Tuko
JF-Expert Member
- Jul 29, 2010
- 11,178
- 7,320
Hili jambo kuwa kura za ubunge na uraisi zitahesabiwa na kubandikwa vituoni lisitupumbaze tukaachia goli la mkono kirahisi
Hali huwa hivi
1. Kura zikishahesabiwa vituoni, masanduku hufungwa kwa kufuli mawakala wote wakiona.
2. Masanduku husafirishwa na magari ya halmashauri kupelekwa point moja ya kuhesabia tena pale halmashauri.
3. Ikumbukwe kuwa magari yanayosafirisha kura mara nyingi hayabebi mawakala, Huwa ni gari moja linazunguka kwa vituo kadhaa likikusanya masanduku
4. Masanduku yakishafika kwenye ukumbi wa kuhesabia huko halmashauri, hupokelewa na mkurugenzi wa halmashauri
5. kazi ya kuhesabu UPYA kura za ubunge na uraisi hufanywa tena pale halmashauri. Hapa wanakuwepo wakala mmoja mmoja kwa kila chama chenye mgombea wa uraisi, na wagombea ubunge peke yao.
6. Mbunge hutangazwa kutokana na idadi ya kura zilizohesabiwa PALE HALMASHAURI, sio za vituoni
7. Matokeo ya kura za uraisi hutumwa na mkurugenzi wa wilaya, ambapo ni yale yaliyohesabiwa pale halmashauri, sio ya vituoni
8. Ujumlishwaji wa kura zilivyohesabiwa vituoni unaweza kufanywa, lakini final say ni kura zilizohesabiwa halmashauri.
Kama kuna mtu anaplan kuzuia goli la mkono atafakari yafutayo;
1. Namna ya kuhakikisha masanduku yaliyotoka vituoni, ndiyo yaliyofika halmashauri
2. Namna ya kuhakikisha masanduku yaliyotoka vituoni hayakufunguliwa njiani
3. Namna ya kuhakikisha hakuna masanduku za ziada yataingia kwenye ukumbi wa kuhesabia pale halmashauri
Tahadhari; Mara nyingi umeme huwa unakatika au unazima kwenye ukumbi wa kuhesabia kura pale halmashauri na kutoa mwanya wa GIZA (bebeni tochi). Kukiwa na sintofahamu yeyote pale halmashauri na mawakala/wajumbe wakahoji, huambiwa wanaleta vurugu, hukamatwa na askari wanaokuwa wamemwagwa pale, na hivyo ukumbi huwa "free" baada ya hao kukamatwa.
Tutaendelea kutafakari...