Kinana Anatukumbusha Kifo Cha Horace Kolimba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kinana Anatukumbusha Kifo Cha Horace Kolimba

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mwanahabari Huru, Jul 12, 2015.

 1. Mwanahabari Huru

  Mwanahabari Huru JF-Expert Member

  #1
  Jul 12, 2015
  Joined: Mar 9, 2015
  Messages: 12,725
  Likes Received: 22,130
  Trophy Points: 280
  Ni miaka kama ishirini hivi imepita,pale aliyekuwa katibu Mkuu wa ccm ndg Horace Kolimba aliposema" ccm imepoteza mwelekeo''


  Mameno haya yalimfanya aitwe Chimwaga kuhojiwa, lakini kabla ya kujieleza alipatwa na umauti akafariki.


  Kinana juzi wakati anahutubia mkutano wa kuhitimisha ziara zake zilizokula fedha ya chama,alisema mambo mengi,ambayo yanaonesha chama hiki kimeishiwa mbinu!

  Mambo hayo ni:

  * serikali ya ccm kila siku inasema iko mbioni,mbio hizo zitaisha lini?

  * serikali ya ccm wabunge wake ni wa hovyo,wanaunga mkono hoja dhaifu,

  * serikali ya ccm imepitisha sheria nyingi zinazowanyanyasa wananchi,

  * serikali ya ccm imekuwa ikiwatesa bodaboda sasa mwiko,

  * serikali ya ccm, wabunge wake na mawaziri hawajawahi kufanya ziara kumi tu mikoani,

  * serikali ya ccm inalea mafisadi!

  Wakati akisema hayo!
  Mugombea urais kupitia chama hicho alibwaga manyanga kwa kuzitupa chini fomu za kuomba kuteuliwa, baada ya kuchoshwa kuombwa rushwa!

  Inashangaza sana.Katibu Mkuu huyu alikuwepo wakati Wabunge wake wakitetea Escrow,alikuwepo wakati ccm ikiwafukuza wafabiaahara wadogowadogo ( machnga) jijini Mbeya,Mwanza na Dar) ,

  Alikuwepo wakati wabunge wa ccm wakiunga mkono kuyakanyaga maoni ya Rasmu ya katiba ya warioba huku akiwa Kule morogoro mjini aliwaita wapinzani kuwa wao ni waroho wa madaraka! Hakuona wakati ule anaona sasa!

  Najua anatapatapa,Lakini alikuqa pembeni mwa ubavu wa Jk wakati wakiunga mkono hoja hizo,alishindwaje kusimama kwenye vikao vya chama kama shuja kuwaonya na kuzuia ujinga huo? Angefanya hivyo tungemwita shujaa!
  Leo anarukumbusha tu kauli za baba wa Taifa;

  * serikali dhaifu haikusanyi kodi,itabaki kukimbizana na wauza pipi ba karanga barabarani!

  Mwanasiasa dhaifu,anapoishiwa hoja anaweza kujinasibisha kwenye udini au ukabila!

  Watanzania wanahitaji,wanahitaji mabadiliko,wasipoyaona ndami ya ccm,watayatafuta nje ya ccm!


  Watanzania,ccm imeyumba,imeishiwa utashi wa kulinda afya, elimu na usalama wao,tunaendelea kuwa maskini huku wanaosimama jukwaani wana miaka karibu 21 hawajui Mwananchi anayeishi kijiji cha Lupembe atasomeshaji,atatibiwaje,ataongezaje kipato chake?
  Tuwakatae Oktoba!
   
 2. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #2
  Jul 12, 2015
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,012
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Haya yote yanaimulika serikali legelege ya chama cha mafisadi na hapa walipotufikisha Watanzania tunasema imetosha!!!!!!!

  Tunawashukuru!
   
 3. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #3
  Jul 12, 2015
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,996
  Likes Received: 493
  Trophy Points: 180
  CCM wameoza, wamebaki wanauana wenyewe......
   
 4. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #4
  Jul 12, 2015
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,177
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  Mwaka Wetu huu magamba tupa Kule...
   
 5. Jihan

  Jihan Senior Member

  #5
  Jul 12, 2015
  Joined: Jul 11, 2015
  Messages: 146
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  UKAWA huu ndio wakati wetu kuchukua nchi japo tujiandae kwa vita maana magamba hayatokubali kuachia nchi kirahisi kama tunavyodhani.
   
 6. Fukara

  Fukara JF-Expert Member

  #6
  Jul 12, 2015
  Joined: Dec 28, 2013
  Messages: 1,444
  Likes Received: 218
  Trophy Points: 160
  Watanzania bwana kwaiyo unataka tuongozwe na malaika au maana ndio yupo perfect.
   
 7. m

  muamasishaji Member

  #7
  Jul 12, 2015
  Joined: Aug 4, 2012
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Kamanda Hiv Upo Hoja Yako Nimeikubali Kaka
   
 8. m

  mkezwag JF-Expert Member

  #8
  Jul 12, 2015
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 3,245
  Likes Received: 499
  Trophy Points: 180
  tatizo la ccm huwa hawaachi akiba wanapoongea.mlisema Slaa ni mwizi wa mke wa mtu Leo unaambiwa ya magufuli unaleta uharo wako hapa.
   
 9. Mwanahabari Huru

  Mwanahabari Huru JF-Expert Member

  #9
  Jul 12, 2015
  Joined: Mar 9, 2015
  Messages: 12,725
  Likes Received: 22,130
  Trophy Points: 280
  Hata wao wanajua kwanzia october nchi niyakwetu Ukawa
   
 10. Jay One

  Jay One JF-Expert Member

  #10
  Jul 12, 2015
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 11,711
  Likes Received: 5,590
  Trophy Points: 280
  Nimesha hama Rasmi CCM... niko CDM tokea niliyoyaona Lowassa aliyofanyiwa...

  Moyo wangu, ndugu, marafiki na watu wengi Watanzania, wameshindwa kuvumilia uonevu uliofanywa na CCM dhidi ya Lowassa... hatuwezi vumilia tena...Sasa ni wakati wa maamuzi magumu...kwa vitendo

  Ni UKAWA tu kura.. tuache maneno, jtatu nitakuwa rasmi na kadi mpya ya CDM...!!!

  Dr. Slaa tunakutegemea sasa.... hakuna mwingine
   
 11. Chademakwanza

  Chademakwanza JF-Expert Member

  #11
  Jul 12, 2015
  Joined: Jun 11, 2014
  Messages: 6,350
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Watanzania walishafanya mamuzi sikunyingi sana kuwa ni Dr. Slaa october nikutekeleza tuu
   
 12. A

  Amon Mahamba JF-Expert Member

  #12
  Jul 12, 2015
  Joined: Jul 24, 2014
  Messages: 402
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Mwisho wake ni hapa mkutano huu mwisho wakimaliza tu watamumwaga chini
   
 13. h

  honoget JF-Expert Member

  #13
  Jul 12, 2015
  Joined: Aug 16, 2013
  Messages: 1,720
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  bora ccm ife,ccm ni majambazi.
   
 14. baharia Ar

  baharia Ar JF-Expert Member

  #14
  Jul 12, 2015
  Joined: Dec 1, 2013
  Messages: 831
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 60
  Hivi ccm wapogo!
   
 15. T

  Tata JF-Expert Member

  #15
  Jul 12, 2015
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 5,075
  Likes Received: 916
  Trophy Points: 280
  Wewe ni mtu wa ajabu sana. Yaani unahama chama kwa sababu tu Lowasa kakosa ugombea wa CCM!! Sasa wewe tukuite ni mfuasi wa sera za chama au mfuasi wa mtu mmoja ndani ya chama?
   
 16. Songambele

  Songambele JF-Expert Member

  #16
  Jul 12, 2015
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 3,565
  Likes Received: 1,110
  Trophy Points: 280
  Mara zote nawakumbusha msisahau kuchukua matokeo yenu hiyo Octoba.

   
 17. R

  Rio Tinto JF-Expert Member

  #17
  Jul 12, 2015
  Joined: Sep 18, 2014
  Messages: 761
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 60
  kinana katibu mkuu jembe by Jakaya Kikwete
   
 18. JET SALLI

  JET SALLI JF-Expert Member

  #18
  Jul 12, 2015
  Joined: Dec 1, 2014
  Messages: 1,045
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Ukawa mwendo mdundo kwa ushindi madhubuti mwaka huu ccm mtanyoosha maelezo.
   
 19. JET SALLI

  JET SALLI JF-Expert Member

  #19
  Jul 12, 2015
  Joined: Dec 1, 2014
  Messages: 1,045
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  mnagawana pesa wakati wananchi hawana dawa mahospitalini ,maisha magumu Hakika oktoba mtatutambua yaani CCM mnatugeuza ss mbuzi wa kushangilia hewa na hatupati kitu miaka yote huku ninyi mkinufaika na familia zenu na kugawana rasilimali za nchi,CCM mtambue haikubaliki ,haikubaliki ,haikubaliki kwa namna yoyote ile.Tuonane oktoba ili tuheshimiane.
   
 20. Nas Jr

  Nas Jr JF-Expert Member

  #20
  Jul 5, 2018
  Joined: May 15, 2018
  Messages: 370
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 60
  Hahaha nimerejea hii kauli kwasabu majibu umeshapata.

  Sasa tunaongozwa na Mkuu wa malaika.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...