Kinana atoa siri ya CCM kukaa madarakani muda mrefu

SautiYaMnyonge

JF-Expert Member
Joined
May 13, 2018
Posts
439
Reaction score
742
Akiwahutubia Wana-CCM mkoani Kilimanjaro Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Ndg Abdulrahman Omar Kinana amesema chama hicho kimekuwa madarakani muda mrefu kwa sababu za msingi. Amezitaja sababu hizo kuwa ni uhuru na haki ya wanachama kuchagua na kuchaguliwa pamoja na utoaji wa maoni kwenye vikao.

Aidha, alisisitiza misingi imara iliyoachwa na waasisi wa chama hicho hayati Mwl Julius Nyerere na Sheikh Abeid Amani Karume ya haki, utu, usawa, uadilifu na utumishi wa watu nayo imekuwa chachu hivyo ienziwe kwa vitendo.

"Tusikubali mambo haya yakatutoka maana nguvu ya ushawishi na uimara wa CCM utapungua au kuyumba. Tusikubali wanachama wakaona siku hizi haki na uhuru hakuna au wananchi wakaona chama walichokiheshimu na kukiamini hakiwasikilizi tutajiweka kwenye hatari."

Kinana amesema atazungumza na waziri wa ofisi ya Rais Tamisemi Mheshimiwa Innocent Bashungwa ili afike mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya kukutana na kuwasikiliza madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Moshi na Moshi Manispaa kwa lengo la kutatua migogoro iliyojitokeza ili kuleta utulivu na kuharakisha maendeleo ya wananchi.

Kinana amehitimisha kwa kuwataka viongozi na watendaji wa chama na serikali mkoani humo kuendelea kufanya kazi kwa ushirikiano na mshikamano ili kuwatumikia wananchi kwa ufanisi.
IMG-20220426-WA0067.jpg
IMG-20220426-WA0053.jpg
IMG-20220426-WA0059.jpg
IMG-20220426-WA0060.jpg
IMG-20220426-WA0045.jpg
 
2015 ye na mwenzie chama kiliwafia mikononi. Walishakataliwa hadi na wana ccm wenzao. Sasa sijui wanachama walikikataa chama au walimkataa kinana, jk na nape.

Nakumbuka ilifikia hatua ni bora utembee uchi utakuwa salama kuliko kuvaa nguo za ccm. Nyumba za wana ccm kindakindaki zilianza kupigwa moto.
 
Safi sana paruaneni wenyewe kwa wenyewe huko.
 
Siri gani zaidi ya wizi wa kura na kubaka demokrasia
Nashangaa Kinana pamoja na kwamba yupo kwenye mfumgo wa mwezi mtukufu bado anasema uwongo mchana kweupe?! Labda aseme misingi ya uwizi wa kura pamoja na matumizi ya polisi na vyombo vingine vya dola.
Bado hatujasahau gilba za kupita bila kupingwa, wapinzani kukatwa ati hawajui kujaza fomu, matumizi ya majambazi kama akina Sabaya kuvamia na kutesa wagombea wa upinzani hasa CDM ili kuwatisha wapinzani.
 
Amefunga basi au ni zuga tu? sahivi wiki ya 2 sijaona hata mavi ya tembo barabarani na wakati ilikuwa ni kawaida kuwaona
 
2015 ye na mwenzie chama kiliwafia mikononi. Walishakataliwa hadi na wana ccm wenzao. Sasa sijui wanachama walikikataa chama au walimkataa kinana, jk na nape.

Nakumbuka ilifikia hatua ni bora utembee uchi utakuwa salama kuliko kuvaa nguo za ccm. Nyumba za wana ccm kindakindaki zilianza kupigwa moto.
Na sahivi tunarudi kulekule
 
Akiwahutubia Wana-CCM mkoani Kilimanjaro Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Ndg Abdulrahman Omar Kinana amesema chama hicho kimekuwa madarakani muda mrefu kwa sababu za msingi. Amezitaja sababu hizo kuwa ni uhuru na haki ya wanachama kuchagua na kuchaguliwa pamoja na utoaji wa maoni kwenye vikao.

Aidha, alisisitiza misingi imara iliyoachwa na waasisi wa chama hicho hayati Mwl Julius Nyerere na Sheikh Abeid Amani Karume ya haki, utu, usawa, uadilifu na utumishi wa watu nayo imekuwa chachu hivyo ienziwe kwa vitendo.

"Tusikubali mambo haya yakatutoka maana nguvu ya ushawishi na uimara wa CCM utapungua au kuyumba. Tusikubali wanachama wakaona siku hizi haki na uhuru hakuna au wananchi wakaona chama walichokiheshimu na kukiamini hakiwasikilizi tutajiweka kwenye hatari."

Kinana amesema atazungumza na waziri wa ofisi ya Rais Tamisemi Mheshimiwa Innocent Bashungwa ili afike mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya kukutana na kuwasikiliza madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Moshi na Moshi Manispaa kwa lengo la kutatua migogoro iliyojitokeza ili kuleta utulivu na kuharakisha maendeleo ya wananchi.

Kinana amehitimisha kwa kuwataka viongozi na watendaji wa chama na serikali mkoani humo kuendelea kufanya kazi kwa ushirikiano na mshikamano ili kuwatumikia wananchi kwa ufanisi.View attachment 2201374View attachment 2201375View attachment 2201376View attachment 2201378View attachment 2201380
Mnafutirisha watu kama Sanaa tu. Mungu gani atapokea Dua ya Mnafiki?

Sent from my M2003J15SC using JamiiForums mobile app
 
Aidha, alisisitiza misingi imara iliyoachwa na waasisi wa chama hicho hayati Mwl Julius Nyerere na Sheikh Abeid Amani Karume ya haki, utu, usawa, uadilifu na utumishi wa watu nayo imekuwa chachu hivyo ienziwe kwa vitendo.
Sawasawa!
Basi, 2025 tusiibe kura ili tupate ushindi halali maana ni kweli chama chetu kinapendwa na wananchi wengi..
Wizi wa kura unatuchafulia taswira nzuri ya chama
 
Kabisa mkuu.
 
2015 ye na mwenzie chama kiliwafia mikononi. Walishakataliwa hadi na wana ccm wenzao. Sasa sijui wanachama walikikataa chama au walimkataa kinana, jk na nape.

Nakumbuka ilifikia hatua ni bora utembee uchi utakuwa salama kuliko kuvaa nguo za ccm. Nyumba za wana ccm kindakindaki zilianza kupigwa moto.
Ule moto sijui hata wameuzima vipi
 
Akiwahutubia Wana-CCM mkoani Kilimanjaro Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Ndg Abdulrahman Omar Kinana amesema chama hicho kimekuwa madarakani muda mrefu kwa sababu za msingi. Amezitaja sababu hizo kuwa ni uhuru na haki ya wanachama kuchagua na kuchaguliwa pamoja na utoaji wa maoni kwenye vikao.
Naunga mkono hoja
Kazi iendelee.
P
 
Back
Top Bottom