Pale inapotokea shughuli fulani ya kisiasa zinapigwa marufuku kwa vyama vyote halafu chama kimoja kinaendelea kufanya hilo lililokatazwa.
Yanazuiwa Mahafali ya wanafunzi wanaoshabikia chama kile lakini yanaruhusiwa ya wale wa chama hiki. Huu ubaguzi ndio unaolimaliza Taifa hili.
Inazuiwa Mikutano ya vyama vya siasa, inatumiwa nguvu kubwa kuwadhibiti wale wanaokiuka katazo kutoka upande ule, lakini wanaachwa wa upande huu wafanye wanavyotaka. Huu ubaguzi ndio unaotuingiza matatizoni, mambo haya yanaonekana na ni hatari jamani..
Mkutano Mkuu wa chama hiki unafanyika wakati kukiwa na katazo la kuzuia mikutano ya kisiasa kwa vyama vyote. Katazo hilo linakuwa ''suspended" siku moja kabla ya Mkutano. Halafu linarudishwa tena baada ya kukamilika Mkutano. Yawezekana litaondolewa tena kukiwa na haja ya kufanya mkutano. Haya mambo hayafai na ndio yatakayotuletea matatizo.
Kama tunataka kujenga Taifa moja hatupaswi kufanya ubaguzi wa aina yoyote kwa wananchi. Tusiweke matabaka miongoni mwetu. Kusiwe na watu wenye haki zaidi kuliko wengine. Tusione mtu ambaye hakubaliani na mawazo yetu kuwa ni mkosaji na hana haki ya kutenda mambo kadhaa.
Leo hii ni nadra sana kuona wale wa upande huu wakiburuzwa Mahakamani kwa makosa ambayo tunaona wale wa upande ule wakihenyeshwa Mahakamani kila kukicha. Haya mambo yanaonekana jamani watu wapo kimya tu lakini wanajua.
Mfano mdogo tu, jaribu kupita kwenye kurasa zao za mitandao ya kijamii, utakumbana na matusi wakitukanwa watu flani flani wa upande ule lakini hutasikia wakihojiwa popote.
Haya mambo jamii inayaona, na niwaambie tu, wengi hawayakubali lakini wanaamua kunyamaza kwa kuwa wameshajua upo ubaguzi na ukionekana hauko upande wao au ukiwapinga, uko matatani.
Nadhani kama Taifa tunahitaji kutafakari masuala haya. Nawahakikishia tunaweza tukawadhibiti sasa wasifanikiwe kufanya hicho wanachotaka kukifanya lakini kama na sisi tutaendelea kufanya haya tunayoyafanya, basi ni muda tu, tutarejea tena hapa hapa.
Mambo haya yakiendelea kufanyika kwa muda mrefu zaidi, basi tutakuwa tunaliingiza wenyewe Taifa letu matatizoni.
Niwambie tu, sababu za wazee wetu zamani kupigania uhuru hazitofautiani sana na haya tunayoyaona leo.
Wazee wetu walibaguliwa, walinyanyaswa, walionekana hawana hakli ya kufanya mambo flani flani ndani ya Taifa lao. Walivumilia hadi wakachoka. Wakatumia kila mbinu walizojaliwa na Mwenye ez Mungu kujikomboa.
Hakuna tofauti sana na sasa.
Swala hili si dogo kama wengi wanavyodhania, hapa ndio tunapohitajika kuonyesha busara zetu, tuumalize mgogoro huu tukiwa wamoja, tuachae kuligawa taifa kwa misingi ya vyama vyetu.
Ajenda yetu iwe moja, kujenga Taifa moja, tuwe wamoja katika kutekeleza hili. Tukubali kukosolewa pia tukubali mawazo ya wenzetu ili kufanikisha lengo letu moja.
Tusidhani kama sisi tuna haki miliki ya Taifa. Kiburi si maungwana, tutumie matukio yaliyotokea kwa wenzetu kama funzo. Tusirudie makosa.