Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia Wakili wake, Godfrey Wasonga, kimeiomba mahakama ya Rufaa Dodoma kuifuta kesi ya kupinga ubunge wa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (CHADEMA) iliyofunguliwa kwa shinikizo la Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
Kwa mujibu wa wakili huyo, sababu ya kuomba kufutwa kwa kesi hiyo ni kutokana na walalamikaji wote kujitoa na kuapa mahakamani kuwa hawapo tayari kuendelea na kesi hiyo.