi ya kusema ukweli.
Mkuu alikuwa Ruaha Kilosa. Hapo ni CHADEMA usipime.
 
Dr. H. Kigwangala upo wapi? Wenzio wanafaidi vitumbua huku.
attachment.php
 
Last edited by a moderator:
Siasa ni kushindana kwa hoja zenye ukweli. Wananchi lazima wauziwe hoja ambazo hazijachakachuliwa.

Vyama lazima viuze ilani zake za uchaguzi na siyo porojo na kile chama ambacho kimekabidhiwa nchi, lazima kitekeleze ilani yake kwa wananchi.

Nchi niya kila mwananchi, kwa maana kuwa kila mwananchi anahitaji kusikilizwa hata kama anachokisema hukipendi kukisikia.

Demokrasia ni pamoja na kukubali kutokubaliana.

Tumekwisha ambiwa na Kagasheki Nchi ni ya Rais, sisi raia ni sawa na wapangaji kwenye nyumba! Sasa wewe unataka kutupotosha!
 
Mkuu aache tena wakati huko alipo ndio kwenye ile mbuga ya milima ya Udzungwa pamoja na Selous. Watu wa TANAPA kwenye hizo mbuga inabidi wawe makini sana na idadi ya tembo. Usishangae wakapungua baada ya ziara ya huyu jamaa.

Alianzia Kigoma kule Gombe, na sasa yuko huku....

Hayo ni mazushi yasiyo na msingi, Tusisahau wahenga walivyo sema " Dua ya kuku imuui mwewe" hiyo ni ushiriki wako katika sakata la character assasination, amabayo inalingana na wale wanaosema Ben Saa 8 na sumu .
 
Vipi kuhusu kuzomewa?naskia ilibidi akache mkutano,au ni porojo tu za chadema??? Spati picha kinana akitoka nduki huku nyuma akisindikizwa na huyooooooo huyooooooo pigaaaaaa mweh!
 
Ruaha kuna ndovu wengi sijui ndio anaenda kuwamalizia......................?
 
Je, anapingana na boss wake aliyesema vyama vya msimu??

si bure inawezekana eneo hilo wapinzani wana nguvu kwa hiyo hakuwa na uchaguzi zaidi ya kusema ukweli.

mkuu hicho kijiji ccm ilishakufa ikazikwa kitambo hapo wametumia busara tu mana hapo hakuna dhambi kubwa ambayo ukiifanya na ukasabibisha wananchi kukupiga mawe kama kuwaambia chadema haifai mana chadema ndo imewafumbua macho hapo hadi vikongwe hicho kijiji ni wanachadema
 
Back
Top Bottom