Kinachonishangaza..Jaji Warioba na Wenziye

1954tanu

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2013
Posts
1,038
Reaction score
487
Mwaka jana Tume ya Warioba ilitikisa sana nchi hii kuhusiana na kukusanya maoni ya wananchi na hatimaye kuja na Rasimu ya Katiba Mpya; wote tunaelewa kilichotokea rasimu ya Jaji Warioba ikatupiliwa mbali na CCM wakiongozwa na mwenyekiti wao. Utupiliaji mbali wa rasimu hiyo uliambatana na kashifa na kejeli kwa iliyokuwa tume ya Warioba.

Kwa uadilifu kabisa, wajumbe wa iliyokuwa tume ya katiba wakajikusanya kwa umoja wao chini ya Nyerere Foundation kutetea rasimu yao ya katiba wakisema yaliyokuwemo ndani ya rasimu hiyo ya katiba yalikuwa maoni ya watanzania. Jaji Warioba, H. Polepole, Butiku, Prof. Kabudi na wengineo walizunguka nchini wakieleza bayana kwamba serikali ya CCM imetupilia mbali maoni ya wananchi. Wananchi walitaka wawe na uwezo wa kuwawajibishia viongozi wao wa kisiasa, kupunguza madalaka ya ya rais, kutoruhusu viongozi kuwa na akaunti nje ya nchi, uadilifu na uwajibikaji.

Kinachonishangaza ni pale ninapoona watu wale wale waliozunguka kote nchini wakiendesha midahalo kuwaelimisha wananchi namna ambavyo serikali ya CCM ilivyodharau maoni ya wananchi. Wananchi wakafika mahala wakawaelewa waliokuwa wajumbe wa tume ya Jaji Warioba; lakini leo hii, wajumbe wale wale wanajitokeza hadharani na kusema hakuna waliobora miongoni mwa viongozi zaidi ya watu hao hao waliokataa katakata kuwajibishwa na wananchi; watu hao hao waliokataa kwa nguvu zao zote kuingiiza vipengele vya uadilifu na uwajibikaji katika katiba mpya.

Mwenzenu, hakika nawashangaa kina Jaji Warioba na wenziye.
 
Nyani walewale na msitu uleule
 
Unashangaa sio? Lakini ingekuwa vizuri ukaanza kushangaa Mbowe alivyochukua uamzi wa kumkumbatia Lowasa pamoja na mauchafu yooote waliokuwa wanatuaminisha Watanzania.
Ungeanza kumshangaa Mbowe kwa maamuzi yake ya kumkata Dr Slaa kwa sababu tu ya ubinafsi na tamaa ya fedha.
Ungeanza kuwashangaa viongozi wa ukawa, Lissu, Mnyika, Mdee, Lema, Wenje, pamoja na wengine pamoja na makelele yoooooooote waliokuwa wanatuaminisha Lowasa, Sumaye ni MAFISADI leo hii wameamua kujiunga nao kuendelea kufisadi nchi? !!!
Ungeanza kushangaa mbona hoja alizozizungumza Dr Slaa mbona hazijibiwi na watu wazielewe? ?
OGOPA MATAPELI
 
Swali lako zuri sana, mm nadhani ugomvi uliozuka ulikuwa wa uongozi wa chama na kundi lake SIO KAMWE chama chote, tukitambua kuwa jaji na hiyo foundation ni member wa chama husika, hivyo basi ni wazi jaji na wenzio walishinda hiyo vita,, kwa sasa swala ni lingine tofauti kabisa, kwa vita hii mpya wao wanaona HAKIKA huku kwa magufuli kuna nafuu kuliko japo sio SALAMA. wamekaa kimya.
 
Unashangaa sio? Lakini ingekuwa vizuri ukaanza kushangaa Mbowe alivyochukua uamzi wa kumkumbatia Lowasa pamoja na mauchafu yooote waliokuwa wanatuaminisha Watanzania.
Ungeanza kumshangaa Mbowe kwa maamuzi yake ya kumkata Dr Slaa kwa sababu tu ya ubinafsi na tamaa ya fedha.
Ungeanza kuwashangaa viongozi wa ukawa, Lissu, Mnyika, Mdee, Lema, Wenje, pamoja na wengine pamoja na makelele yoooooooote waliokuwa wanatuaminisha Lowasa, Sumaye ni MAFISADI leo hii wameamua kujiunga nao kuendelea kufisadi nchi? !!!
Ungeanza kushangaa mbona hoja alizozizungumza Dr Slaa mbona hazijibiwi na watu wazielewe? ?
OGOPA MATAPELI

Hoja hizo wameshazijibu wananchi kwa niaba yao. Mathalani, Dr. Slaa alifananisha kuja kwa EL Chadema na kitendo cha kupakua uchafu wa chooni na kuuleta sebuleni. Vijana wamejibu kwamba Watapiga deki ila chooni kutaendelea kuwa na uchafu ule ule. Upo hapo!
 
Kinachowasumbua wanasiasa wengi wa Tanzania ni njaa na unafiki!
 
Hoja hizo wameshazijibu wananchi kwa niaba yao. Mathalani, Dr. Slaa alifananisha kuja kwa EL Chadema na kitendo cha kupakua uchafu wa chooni na kuuleta sebuleni. Vijana wamejibu kwamba Watapiga deki ila chooni kutaendelea kuwa na uchafu ule ule. Upo hapo!

Ni vigumu mtu kukata tawi ulilokalia,wote wanajali maslahi yao zaidi kuliko wanachi.
 
Back
Top Bottom