kuna jambo moja wapambe wa lowassa walijidnaganya sana,wao walidhani lowassa ni mkubwa kuliko chama na chama ndio kinamtegemea kumbe hali imedhihirika ni tofauti sana kwanza baada ya kuondolewa kwenye kamati kuu na nec kubariki maamuzi ya kuivunja kamati kuu na kuiunda upya ambapo jina lake halikurudi,hilo lilikua pigo la kwana kwa wenye akili tukajua yametimia.
Ila haya maamuzi ya nec ya kuwaondoa wastaafu wote kwenye kamati kuu na uamuzi wa kutenganisha kofia ya ujumbe wa nec na ubunge ndio maamuzi magumu na mabaya kwa harakati za lowassa kupita yote kupata kutokea,hii maana ni kwamba lowassa hana nguvu tena ndani ya ccm,kabaki kama nyoka wa kibisa ambae anatisha tu kwa kuwa ni nyoka jina lakini hana madhara yeyote.Pia wapambe wake kama peter serukamba,januari makamba na yeye mwenyewe sasa watalazimika kuchagua ama kugombea ubunge au ujumbe wa nec.
Na kwa maamuzi hayo mwenyekiti wa ccm sasa anakua na nguvu kama nyerere kipindi akiwa mwenyekiti.