Kinana afichua mbinu za kikundi cha UKAWA katika ziara Mkoani Manyara

Si mmesema anaenda kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM? Sasa ya UKAWA yanatoka wapi tena? Hivi na wewe, utaacha lini kutumia Mekako na Diprosoni na maji ya betri?

Kweli UKAWA ndiyo habari ya mjini.
 
Yaani wewe bongolala kweli nani kasahau uhalifu wa huyu msomali kwa tembo wetu.......?? Pocha ni pocha tu asitusahaulishe machungu ya ndovu wetu aisee
Ndugu, Watanzania walio wengi hawatambuani kwa kutumia makabila, otherwise utakuwa unasumbuliwa na fikra za kibaguzi ambazo kwa sasa dhambi yake inavitafuna baadhi ya vyama vya siasa mpaka vimeamua kulikimbia jina lake linalotambuliwa na msajili wa vyama vya siasa na vimeamua kujificha kwenye mwanvuli wa kikundi kinachoitwa UKAWA,
 
Si mmesema anaenda kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM? Sasa ya UKAWA yanatoka wapi tena? Hivi na wewe, utaacha lini kutumia Mekako na Diprosoni na maji ya betri?

Kweli UKAWA ndiyo habari ya mjini.
Ndugu, Ni kweli UKAWA ni habari ya mjini ndiyo maana hata viongozi wa hicho kikundi wanaenda mijini pekee kufanya mikutano.

CCM ni habari ya Kijijini na ndiyo maana viongozi wake wako vijijini wakihimiza maendeleo ambako more than 70% ya Watanzania wanaishi.

Mikutano ya hadhara ni moja ya sehemu ya ajenda katika ziara za viongozi wa CCM.
 
Ndugu, Wananchi wanachokitaka na kukihitaji huwa kinakuwa manifested kwenye sanduku la kura kupitia sera za vyama na Ilani za Uchaguzi.

Sihitaji kukukumbusha nini wananchi wamekuwa wakihitaji kuanzia mwaka 1995 mpaka leo.

Katibu Mkuu, Kinana anakifahamu kile ambacho wananchi wanakihitaji ndiyo maana CCM imeaminiwa na wananchi kuongoza taifa lao.

Imeaminiwa na nani mpuuzi wewe? Yapo wapi mapendekezo ya tume ya Jaji Nyalali au Kisanga yaliyofanyiwa kazi ili kuweka mazingira sawa na ya haki kiushindani? Kama mnakubalika hivyo kwa nini miaka nenda rudi munaogopa kuwepo tume huru ya uchaguzi??? Kama huwa mnakubalika inakuwaje mwahadae wananchi hasa vijijini wasio na uelewa kwa wali,kanga,tshit,vilemba vya kijani na kununua shahada zao ili wasipige kura??? Mmezoea vya kunyonga vya kuchinja hamviwezi!
 
KINANA AFICHUA MBINU ZA UKAWA

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana amesema Katiba sio kichochoro kwa wapinzani kuingia Ikulu.

Alisema wenye uwezo wa kuwaweka madarakani ni wananchi, lakini sio Katiba, kwani haipigi kura.

Kinana aliyasema hayo juzi wakati anahutubia wananchi wa Kateshi mkoani Manyara ambapo aliyafananisha madai ya Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), Tundu Lissu kuhoji uhalali wa saini ya Hayati Baba wa Taifa Julius Nyerere na Abeid Karume kwenye Hati ya Muungano ni sawa na mtoto kuuliza uhalali wa cheti cha ndoa cha wazazi wake.

Pia aliongeza kuwa, madai ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kutaka Serikali Tatu ni ndoto wanazoota kuwa huenda Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kikaongoza Serikali ya Tanganyika na Chama cha Wananchi (CUF) kikatawala Zanzibar.

“Katiba haiweki watu madarakani, wala Katiba haipigi kura, kwani wanaopiga kura ni wananchi.Lakini pia CCM haikatai Katiba mpya kama wapinzani wanavyodai... CCM wanatumia wingi wao bungeni kuweza kuamua Katiba wanayoitaka.

“Kwa nini tusijivunie wingi wetu wakati wananchi ndiyo wametupeleka bungeni na kuiweka madarakani Serikali ya CCM? Halafu duniani kote wachache wao wanasikilizwa, lakini wengi ndiyo wanapewa,” alisema Kinana.

Kinana alisema madai ya Lissu kudai saini za Nyerere na Karume sio halali, hizo halali alizionea wapi wakati yeye alikuwa mtoto mdogo na kufananisha kitendo hicho na baba mwenye watoto na wajukuu baadhi ya watoto wake kudai uhalali wa cheti cha ndoa na mkewe.

“Madai ya wapinzani hasa Tundu Lissu kudai Hati ya Muungano si halali ni sawa na mtoto kumuuliza baba yake ambaye tayari ana wajukuu, uhalali wa ndoa yake na mama yao. Lakini yeye anasema saini hizo sio halali, saini halali aliziona wapi wakati huo anasoma shule ya msingi. Lakini pia UKAWA wanadhani kukiwa na Serikali tatu, CHADEMA wataongoza Tanganyika, CUF Zanzibar na Serikali ya Muungano itaachiwa CCM.

“Halafu wananchi, suala la muungano kwenu sio muhimu, umuhimu ni kupata huduma za jamii kama maji, elimu, afya na barabara.

"Nawashauri wananchi wa Hanang’ achaneni na siasa zisizo na tija kwenu, bali fanyeni kazi muweze kujiongezea kipato, hata kama Katiba mpya itakuwepo haiwezi kubadilisha maisha yenu kuwa mazuri bila kufanya kazi,” alisema.

Kinana is talking the reality and the reason for CCM being against three tier country system of governments. Unfortunately he pimp himself and his party in the thought that they will lead in the Union governmen, teh teh teh. How come if the majority would have given the opposition the leadership to the federal states and not the federation itself? Obviously the Federal Government will be having a GNU structure.

Hongera Kinana for revealing the 'secret' why CCM does not want 3 government system!!! :clap::clap: Ritz, FaizaFoxy, mfumo, Polite
 
Last edited by a moderator:
Ndugu, Wananchi wanachokitaka na kukihitaji huwa kinakuwa manifested kwenye sanduku la kura kupitia sera za vyama na Ilani za Uchaguzi.

Sihitaji kukukumbusha nini wananchi wamekuwa wakihitaji kuanzia mwaka 1995 mpaka leo.

Katibu Mkuu, Kinana anakifahamu kile ambacho wananchi wanakihitaji ndiyo maana CCM imeaminiwa na wananchi kuongoza taifa lao.
Nape hujambo povu linakutoka
 
Ukawa ni ugonjwa Wa fikra kila siku wanatoka na kiroja kipya ni watu wanaowadaa watanzania hawana lolote

Sasa ndugu mbona wana ccm wote ni maziro brain hivi? Hebu kama wewe nawe hutumii tumbo na makalio kufikilia ni mbinu gani alizofichua hapa huyu mtaalamu wa twiga na tembo? CCM kuanzia baba,mama,mtoto mpaka kitukuu wezi,ukoo wa panya
 
Kinana is talking the reality and the reason for CCM being against three tier country system of governments. Unfortunately he pimp himself and his party in the thought that they will lead in the Union governmen, teh teh teh. How come if the majority would have given the opposition the leadership to the federal states and not the federation itself? Obviously the Federal Government will be having a GNU structure.

Hongera Kinana for revealing the 'secret' why CCM does not want 3 government system!!! :clap::clap: Ritz, FaizaFoxy, mfumo, Polite

The reason and only reason for Tanganyika, or rather CCM, to keep on refraining Zanzibar to be sovereign is and will stiil remain as recently preached in the church by our dear Mr. Lukuvi. Nothing more nothing less.

Everything else is just another reason.
 
Ndugu, Mimi siko hapa kubishana. Kama wewe uko hapa kujenga ubishi, basi mimi siyo mmoja wao.

Kila mbunge aliyeko bungeni yuko kisheria na wale ambao walishindwa katika chaguzi walishindwa kisheria. Kama unajenga hoja kwa kutumia hisia, basi hilo,ni tatizo lako ambalo halitambuliwi hata kisheria. Ndiyo maana nikakuambia huwezi kusema umeibiwa kura wakati milango ya mahakama iko wazi.

Huwezi kujadili 'ujinga', otherwise utakuwa hufahamu unachokifanya. Vile vile huwezi kujadili 'ujinga' na kudai unauweka hadharani ili wengine pia wauelewe kama vile unaowawekea hawafahamu kama unaojadili ni ujinga. Kujivika kazi ya uchambuzi wa hoja ya 'kijinga' ili uweke hadharani bila kuombwa kufanya hivyo ni dalili ya kuwaingiza wananchi wengine kwenye box la fikra zako.

Last time I checked I still had my freedom of expression!
 
Imeaminiwa na nani mpuuzi wewe? Yapo wapi mapendekezo ya tume ya Jaji Nyalali au Kisanga yaliyofanyiwa kazi ili kuweka mazingira sawa na ya haki kiushindani? Kama mnakubalika hivyo kwa nini miaka nenda rudi munaogopa kuwepo tume huru ya uchaguzi??? Kama huwa mnakubalika inakuwaje mwahadae wananchi hasa vijijini wasio na uelewa kwa wali,kanga,tshit,vilemba vya kijani na kununua shahada zao ili wasipige kura??? Mmezoea vya kunyonga vya kuchinja hamviwezi!
Ndugu, mimi kuwa mpuuzi hakuondoi ukweli kuwa CCM ina wabunge zaidi ya 250 wanaotambuliwa kisheria ambao kwa sasa wanatunga sheria ambazo ni lazima uzitii ukiwa nchini na kuendesha maisha yako ya kila siku ndani ya sheria hizo.

Haya mambo mengine ni kelele tu za kisiasa ambazo mtu yeyote anaweza kuzungumza kulingana na utashi wake.

CCM haiingii kwenye chaguzi peke yake na kwa mantiki hiyo, huwezi kusema mazingira hayako sawa wakati kuna vyama vinakubaliana na political playing field katika chaguzi.
 
Kinana atawanyoosha tu make wanajifanya wamepinda lakini kwa kinana visilani vitawaisha hata iweje hili taifa siyo la kupotoshwa na kuchezewa na ukawa ni tifa la watu wanaojua wanafanya nini.
 
Hivi huyu Mbunge wa Babati aliyeshika hicho kifaa eti anajenga ni kweli huwa kinashikwa hivyo? imefikia wakati sasa CCM muache usanii kwa kutumia picha

IMG_1152.JPG

Kinana akiasaidiana na Mbunge wa Babati Mjini, Kisyeri Chambiri kujenga jengo la Zahanati ya Malangi, katika Kata ya Maisaka, Babati.
 
Si mmesema anaenda kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM? Sasa ya UKAWA yanatoka wapi tena? Hivi na wewe, utaacha lini kutumia Mekako na Diprosoni na maji ya betri?

Kweli UKAWA ndiyo habari ya mjini.
Hawa ukawa wanavuruga mipango ya maendeleo hivyo lazima wakemewe make kutwa wanaandamana na kuleta usumbufu kwa wafanyabiashara.
 
Hivi huyu Mbunge wa Babati aliyeshika hicho kifaa eti anajenga ni kweli huwa kinashikwa hivyo? imefikia wakati sasa CCM muache usanii kwa kutumia picha

IMG_1152.JPG

Kinana akiasaidiana na Mbunge wa Babati Mjini, Kisyeri Chambiri kujenga jengo la Zahanati ya Malangi, katika Kata ya Maisaka, Babati.
Unataka ashike kama unavyoshika bakuri la gongo.
 
Sikutegemea...! Kumbe kinana bado mtoto mdogo sana yaani hajui hata kazi za katiba katika inchi. Hebu tujaribu kufuta katiba yetu ya sasa na tuishi bila katiba halafu tuone kama itawezekana. Kinana ni mpumbafu na wote wanaomsikiliza ni mbumbumbu. Huyo kinana akiwa rais anaweza kufuta katiba maana hajui umuhimu wake mjinga mkubwa huyo. Yaani ndivyo anavyowadanganya? Na mkijaribu kuyafuata maneno yake tu wooote mtakuwa maahila.
 
Kwa watu wanaoelewa maana ya katiba na umhimu wake kwa nchi changa kama zetu na zenye wizi na ubadhirifu mkubwa wa mali ya umma, hawawezi kuzunguka nchi nzima wakiwahubiria wananchi kwamba hatuhitaji katiba na eti katiba haileti maendeleo. Naona mbinu hii ya kutumia uelewa mdogo wa watz wengi kama kigezo cha kupata short cut ya mambo. Ni kweli katiba haileti maendeleo direct lkn imagine katiba yenye sheria ambazo hazina meno; Fedha za umma zikiibwa hakuna wa kushtakiwa, fikiria fedha za rada pamoja na UK kutanabaisha kweli kulikua na wizi na chenji ikarudi lkn hakuna mtu alishughulikiwa vilivyo, <br><br>Katiba haileti maendeleo directly lkn fikiria watendaji wasiowajibika mpaka mambo yanaharibika huku wakisababisha hasara kubwa kwa nchi lkn hakuna jinsi, yote sawa tu, fikiria tume ya uchaguzi inayoteuliwa na mtu mmoja ambaye nae ni mwanasiasa, akiamua kuweka hisia za chama chake ndani yake itakuwaje.<br>Hii kubadilisha mawaziri na watendaji wa taasisi kila kukicha kisa utendaji mbovu, hakuna sheria za maadili ya uongozi wa umma ndio umaskini wenyewe, imagine hao wanaotemwa nafasi zao wanalipwa stahiki na mafao yao, hivi idadi hii kubwa hivi ya wanaohitaji haya yote sio umaskini????? sherehe tu za kuapishwa kwa watendaji kama mawaziri mbona ni umaskini tosha tu, hiyo bajeti mbona inatosha kununua madawati shule moja sio mbaya. Kwa kifupi katiba mbovu inajenga mfumo mbovu, mfumo mbovu unajenga watu wabovu, watu wabovu wanafanya kila aina ya uovu ndani ya nchi
 
Back
Top Bottom