Kinana kupitia Wanasheria amuandikia Msigwa kumtaka amuombe radhi

Sangarara

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
13,112
2,000
Katibu Mkuu wa CCM ndugu Abdulrahman Omar Kinana, kupitia kwa wanasheria wa LAW OFFICES OF ERIC S. NG'MARYO wa Moshi amemuandikia Mbunge wa Iringa Ndugu Peter Msigwa agizo la kumtaka amuombe radhi kwa matamshi ambayo kinana anadai ni ya uongo kwamba,

"Nakuandikia kwa maagizo niliyopewa na mteja wangu, Ndugu Abdulrahman Kinana, kufuatia matamshi yako ya uwongo ambayo yamemkashifu, kumfedhehesha na kumshushia hadhi, Matamshi hayo uliyoyatoa mchana wa tarehe 21 April, 2013 katika mkutano wa hadhara wa kisiasa uliofanyika kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Mbugani, Wilaya ya Nyamagana, jijini Mwanza. Mkutano huo ulihudhuriwa na watu wengi. Pamoja na watu hao walikuwepo pia waandishi wa habari, wakiwepo wanahabari wa magazeti, radio televisioni. Habari zenye Maneno yako ya Kashfa zimeenea nchi nzima na duniani kote kwa njia ya habari elektoniki, ikiwepo mitandao ya kijamii. Habari hizo zinaendelea kusomwa hadi sasa, na zitabaki kuwa kumbukumbu ya kudumu katika intaneti na kwenye hifadhi nyingine za habari" hiyo Para ya kwanza,

Para ya Pili ina hit point sasa, kwamba "Katika Mkutano huo, ulisikika ukisema maneno mengi ya Kashfa kwa mteja wangu, yakiwemo haya yafuatayo: Kinana (na naomba waandishi w habari mnisikie na nyie usalama wa Taifa mkapeleke habari) hana sifa za kupita barabarani na kuwaambia watanzania waiamini ccm. Kinana mikono yake si misafi hata kwenye NASACO, Shirika la Meli Tanzania, kuna harufu ya ufisadi ndani yake, ajibu hapa... Kinana Meli zake ndio zinahusika kubeba mapembe nchi hii, hajajibu hoja hizo! kwa siku katika nchi hii tembo sitini na saba wanauwawa...

Hao ndio wanaokifadhili Chama cha Mapinduzi wakina Kinana halafu wanakuja eti kuwashawishi watanzania muwasikilize na kwamba Chama cha Mapinduzi eti ni kizuri. Halafu leo tukikaa ndani ya Bunge tunapojaribu kuwatetea wananchi tumeacha majimbo yetu, Haya mambo ninayaongea ni hatari kwa sababu haya yote ni majangiri ni organized crime ni mtandao wa kimataifa uko duniani kote. unaweza ukatuua lakini wabunge tumesimama tunawatetea.."

Hivyo anamtaka Msigwa amuombe msamaha yaishe au la atamvuruta mahakamani, tena kwa vitisho katika para ya mwisho anasema "Nakuangaliza na kukutahadharisha kwamba iwapo hutatimiza matakwa ya Mteja wangu kama yalivyoainishwa kwenye barua hii, basi kesi itakayokuja dhidi yako itakuwa na madai makubwa na mengi kuliko yale yaliyotajwa humu, na unaweza kubebeshwa mzigo wa uharibifu, hasara na madhara uliyomsababishia Mteja wangu, pamoja na gharama za kesi nzima, ambazo zote zinaweza kufikia mamilioni ya Shilingi za Kitanzania"

Kuna para kumi na mbili, nimeweka attachment, na inapatikana ukurasa wa ishirini na tano wa gazeti la mwananchi, sina hakika juu ya magazeti mengine.

Sina hakika kama kazi ndio imeanza au imefikia Mwisho.

Zaidi, soma;

Mchungaji Msigwa akiri kumsingizia Kinana ujangili, amwangukia na kumwomba msamaha - JamiiForums

DBCEBFCC-7D40-4F7D-8C67-FF5E23FE69B0.jpeg

 

T2015CCM

JF-Expert Member
Sep 13, 2012
7,932
1,500
Sasa Msigwa amekwisha, kuna watu ambao ni makini kwenye mambo yao, hawakurupuki.
 

Tiba

JF-Expert Member
Jul 15, 2008
4,581
2,000
Mkuu Sangarara,

Umetumia neno sahihi "kutishia nyau". Hii kweli ni kutishia nyau lakini anasahau kwamba mtu mzima hatishiwi nyau. Sioni kama kuna haja ya kumuomba msamaha jangiri na mwizi mkubwa huyu.

Tiba
 

T2015CCM

JF-Expert Member
Sep 13, 2012
7,932
1,500
Hizi habari za udaku wa kwenye magazeti ya uwazi, tz daima na kiu msigwa amezichukua kuwa ni agenda amezipeleka bungeni, sasa zinamtokea puani
 

bily

JF-Expert Member
Apr 5, 2012
8,040
2,000
hakuna kumuomba mkimbizi radhi huku akiiba mali za wazawa hatulie kimya mharamia mkubwa.
 

Ngalikihinja

JF-Expert Member
Sep 1, 2009
21,072
2,000
Vijana wengi wa bavicha huwa wanadhani kuwa ubaguzi ni pale mzungu anapombagua mtu mweusi tu!
We sema maneno yako haya lakini ukumbuke tembo 67 kwa siku wanauwawa... Kuna wakati tuache blah blah za siasa na kuteteana kwa ujira wowote ule ule.... After 15 years, utajutia ulichokiandika...
 

Sangarara

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
13,112
2,000
We sema maneno yako haya lakini ukumbuke tembo 67 kwa siku wanauwawa... Kuna wakati tuache blah blah za siasa na kuteteana kwa ujira wowote ule ule.... After 15 years, utajutia ulichokiandika...
Hizi statistics za Msigwa ni confirmed lakini?
 

ilboru1995

JF-Expert Member
Oct 4, 2007
2,329
0
Msigwa asilale kuanzia sasa, Lazima afanye juu chini akusanye ushahidi wa kutosha dhidi ya madai ya tuhuma alizomshushia Kinana... Kinana ni one of the best Brains nchi hii imebahatika kuwa nazo, hawa ni masterminder wa mambo mengi katika nchi, uwezo wake ni mkubwa kuliko wengi wetu tunavyo mjua...Msigwa asipoangalia anaweza akaichukia siasa soon...once again, Mhe Msigwa kusanya ushahidi wa kutosha mapemaa kabla kibao hakijageuka...
 
Top Bottom