lisemwalo lipo,kama halipo linakuja. Acha tuongee tu,hawa jamaa wanajua kuchapana bakora tu, wametuharibia nchi kwa udhaifu wao. Kwa nn kila wakiwepo wao nchi inakuwa na madeni kibao na hatuon hizo fedha wanafanyia nn na zinapelekwa wapi na magenge yao ya ujambazi.
Mnyisansu, usijali kubezwa, kudharauliwa na kutukanwa kwa jambo ambalo litakuja kutokea, likishatokea ndipo utaheshimiwa!.Hapa JK anaandaa mazingira ya kumwingiza mwislam ikulu 2015!
Jesuit nadhani hii sio mara ya kwanza mimi kukuambia jina lako zuri ila mawazo yako!. Kama jina hilo limetokana na wale ma Jesuit Fathers kama wanaoendesha shule za Loyola duniani kote, nimekusamehe sio kosa lako ni effect ya free masonry kwako kwa sababu ma Jesuit Fathers ni ma freemasons wakubwa!.Kumbe na wewe Pasco uko kwenye hili gonjwa la kumpenda mtu au kumchukia kwa sababu ya DINI yake? Basi ukombozi wa Tanzania uko mbali!
Yote ya yote wakati mwingine uwa nakubali maneno ya marehemu baba yangu kuwa kila jambo linasababu yake,hakika Tanzania kumchagua Kikwete kwa lolote au namna yoyote haramu au halali amefanya ambyo ni nadra sana mtu mwingine yeyote angeyafanya bila kumwaga damu kwa maelfu ya watu.Akiongea kwa jazba,Ngombale alikaririwa akipinga kwanza,kuundwa kwa Baraza la ushauri ambalo litakua na viongozi wakuu wastaafu kwa maana ya marais na mawaziri wakuu wastaafu akidai hatua hiyo itafanya chama kikose watu wa kukilea japo haikueleweka alikua anamaanisha nini!
Pia bwana kingunge alipinga mpango wa kuzuia wabunge kujilimbikizia vyeo vinavyoambatana na posho pia kwa kuwa wajumbe wa NEC.Tayari wabunge pia ni madiwani katika halmashauri wanazotoka na wanahudhuria vikao kama kama madiwani wengine.
Kuhusu mpango wa kuzuia wabunge kuwa wajumbe wa NEC, Ngombale alisema, Huwezi kufanya haya kama unakitakia mema chama hiki. Labda kama mtakuwa mnathibitisha madai kuwa kuna agenda iliyojificha.
Akiongea kwa jazba kali bwana Ngombale alisema, Naomba mniweke kwenye kumbukumbu kwamba nimelipinga jambo hili. akaendelea kufoka kwa kudai bila kuthibitisha kwamba utaratibu wa kupata wajumbe wa NEC kutoka wilayani eti utakuwa na athari kubwa kwa chama hicho kwenye siku za usoni; kwani utakifanya chama kuwa na makundi makubwa ya ugomvi na visasi!!!
Katika hali inayoonyesha kama walikua wamejipanga kabla ya bwana Ngombale kuchangia, Peter Serukamba , mjumbe wa NEC na mbunge wa Kigoma Mjini,nae alisimama na kupinga utaratibu mpya wa kutaka kuwaundia chombo maalum viongozi wakuu wastaafu na kuwatumia katika kukishauri chama.
Lakini hoja dhaifu za Peter akifuatiwa na Kingunge,zilizimwa na Mh.Abdulrahman Kinana aliyepigilia msumari wa mwisho kwa kueleza kuwa hata wastaafu wenyewe wamekubaliana na jambo hili. iweje nyie ndio mpinge kwa nguvu leo??
Huku akimuangalia rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi, Kinana alisema, Au siyo Mzee Mwinyi. Mwinyi aliitikia kwa kutikisa kichwa kuashiria kukubaliana.
.
Hapa JK anaandaa mazingira ya kumwingiza mwislam ikulu 2015!
Kwa staili hii EL mbuyu unaokitesa chama unakuwa ushang'olewa
sidhani kama CCM ina weza jifunga hicho kitanzi kumpendekeza Mzanzibari kuwa mgombea Urais 2015.Hoja ya Mzanzibar kuja kututawala huku haina mashiko kamwe.
kajifunze kwenye katiba kama huwa tunaangali dini kwenye kuchagua Rais!!
Unajua kwa nini nakupenda mkuu wangu.. Ni kwa sababu unazungumza Hali halisi - ukweli wa fikra za Wadanganyika ambao wengi wanapenda sana kuuficha japokuwa nyoyo zao zinaweka madai haya na hawatapenda iwe kinyume. Hakuna swala nchini lisilotazamwa kwa picha ya dini ama hizi nchi mbili zilizoungana japokuwa la Ukabila ni hafifu lakini nalo lipo.Mnyisansu, usijali kubezwa, kudharauliwa na kutukanwa kwa jambo ambalo litakuja kutokea, likishatokea ndipo utaheshimiwa!.
Kwenye CCM hakuna mwenye uwezo wa kuizuia kasi ya EL kuutaka urais kama ilivyokuwa kwa Sitta kurejea kwenye uspika. Kilichofanyika ni ku device suicidal mechanizim ili kuua ndoto jumla!. Namna pekee ya kumzuia Sitta ilikuwa ni kujenga hoja ya gender eti safari hii ni zamu mwanamke!. Sitta kwisha kazi!, hata huo uwaziri kapewa tuu kama kifuta machozi!.
CCM inaweza kuizima ndoto ya EL kwa kuutumia hoja ya baada ya bara kuushika urais wa muungano kwa vipindi viwili mfululizo "sasa ni zamu ya Zanzibar!". Hii inamaanisha atakayepitishwa ni Dr. Shein na ni Muislam!.
Kitu pekee kitakachoizuia CCM kumpitisha Shein au kutoa zamu kwa Zanzibar ni hoja mbili tuu za uwezekano wa mgombea wao kushindwa iwapo
1. Wapinzani wakuu wataungana kumsimamisha mgombea mmoja strong prefarably Dr. W. Slaa.
2. Matumizi ya siasa chafu zenye sumu ya udini kuwa haiwezekani atoke Muislamu, aje Muislamu, hivyo Wakristu waipigie CCM kura za chuki, hivyo uwezekano wa mgombea wao kushindwa!.
Hoja hizo ndizo pekee zitaifanya CCM kumuepuka Mzanzibari hivyo watawarudia wagombea wa bara wenye posibility ya kuuzika kumshinda mgombea wa upinzani!. Na hapa ndipo jina la EL litakuwa top of the list!.
mkuu badilika kidogo,naona sasa kila mtu humu amekujua mwanzo ilikua ni mimi tu sasa hata mtoto mdogo anajua kwamba wewe ni mlutheri kupita kiasi na ungependa safari hii rais awe mlutheri mwenzake,lakini sisi tunataka rais atakaekidhi matarajio ya watanzania kuijumla sio matarajio yako wewe na walutheri wenzako pekeenu na lowassa kaligundua hilo ndio sasa hivi yuko busy na wakatoliki na waislam,nyie kaona mtamurabia mipango yake kwanza hamna political hapa kama waislam na wakatoliki hapa tanzania,huo ndio ukweli japo ni mchungu.It is a matter of time! Mtayakumbuka maneno yangu.
Kwa staili hii EL mbuyu unaokitesa chama unakuwa ushang'olewa
Naaam.... Nice thinking ability.... mie nshaliona hili quickly kwani EL anakubalika kichama mnooo hadi makanisani.... So wazee wamekaa referee akiwa Mkuu wa kaya, kufanya mabadiliko makubwa kichama then EL hatakuwa na nguvu,
yaani EL atakuwa kavunjwa vunjwa, udini upo tu hasa pale AK alipo mwambia AU SIO MZEE MWINYI NA MWINYI AKATIKISA KICHWA KUKUBALIANA NA MABADILIKO MEANING LABDA MKAPA NA KINGUNGE HAWAKUJUA WHAT WAS GOING ON .... KUMBUKA SUMAYE + MKAPA LAST MEETING ya NEC WALIONYESHA WAZIII KUMSUPPORT EL HASA PALE EL ALIPOSEMA MWAMBIA JK KAMA SIO BUSARA ZA MZEE MKAPA LEO USINGEKUWA HAPO akikumbushia shutuma JK alizoundiwa kutoka Znz, NA MKAPA PLUS KINGUNGE PLUS SUMAYE WOOOTE WALIMKUBALI MNO EL, KWA
MAANA HIYO JK KAJIBU MAPIGO KWA EL THIS TIME, na Kinana plus Mwinyi wapo na JK, sasa unaona jinsi mchezo unachezwa..... Kingunge kabaki mdomo waziiii kwa kushangaaaa JK anapiga mpira ka Barca but politically.... EL next time tutamwona kajipanga vipi.... So MKUTANO ULIOPITA JK kashinda.... But ule wa awali kabla ya haya mabadiliko EL kashinda vibaya... So let's wait next NEC meeting tuone EL kajipanga vipi? EL is a powerful TYCOON, not an average fighter just to remind you... anaweza kuwakimbiza kambi ya JK, kina Nape ni vitoto tu na ujue nasema hivi kumbuka HATA KILE KIKAO CHA NEC KABLA YA HIKI CHA MABADILIKO YA MARAIS WASTAAFU JK MWENYEWE KASEMA KUMSUPOTI EL KUWA ANAYESEMA EL FISADI ASEME SASA NA USHAHIDI ALETE LA SIVYO KAMATI YA MAADILI ITAWACHUKULIWA HATUA WALIOKUWA WAKIMCHAFUA EL akimaanisha Nape na Sitta ila kumbuka alitamka haya BILA KUPENDA NI NGUVU ZA EL ZILIZIDI KTK KIKAO, ilibidi tu aseme hivyo that time, ila ndio akajipanga kuja na mabadiliko huku Tycoon Kinana akiwa upande wake ...... Let's watch this next time.... Hapa JF jaribuni kusearch & dig deep kidogo kujua hawa watu.... ..c u.. next time... @ take off ....
Hata Kanisa likimtangaza utakatifu basi ataitwa Saimt Julius, kwa binadamu mwenye jina Nyerere hakuwahi kuwa mkristo.Are you serious dude? St. Nyerere aliangamiza uchumi wa nchi hii kwa mikono yake beyond repair! Mpaka Mwinyi na Salimu walipokuja na sera za kufufua uchumi! Au wewe ulikuwa unachapa divai tu?