TandaleOne
JF-Expert Member
- Sep 4, 2010
- 1,644
- 709
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, Mhe. Abdurahaman Kinana anazungumza katika wilaya ya Sumbawanga Mjini ambako amezungumzia juu ya suala la kero za Usafiri na Barabara, ambapo amesema tayari serikali imeshatenga fedha ya kutosha kwa ajili ya barabara hiyo ambapo tayari baadhi ya makandarasi wanaendelea na ujenzi wa makaravati tayari kwa kuendelea na ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami.
Pia Mheshimiwa kinana amezungumza juu ya suala la Uhifadhi wa mazingira ambapo amewataka wachina ambao wanaendesha zoezi la uchimbaji wa madini katika mbuga ya katavi kuondoka mara moja katika hifadhi hiyo na kusisitiza kuwa suala la uhifadhi wa mazingira ni jambo muhimu na kimsingi linaendana na siasa ya CCM ya kupambana na umasikini, alisema " Moja kati ya malengo na maudhui ya CCM ni kuona kwamba matumizi ya utajiri wa taifa yanatilia mkazo maendeleo ya wananchi na hasa jitihada za kuondoa Umasikini, Ujinga na Maradhi" alimalizia kueleza kuwa Mazingira ni nyenzo muhimu ya maendeleo na suala mtambuka, ambalo linagusa sekta mbalimbali za kiuchumi na kijamii.
Kisha Mheshimiwa Kinana alizungumza juu ya suala la uwezeshaji wa wananchi kiuchumi na ujenzi wa msingi wa uchumi wa kisasa wa Taifa linalojitegemea hasa kutokana na rasilimali zetu akisisitizia zaidi juu suala la kilimo na utekelezaji wa sera ya kilimo kwanza. Akahimiza vijana kuchakalika na kutumia kikamilifu fursa ya kijiografia ya sumbawanga ambapo hupata mvua nyingi na ya kutosha.
Hivi sasa Mheshimiwa Nape Nnauye, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Idara ya itikadi na Uenezi anashambua jukwaa...,updates zaidi hivi punde...!