Kinana ameiva au amechacha?

Kinana ameiva au amechacha?

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,746
Reaction score
25,637
KURUKARUKA kwa maharage ndio kuiva kwake. Katibu Mkuu wa zamani wa CCM, Abdulrahman Kinana, alirukaruka weeee!
Mwisho, Kinana amejitokeza kumuomba radhi Rais John Magufuli kwa maneno aliyotamka dhidi yake.

Kinana amesema kuwa ‘anadhani’ alivuka kiasi baada ya kukereka, kwa hiyo akatamka maneno ambayo hayakuwa mazuri kwa Rais Magufuli, hivyo amemuomba radhi Rais Magufuli binafsi na wote waliokwazika.

Kinana alizungumza nini? Bila shaka ni ile sauti yake iliyovuja akizungumza na aliyekuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye. Hilo ni tukio la Julai 2019.

Mazungumzo ya Kinana na Nape yalifuatia waraka wa malalamiko ambao Kinana aliuandika kwa kushirikiana na Katibu Mkuu mwingine wa zamani wa CCM, Yusuf Makamba. Waraka ni wa Julai 2019.

Kinana na Makamba waliandika waraka kwenda kwa Katibu wa Baraza la Wazee CCM, lakini waliusambaza kwenye mitandao ya kijamii.

Malalamiko yao yalihusu ukimya wa viongozi wa CCM, kipindi ambacho wao walikuwa wakishambuliwa na mwanaharakati mtetezi wa Rais Magufuli, Cyprian Musiba.

Kwa maelezo yao, Kinana na Makamba walidai kuwa Musiba amekuwa akiwashambulia na kuwachonganisha na Mwenyekiti wa CCM na wanachama wengine, kwa kuwapa jina la uasi na wahujumu wa chama.

Walisema kwa mshangao, kwamba wao wakiwa nyumbani kwao, bila mamlaka yoyote, wanawezaje kumhujumu Mwenyekiti wa CCM?

Zikafuata zama za sauti za Kinana na Nape, Makamba na mwanaye Januari, William Ngeleja na Nape, vilevile Bernard Membe, kuvuja mitandaoni wakimteta vibaya Rais Magufuli. Hayo ni mambo ya Julai 2019.

Kisha zikaja zama za kuomba radhi; Nape, Ngeleja na Nape waliomba msamaha Agosti 2019. Makamba, Kinana na Membe walibaki kimya.

Kilichofuata; Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), iliagiza Makamba, Membe na Kinana waitwe kwenye kamati ya Maadili. Baada ya kuitwa, Makamba aliomba radhi na kusamehewa. Hiyo ni Februari 2020.

Kinana hakuomba radhi, akapewa adhabu ya kifungo cha kutogombea nafasi yoyote CCM kwa kipindi cha miezi 18, Membe alifukuzwa uanachama CCM. Hukumu hiyo ilitangazwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Humphrey Polepole Februari 2020.

TUJADILI
Kwa nini Kinana hakuomba radhi muda wote na aombe sasa? Ina maana siku zote hizo Kinana hakuwa amegundua kama alimkosea Rais Magufuli? Tangu Julai 2019.

Kweli, Kinana hata baada ya kukutana na wazee wenzake katika kamati ya Maadili, hakuona kosa lake na kushindwa kuomba radhi mpaka imepita takriban miezi mitatu? Alikutana na kamati ya Maadili Februari 2020.

Hivi karibuni, mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa, alimuomba radhi Kinana kwa matamshi yake aliyowahi kuyatoa bungeni na kwenye mikutano ya hadhara, akimhusisha Kinana na kashfa za ujangili.

Siku chache baada ya Kinana kuombwa radhi na Msigwa, ndio na yeye amemuomba radhi Rais Magufuli. Je, alikuwa anangoja Msigwa amuombe radhi ndipo na yeye amuangukie Rais Magufuli? Au baada ya kuombwa radhi na Msigwa ndio na yeye amegundua uungwana wa kuomba radhi?

Inafahamika kuwa pamoja na tofauti za kisiasa kati ya Msigwa na Rais Magufuli, lakini ni ndugu. Familia zao zimeoleana. Kwa kuzingatia undugu huo, kuna uhusiano wowote wa ombi la radhi alilotoa Msigwa kwa Kinana, kisha Kinana kwa Rais Magufuli? Au imetokea tu?

Raia wa 32 wa Marekani, Franklin Roosevelt alipata kusema kuwa katika siasa huwa hakuna ajali. Ukiona kitu kimetokea, unaweza ‘kubeti’ kwamba hivyo ndivyo ilivyopangwa.

Je, Kinana kaomba radhi kutoka moyoni au ni katii matakwa ya mazungumzo ya pembeni?

Je, Kinana kwa utashi wake aliona umuhimu wa kumwangukia Rais Magufuli au alifuata ushauri wa waona mbali ambao husema "kwani ukimuomba msamaha utapungukiwa nini?" Walimwengu tunafahamiana.

Je, Kinana kuomba radhi inamaanisha adhabu aliyopewa imemuivisha au msimamo wake umechacha?

Mwisho; kuomba radhi ni uungwana bila shaka Rais Magufuli amemsikia na atamsamehe. Amani itawale.




Credit: Luqman Maloti

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hayo yao hata wakichapwa viboko ni sawa tu.Walilea waliotengeneza mfumo wa kuja kuwatesa na kuwadhalilisha hivo wanavuna walichopanda,maana wakiwa kwenye mfumo akili huwa likizo.Walionywa huu mfumo utawaumiza mbeleni waliweka pamba eti sumaye, Lowasa,membe,Mkapa Leo ndio wanaona umuhimu wa katiba mpya.Hata wa Sasa wanaoutesa upinzani si ajabu kesho mfumo utakapowatupa wakajiunga upinzani Kama alivofanya mugabe
 
Kuna kafaili fulani hivi kalipotea pale uhamiaji miaka ileee sasa kamepatikana.
Huyu usijilinganishe naye amekuwa waziri wa kanali wa jeshi .waziri wa ulinzi.spika wa bunge la Africa mashariki ,katibu mkuu wa chama na manager campaign wa ccm wewe kikatuni usijilinganishe naye
 
Aliulizwa swali na mwandishi na akalijibu kwa hekima na busara.
Huo ni uungwana.
 
Kama ni mboga, basi Kinana amechacha. Nachukua nafasi hii pia kumpongeza Mh. Bernard Membe kwa tamko lake la jana. Hakika Tanzania tunahitaji Viongozi wa aina yake! ambao siyo Waoga, Wanafiki, Wezi na Wasio jiamini.

"Ni bora kufa ukiwa umesimama kuliko kuishi ukiwa umepiga magoti". Anayestahili kutukuzwa ma kuabudiwa ni Mungu pekee. Mwanadamu ni mavumbi tu.
 
Huyu usijilinganishe naye amekuwa waziri wa kanali wa jeshi .waziri wa ulinzi.spika wa bunge la Africa mashariki ,katibu mkuu wa chama na manager campaign wa ccm wewe kikatuni usijilinganishe naye
USSR, Hapa umejibu hoja?
Hebu soma vizuri alichoandika, kama kitu hujaelewa kaa kimya kutunza heshima yako
 
Hii michezo yote walengwa ni wapinzani waingizwe "king" na wataingia tu. ccm ni mabingwa kwenye haya mambo.Sa sijui hapa wanaandaa mtego gani? au wanamwandalia njia Membe akagombee upinzani?



amini! amini! nawaambieni mbowe ni ccm aongozaye chadema
 
Hayo yao hata wakichapwa viboko ni sawa tu.Walilea waliotengeneza mfumo wa kuja kuwatesa na kuwadhalilisha hivo wanavuna walichopanda,maana wakiwa kwenye mfumo akili huwa likizo.Walionywa huu mfumo utawaumiza mbeleni waliweka pamba eti sumaye, Lowasa,membe,Mkapa Leo ndio wanaona umuhimu wa katiba mpya.Hata wa Sasa wanaoutesa upinzani si ajabu kesho mfumo utakapowatupa wakajiunga upinzani Kama alivofanya mugabe
aisee kwahiyo hadi lodilofa anasoneshwa namba?
 
Hii michezo yote walengwa ni wapinzani waingizwe "king" na wataingia tu. ccm ni mabingwa kwenye haya mambo.Sa sijui hapa wanaandaa mtego gani? au wanamwandalia njia Membe akagombee upinzani?



amini! amini! nawaambieni mbowe ni ccm aongozaye chadema
aisee kama una make_sence hivi
 
Naona mnaongea utumbo tu humu kwanini hamjadili swala la mbowe kuwa mwenye kiti wa maisha...mnamjadili kinana uyo ndio anawauma sana....hamna cha mana
 
aisee kwahiyo hadi lodilofa anasoneshwa namba?
Hata jiwe nae atasomeshwa na ajae kwa mfumo wa katiba ya chama chao,maana wanaoisoma Sasa hata wao walikuwa na nafasi ya kufanya mabadiliko wakaweka pamba.
 
Mjue Msigwa naye alimuomba Radhi Kinana....history lazima iwekwe sawa. Hapajawahi kutokea wapinzani kuwaomba Radhi wanachama au viongozi wa CCM walio bado Ni wanachama wa huko. Pengine Kinana alitaka kuvuka gepu kuja huku akawahiwa kwa maelekezo
 
Kuwa muungwana siyo dhambi amefikiria aliyoyafanya na hakuna alichomsema jpm akaona hanabudi kuomba msamaha! Atulie mwenzake afanye kazi amalize na watakuja wengine
 
Back
Top Bottom