Kinana asema CCM haifai, awashangaa wanaopinga

David Djumbe

Member
Oct 14, 2013
42
36
katika hali ya kushangaza , leo akihutubia mkutano wilayani Chunya Katibu Mkuu wa CCM A . Kinana , amesema sera za ardhi zipo ni nzuri lakini zinashindwa kutekelezwa na ndio maana anawashangaa wanaCCM wanapinga kuambiwa hawafai... " inakuweje Serikali ichukue mashamba kwa wananchi halafu ikashindwa kuyaendeleza? na kama imeshindwa kwanini wasiwarudishie wananchi? je ni halali wananchi kukodi mashamba yao wenyewe? sasa kwanini tukiambiwa CCM haifai tunakataa?

huyo ni katibu mkuu CCM ngoja tuwasikie vibaraka wanasemaje hapa.
nimewasilisha
 
katibu mkuu wa ccm mwenye ile meli iliyokamatwa na pembe za ndovu mchini China leo amekiri udhaifu na kushindwa kwa chama anachokiongoza.

Akiwa kwenye ziara ya kichama huko Chunya mkoani Mbeya wakati akiwahutubia wananchi alisema "Wananchi mkiona mambo hayaendi vizuri mnailaumu ccm na kuona haifanyi chochote, hiyo ni kweli na mko sahihi".

kauli hii pamoja na ile kauli yake pamoja na Nape kusema kuwa kuna mawaziri mizigo ni sawa na kuwaambia wananchi kuwa hata aliye wachagua na kusimamia baraza la mawaziri naye ni mzigo, kwa maana hiyo hata aliye peperusha ilani yenye ahadi ambazo leo hii hazitekelezeki naye ni mzigo tu maana wananchi wanapo lalamika kuwa serikali haifanyi chochote ni matunda ya kuwa na kingozi legelege ambaye ni mzigo.

mwalimu Nyerere aliwahi kusema "Viongozi legelege huzaa serikali legelege" na ndio tunacho kishuhudi leo na ndio Kinana anacho kikiri mbele ya wana Chunya.

kama Kinana anakiri, watetezi wa CCM wanaoshinda na kutukana mitandaoni wanataka ushuhuda wenye ushahidi gani?
 
Labda ukiweka speech yote itaeleweka zaidi. Hii ya kuchomoa mstari mmoja tu ni ngumu kueleweka. All in all naona kama alikuwa anatoa changamoto kwa serikali. Kuna tofauti ya serikali na chama tawala. Dhana ya kutofautisha chama tawala na serikali haieleweki kwa watu wengi. Lakini mtaelewa tu as we go. Ndo maana mmesikia Nape akiwananga Mawaziri mzigo.
 
Kinana atasemaje sasa ilhali mpaka leo hatuna nishati ya umeme ya uhakika

btw, vipi mpango wa flyovers pale ubungo na ukanda wa gaza pale Migo, kuna matumaini? vipi kuhusu pale Tazara, ama ilani ya 2010 ilisemaje?

Neno la Mwenyekiti Kikwete lipo sahihi kuwa wakati ndio huu kwa CCM kujiandaa kisaikolojia kuelekea baada ya uchaguzi wa 2015
 
David, hujaongeza chumvi hapo?

Kitu ambacho sina shaka nacho ni ukweli wa kuwa CCM ni completely IRRELEVANT kwa Tanzania ya sasa na ijayo.

,
 
Nimefuatilia karibu Taarifa ya Ziara anazofanya Katibu Mkuu wa CCM na kila sehemu anayopita anaonyesha kupinga mambo yaliyopangwa na serikali huku akitaka yasitishwe au yarekebiswe huku yakiwa yamepangwa na serikali inayoongozwa na chama chake mfano hai ni hii leo nimemsikia akikosoa sera ya uwekezaji inayotekelezwa na kusema kuwa inawanufaisha zaidi wawekezaji na kuwanyanyasa wananchi, pia nilimsikia akikosoa mpango wa mikopo uliopangwa na serikali kwa wachimbaji wadogo wa madini inayotaka mkopaji awe na dhamana ya nyumba yeye amesema hilo haliwezekani kwani wanatakiwa wakopeshwe tu bila kujali dhamana hiyo.

My Take
Ninavyojua mimi mambo mengi ya jinsi ya kuiendesha serikali hii huwa wanaongea katika kikao chao cha CC ambacho wote waliomo humo ni wana CCM akiwemo na yeye je alishindwa kuyawasilisha huko hadi leo hii anayaongelea mbele ya wananchi na kuionyesha kuwa serikali ni dhaifu pamoja na watendaji wake yaani wakiwemo mawaziri pia na Mh. Rais.

Ushauri wangu angejikita kuelezea mafanikio ya utekelezaji wa Ilani ya CCM kuliko kuongea maneno ambayo ni dhahili yalitakiwa yasemwe na vyama vya Upinzani na sio chama kinachotawala nchi.

View attachment 124672 nape na baiskeli.jpg

View attachment 124675 migiro.jpg
 
Tunasubiri Magazeti Kesho Asubuhi... Kama Kawaida yao angekuwa ni Kiongozi Chadema ametamka hivyo... Ungepigwa Mwano Kesho!...
 
Back
Top Bottom