Kinachotokea Iringa, Tafsiri Yangu...

Kinachotokea Iringa, Tafsiri Yangu...

maggid

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2006
Posts
1,084
Reaction score
1,250
Ndugu zangu,

Leo saa mbili na nusu asubuhi nilifika Jengo la NSSF nikitokea kufanya jogging yangu ya asubuhi. Nilifika hapo kuwahi kununua magazeti.

Hali ilikuwa shwari kama ilivyo kawaida ya Iringa Jumapili asubuhi. Kunako saa tatu asubuhi nilipokuwa nyumbani nikisoma magazeti, ndipo niliposikia mlio wa kwanza wa bomu la machozi. Idadi yake ikaanza kuongezeka.

Nikiwa na kamera yangu nikajisogeza hadi katikati ya mji kufahamu zaidi kinachotokea. Nilichokiona ni vurugu kati ya Wamachinga na Jeshi la Polisi.

Tatizo?

Ni dogo sana, lakini linakuzwa kwa vile siasa imepelekwa mbele badala ya kutanguliza hekima na busara. Kwa kufuatilia suala la Wamachinga kufanya biashara eneo la barabarani pale Mashine tatu naamini kabisa, kuwa Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Msigwa angeweza kuepusha hali inayoendelea sasa kwa kuwasihi Wamachinga watii kwanza amri ya Manispaa, na yeye, kama Mbunge wao, kujiingiza kwenye mazungumzo ya dhati na wenzake kwenye Halamshauri ya Manispaa ya Iringa katika kutafuta ufumbuzi wa suala hili. Na hiyo ndio siasa. Siasa ina maana ya majidiliano endelevu badala ya kuhamasisha matumizi ya nguvu au vurugu pale milango ya majadiliano ingali wazi.

Kinachotokea Iringa kwa sasa ni doa kubwa kwa mji wetu wenye sifa ya muda mrefu ya utulivu. Kina athari kubwa kiuchumi pia. Pale Iringa mjini nilichokiona leo ni kama mji ulio katika mapigano ya kivita. Watu ni wachache na wenye hofu.

Biashara nyingi zimesimama. Niliziona Daladala zikitoka Kituo cha Miyomboni bila hata abiria, watoke wapi? Wakati kwa sasa walio nje ya mji wameambiwa na jamaa zao walio katikati ya mji kuwa wasijaribu kufika mjini, kwamba hali imechafuka.

Nimeongea na mwuza nyama ya bucha aliyeniambia kuwa mgomo wa Daladala wa hivi karibuni ulimfanya apate hasara kubwa kwenye biashara yake ya nyama kwa vile wateja wake wengi wanatoka nje ya mji. Na anachokiona leo ni hasara nyingine kwa vile hakutakuwa na biashara nzuri. Je, ni wafanyabiashara wangapi watakaoathirika na hali hii ya leo?

Na kwa kuwa mkweli, kisiasa kinachotokea Iringa kwa sasa kinaweza kuwa na athari hasi kwa Mchungaji Msigwa badala ya kumjenga kisiasa, kwani, wengi niliozungumza nao katikati ya mji wanamwona Mchungaji Msigwa kuwa ni mtu ambaye angeweza kuiepusha hali hii kama asingeyatumia majukwaa ya siasa kuwahamasisha Wamachinga kuendelea kufanya biashara, na hivyo, kutokutii amri ya Manispaa.

Mchungaji Msigwa ni rafiki yangu, muda mfupi uliopita nimempigia simu. Imeita bila majibu. Mmoja wa watu wake wa karibu ameniambia yuko kwenye Harambee pale Tumaini University.

Kama Mchungaji Msigwa angejibu simu yangu, basi, ningemwambia haya ninayoyaandika hapa.

Maggid Mjengwa,
Iringa.
0754 678 252
MjengwaBlog :: Habari, Picha, Matangazo na Matukio






 
poleni sana wanyalukolo kikubwa mkae nae chini mumueleweshe kwamba kakosea huo ndio ubinadamu na yeye aombe samahani kwa wanaIringa hiyo itakuwa ni busara zaidi na tushukuru kwamba hakuna maisha yaliyopotea!!!!!Maggid una Busara sana Big Up
 
Maggid, nadhani ingekuwa vyema kama ungeclarify kosa la mbunge Msigwa ni nini haswa? Kupingana kimawazo sio kosa ni demokrasia. Pia nashindwa kuelewa kwa nini unamlaumu Msigwa wakati polisi ndio waliokuwa wakirusha mabomu? Je ni sahihi kwa polisi kutumia unnecessary force? Nadhani article yako hiko biase!
 
Sidhani kama ni sahihi kumnyooshea kidole Mh. Msigwa pekee yake kwani upo uongozi wa machinga na serikali ambao wangeweza kukaa na kuangalia namna nzur ya kulitatua tatizo na siyo kutoa kisingizio cha mch. msinwa pekee.
 
Post Kama hii ndo ilinifanya nijiunge JF, unatoa uchambuzi usio wa kishabiki, binafsi mi sio muumini wa violence, hivyo that's my last resort!
Hata hivyo kwa mtu anayetegemea nguvu ya umma huwa anaangalia umma unataka nini in exchange ya nguvu Zao inaweza kuwa hata wakitaka bangi wapewe ili nao watoe nguvu zao.
Nawasilisha!
 
Kwa kufuatilia suala la Wamachinga kufanya biashara eneo la barabarani pale Mashine tatu naamini kabisa, kuwa Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Msigwa angeweza kuepusha hali inayoendelea sasa kwa kuwasihi Wamachinga watii kwanza amri ya Manispaa, na yeye, kama Mbunge wao, kujiingiza kwenye mazungumzo ya dhati na wenzake kwenye Halamshauri ya Manispaa ya Iringa katika kutafuta ufumbuzi wa suala hili. Na hiyo ndio siasa. Siasa ina maana ya majidiliano endelevu badala ya kuhamasisha matumizi ya nguvu au vurugu pale milango ya majadiliano ingali wazi.

Mkuu kama mwandishi wa habari na pia mkazi wa Iringa unajua kuwa hili tatizo halikuanza leo... Je, unaweza kutupa hints kama Mchungaji Msigwa hajawahi au ni kwa kiasi gani amelishughulikia tatizo hili kwa mazungumzo kabla ya vurugu za leo?
 
Busara ulotumia kuandka n kubwa lakn sijaona point yyte ulozungumzia zaid ya kujisifia kua umetoka jogging na kutangaza blog yako hapo mwisho.umesahau kua NO CHANGES WITHOUT REVOLUTION
 
Heshima kwako Kiongozi!

Kwanza naamini tangu siku ile ulipoitwa kuhojiwa kuhusu suala la Ugaidi na Ludovick umesha kuwa muoga na serikali hii. Vile vile ninaona hoja zako katika mabandiko mbali mbali zimekuwa za ki- muegemeo kwenye serikali.

Kiongozi! Nina hofu huenda ndio zile mbio za kuminywa uhuru wa habari zimekutembelea kwa kunyooshewa kidole, au?!

Kiongozi!

Hivi kweli inaingia akilini kusema kwamba Mh. Mch Msigwa awashauri machinga kutii amri ya kuto kufanya shughuli zao huku akijikita kwenye mazungumzo ya namna ya kuondokana na ufanyaji shughuli zao kwenye eneo la Mashine Tatu? Unataka kuniambia kwamba suala hili ni la jana au leo asubuhi? Mbona lina muda mrefu na hakuna suluhu yoyote iliyo patikana kupitia serikali kama si Halmashauri ya Iringa?

Kipi kinge stahili kuanza kati ya kutafuta eneo jipya la kufanyia shughuli za wamachinga kabla au kuwaondoa kwanza? Na wakiondoka kwanza kabla ya kujua hatima yao, je, kipato chao cha kila siku walicho kuwa wanakitegemea watakipatia wapi. Je, tegemezi wao ikiwa ni pamija na watoto wanao hitaji kugharimiwa shuleni watakuwa kwenye hali gani?
Ukizingatia kwamba hata hiyo serikali inayo wafukuza hao wamachinga,tayari ilisha wasusa watoto wetu huko mashuleni kwa kuambulia viwango vya Division 0.

Kwa serikali hii ambayo wakubwa wakivunja sheria wanaongezewa kama sio kupandishwa vyeo, ifike mahali kila tunacho dai, tukidai kwa nguvu maana wanyonge wanaonekana kukosa haki, huku wakubwa wakivunja sheria na kutunukiwa nishani na kuzidi kusifiwa.

Ukweli ndio utarudisha heshima ya nchi hii ambayo tayari imesha potea kwenye macho ya dunia ya leo.

KIONGOZI!

TUFIKE MAHALI KWA UMOJA WETU TUKIRI KWAMBA SERIKALI YETU IMEFIKIA KIWANGO CHA KUTO KUWAJALI WANANCHI WAKE. VIONGOZI WENYE MAAMUZI KATIKA NCHI HII WANAJALI MASLAHI YAO TU!!!!!

Pole kama nimekukwaza Kiongozi!
 
Ngoja wenyewe waje wasiopenda kuambiwa ukweli na wasiopenda kuoneka wamekosea. Mnyanyii wakikutukana wewe kaa kimya.
 
Majjid,ubarikiwe,hakika chadema shetani anawatumia kuliangamiza taifa,wewe unayejiita mchungaji hebu Nijibu ni lini Huyu Yesu unedai kumtumikia alikua akihamasisha umma kupinga utawala na kuleta machafuko,wewe ni ajenti wa kuzimu,unatimiza unabii mkuu wa Mungu wa siku za mwisho,wewe ni mtumishi wa dunia hii sio wa ulimwengu ujao,acha kutumia jina la Yesu kwa tumbo lako,shetani amewakamata mmeamua kuliangamiza taifa letu,na sisi hatutawaacha ,the current state of our dear nation is fast filling up its cup of iniquity throug CHADEMA,violence and crime of political gain are filling our nation,and Satan is using Mchungaji msigwa to torn apart this innocent Nation.

The youth who walk the streets are surrounded with handbills and noice of crime and sin,their mind are educated to misbehave and crime,hatred and sin against the government,ole wenu chadema mnaodhani Mungu anazibariki kazi hizi za Ibilisi.

Mungu lete utulivu watu Wako tumalize kazi,Yesu urudi kulichukua kanisa lako,Amen
 
tataizo la wewe magidi ndio hili...uanaanza kumlaumu msigwa kwa lipi...sisi wamachinga tuna njaa ndio maana tuapiagania biashara zetu ambazo zina fanya watoto wetu waende chooni huo ni unafiki ndio maana hajapokea simu yako sababu unaonekana una majungu....wewe una mke wa kizungu ndio maana uanaona kama wamachinga wana fujo,tatizo ni munispaa wanalitumia vibaya jeshi la polisi..kulikua hakuna sababu ya kupiga mabomu leo.....acheni majungu tumia kalamu yako kuandika vitu ambavyo vinatugusa hata sisi watu wa kawaida,sio kujipendekeza kwa kina msambatavangu.......
 
Endesha mambo yako kisomi! Umepotoka sana kwa hili labda ukiri tu. Watu makini huwa hatukosei hivi! Msigwa kosa lake nini? Mchinga wafanye biashara porini,mbona nyie malimbukeni hv hasa mliopata kdogo.
 
Tatizo Msingwa anaiga tabia ya Lema, lakini inabidi ajue kuwa hulka ya mnyalukolo ni tofauti kabisa na hulka ya chalii.

Hizi zote ni harakati za Msigwa kujaribu kujisafisha jina lake baada ya kujidhalilisha kwa hotuba mbovu aliyotoa. Kama hotuba kashatoa, maji yameshamwagika, ajitahidi tu next time atoe hotuba yenye mashiko.

Maggid, poleni sana hapo. tafadhli jitahidi kumtafuta Msigwa muongee, afanye siasa za kujenga nchi. Naona katuma vijana wake waje kusema kashikwa na polisi kumbe yuko kwenye Harambee!!!
 
hakika chadema shetani anawatumia kuliangamiza taifa

hivi mpaka sasa hujui kuwa taifa hili limeshaangamia? Inaelekea hujui hata aliyeingamiza ni nani! Aliyeangamiza taifa hili ni serikali ya ccm ambayo imegubikwa na ufisadi kiasi cha kushindwa kuwapa ajira vijana wake. kuwepo kwa wamachinga wengi mitaani ni dalili mojawapo ya vijana kukosa ajira. Unatumia dini kubariki uovu. Hii ni dhambi kubwa sana. Yule anayesimamia uovu kwa kisingizio cha dini ni mfuasi wa shetani. Funguka roho yako na macho yako yatafunguka.
 
Back
Top Bottom