Kinana: CHADEMA wana potosha maana ya 'nguvu ya umma'

Kwani wewe hilo neno uwa uliloliweka hapo lilipaswa kuwepo? Mbona unakuwa mbishi kama mwenezi wako?
usianze kukimbia kimbia, hilo neno ambalo umetumia "huwa" linapaswa kuwa mahali hapo?

Usilete habari za "ua" wakati mimi nimeuliza "huwa".
 
WanaJF!

Katibu mkuu wa CCM, bwana Kinana, ametoa ufafanuzi wa kina kuhusu msemo 'nguvu ya umma' kwani msemo huu umekuwa ukitumiwa kimakosa na CHADEMA.

Bwana Kinana kama ilivyo ada kwake, uwa hapendi kuona udanganyifu na upotoshaji ukifanywa, kwani yeye ni mtu mkweli na hupenda kuona haki ikisimama.

Bwana Kinana amesema kuwa, "nguvu ya umma ipo kwenye sanduku la kupiga kura, kwa kuwa CCM ilipata kura nyingi kwenye uchaguzi mkuu, hivyo nguvu ya umma ipo kwa CCM".

Maneno hayo ya hekima yaliyo tolewa na bwana Kinana amekuwa akiyasema mara kwa mara ili kuelewesha wananchi maana halisi ya nguvu ya umma ili wananchi sasa wahoji ni nguvu gani ya umma ambayo CHADEMA wana imaanisha!


Bwana Kinana kama ilivyo ada kwake, uwa hapendi kuona udanganyifu na upotoshaji ukifanywa, kwani yeye ni mtu mkweli na hupenda kuona haki ikisimama.

Amewahi kueleza ukweli kuhusu meli kukamatwa na meno ya Tembo?, Vipi biashara yake ya vipusa mbona hatuelezi watanzania tukaelewa kama anaifanya hii biashara kihalali
 
Kiongozi!

Labda kama hekima unayo isema ina tofauti na HEKIMA (kuwa na busara, fikira/maono chanya) tunayo ijuwa. kinana huyu huyu anaye beba pembe za ndovu kwenye vyombo vyake vya usafiri? Kinana huyu huyu anaye lalamikiwa kwa kubadilisha umiliki wa mashine za kufulia za hospital ya Arusha? Kinana huyu huyu anaye lalamikiwa kupanga mbinu chafu za kufifisha upinzani? Kinana huyu huyu anaye lalamikiwa vijana wake kuhalalisha Miraa kuwa buashara halali Arusha?

Na MAZAGA ZAGA mengine yanayo fanana na hayo...................? POOR MY CCM.
Mkuu umechanganya na stori inayomuhusu Leema wa arusha


Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Ndiyo bwana eh bwana sawa bwana hivi huyu kinana si alishawazuia kumuita bwana mheshimiwa ? Bwana?
 
Vipi kuhusu ile kesi ya Madai dhidi ya Mchungaji Msigwa uliyoifungua Mh Kinana?Au ilikuwa mkwara mbuzi tu?
 
Amesema wapi. ok, kachukue buku 7 Lumumba,leo wikend mambo safi, weka na maneno ya nape na mwigulu unaweza jikuta na buku 21 ya viroba.

ufipa fc, kinondoni hq, mia 2 per post...badae unaenda kugonga viroba ili mkajilipue kwenye mkutano wenu
 
Huyu kilaza ana meli za kusafirisha meno ya tembo!

Can you imagine Secretary General wa Labour Party,au Republican awe anacheza mchezo huu?ni Tanganyika tuu hii inawezekana
 
Chadema kweli sasa imetisha. Inawanyima watu usingizi. Imewapeleka watu shule kila iitwapo leo. Dah!
Safi sana

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Waje kwenye midahalo hapo tutawaamini kwa yale wayasemayo, lakini anaongea na familia yake na wewe KIBARAKA wake unatuletea sisi huku huo utumbo, ukweli upo wakutanapo wenye akili ktk meza moja tumewachoka wazee wa kuepa hamna HOJA MAGAMBA
 
Alichosema Kinana ni kweli kama huo uchaguzi utakuwa huru, bila mizengwe na uchakachuaji. Kama kweli wanaamini nguvu ya umma hupatikana katika box, mbona serikali ya CCM inawaingilia wakazi wa Arusha mjini ambao walishasema 2010?
 
Hivi Kinana siku hizi amekuwa mtafasiri wa terms za CHADEMA au ameanza kazi BAKITA?AU DICTIONARY?
Basi pia atupe tafsiri ya UJANGILI WA WANYAMAPORI!!!!!:coffee:
 
Mpaka sasa Tanzania tuna jumla ya Tembo wangapi waliobaki? Nimepita mikumi sijaona hata mmoja. Au wamehamia serengeti:bored:
 
THITHIEMU badala ya kutangaza sera mmeamua kukaa mezani na kuwatafsiria watanzania kuhusu terminology na misemo wanayotumia CHADEMA. Do you really think hicho ndicho wanachama wenu wanakihitaji kwa sasa? Hata hivyo nikipiga darubiri sioni kama mna chochote cha ziada kuwaeleza wanachama wachache waliobaki
 
Mi nafikiri ana mengi ya kutolea ufafanuzi yanayohusu chama chake, hembu atufafanulie na ile kauli yao kuwa CCM ni chama cha wakulima na wafanyakazi,je bado CCM imebaki hivyo,au imekuwa ya wafanyabiashara na matapeli?
 
Nguvu ya uma kwa kinana ni kuhakikisha TEMBO wote wanaisha duniani.
 
WanaJF!

Bwana Kinana amesema kuwa, "nguvu ya umma ipo kwenye sanduku la kupiga kura, kwa kuwa CCM ilipata kura nyingi kwenye uchaguzi mkuu, hivyo nguvu ya umma ipo kwa CCM".

Maneno hayo ya hekima yaliyo tolewa na bwana Kinana amekuwa akiyasema mara kwa mara ili kuelewesha wananchi maana halisi ya nguvu ya umma ili wananchi sasa wahoji ni nguvu gani ya umma ambayo CHADEMA wana imaanisha!

Nakubaliana na wewe kabisa!! hebu niambie, ile 4-0 ya arusha ilikuwa nguvu ya nini?
 
Back
Top Bottom