Kinachomtesa ile siku ya mwisho hakulia, alicheka!

James Hadley Chase

JF-Expert Member
Mar 25, 2020
1,578
2,664
USIKU wa Manani, nipo macho. Nazungumza na Manani. Nawaombea pumziko jema waliotangulia. Namuombea afya mama yangu. Naukabidhi ukuaji wa mtoto wangu kwa Manani. Nawaombea heri ndugu zangu. Nalitakia salama taifa langu. Namsihi Muumba kuifanya dunia iwe tulivu.

Napanda kitandani. Mbilinge za mwanasheria Harry Spencer nilizozisoma siku hiyo kwenye kitabu “Judge Spencer Dissents” zimeniteka. Mwandishi Henry Denker ananifanya nitabasamu muda wote.

Nilipozima taa nikabaini simu yangu ilikuwa ikiita. Kioo kilitoa mwanga. Kutazama, rafiki yangu Modize ndiye alinipigia. Simu ilishakata. Nilipotazama vizuri zaidi, nikagundua alipiga mara nyingi. Missed calls 18, katika hizo, 12 ni za Modize.

Ana nini huyu mzee usiku wote huu? Nilijiuliza kisha nikampigia. Sikusikia ikiita, badala yake ilipokelewa. Modize amezoea kuniita “Swahiba”, basi huku akihema kwa nguvu, Modize alisema “Swahiba nateseka. Vendana ananitesa.” Nikashituka!

Vendana ni marehemu sasa. Ni mwaka tangu tulipomzika makaburi ya Chang'ombe, Temeke. Nikamuuliza Modize “Vendana anakutesaje?” Akanijibu: “Ananitokea ndotoni ananicheka. Anafurahia mateso yangu. Inaonekana yeye yupo nyuma ya hii mitihani ninayopitia.” Nilinyamaza nikitafakari. Nilimsikia Modize akilia upande wa pili.

Modize ana mengi kuhusu Vendana. Maisha yao ya ndoa yalitengeneza chemchemi iliyotiririsha machozi kila uchwao kwenye macho ya Vendana. Alilia asubuhi na hata mchana. Usiku kitandani alilia. Modize hakujali. Kinachomtesa Modize, ni ile siku ya mwisho, Vendana hakulia, alicheka.

Labda, kama si kile kicheko cha mwisho cha Vendana, leo Modize angekuwa hateseki. Labda Modize angemuona Vendana analia mwishoni, leo ingekuwa shwari. Alizoea kumuona akilia, lakini mwishoni alicheka. Na hakupata nafasi ya kumuona tena akilia. Kwa nini alicheka halafu akafa? Hicho ndicho kinamtesa Modize.

Modize akaniuliza: “Kwa nini Vendana hataki kunisamehe? Mbona nimeshamuomba sana msamaha? Au shida yake na mimi nife? Nitajiua afurahi, maana ndicho anataka.” Sikuwa na jibu la kumpa Modize. Ningemjibu nini?

Modize alipoona sijibu, akasema: “Vendana anayenitokea ni katili na mkorofi. Nilimzoea Vendana mpole. Alinipigia magoti kuniomba msamaha japo mkosefu nilikuwa mimi. Alinipa pole kwa kazi hata niliporejea nyumbani asubuhi nimelewa, nikiwa nimetoka kustarehe na wanawake wengine.” Nilimsikia tena Modize analia!

Kuna watu wakilia ni busara kuwaacha walie, kuliko kuwabembeleza, wanaweza kudhani unawasanifu. Ni kama Modize, ukijifanya bingwa wa kubembeleza, yanaweza kukutokea mazito. Hasira za Vendana zitahamia kwako.

Ni kama namuona Vendana. Mwanamke mzuri, mrembo sana. Naogopa kukutajia sifa zake nisije kukuchumisha dhambi. Unaweza kumtamani marehemu. Au ukamchukia Modize kumnyanyasa mwanamke mzuri kama Vendana. Na chuki ni dhambi. Hushindwi kulaumu kwa nini Vendana alikufa mapema. Je, unampangia Mungu?

Nakumbuka siku Modize na Vendana wanafunga ndoa, furaha na bashasha viliteka nyuso zao. Nayakumbuka mapenzi yao, usingedhani yangebadilika. Mwaka mmoja na miezi mitatu ya ndoa iliondoka na furaha pamoja na upendo wote. Ndipo Vendana aligeuka mtu wa vilio. Kinachomtesa Modize ni kuwa siku ya mwisho Vendana hakulia, alicheka.

Walianza kama marafiki, uchumba ukafuata. Kisha Modize alijisalimisha kwa wazazi wa Vendana, ndoa ikachukua nafasi. Ingekuwa Modize alilazimishwa ndoa, angalau tungemtetea. Alimpenda mwenyewe na alimlia yamini.

Ndoa ilianza kwa furaha, upendo na amani. Modize alirudi nyumbani mapema na Vendana alimpokea kwa bashasha. Kama tungekaa viwanja na Modize, isingechukua muda Vendana angetokea. Walipeana ratiba zote, hawakunyimana location. Walikuwa wanandoa marafiki wapenzi.

Ungewakuta wakiongea na kucheka, ungesema duniani hakuna ndoa bora kama ya Vendana na Modize. Walitaniana na kucheka. Walipeana stori na michapo. Halafu walipanga pamoja maendeleo yao na kujiwekea malengo. Waliishi kama timu moja ya ushindi. Bonge la timu!

Kama si yule mwanamke mwenye makalio kama kichuguu chenye nyoka, wala yaliyotokea yasingetokea. Sijui yule mwanamke alimpa nini Modize na makalio yake?

Ghafla Vendana akawa hana chake. Ratiba za Modize hazikumhusu. Raha za Modize hazikuhusiana na Vendana. Ile ndoa bora, ikageuka jinamizi linalonyonya damu. Vendana akakonda na kupukutika. Faraja yake ikawa kilio. Modize hakufanya chochote kumwepusha Vendana na vilio.

Kuna wakati Vendana alimuuliza Modize akilia: “Hivi hao wanawake zako huko nje wanakupa nini na mimi nikupe ili utulie?” Modize badala ya kujibu, alimtazama Vendana kwa dharau, kisha akaondoka zake.

Modize hakuishiwa maneno makali, alimwita Vendana mshamba. Alimsema hajui mapenzi. Akamtamkia kuwa alijuta kumuoa. Akamsimanga kuwa amezeeka. Modize aliacha neno lipi baya? Vendana aliyapokea yote. Alimlilia Mungu Modize abadilike. Awe mwanaume mzuri tena.

Modize alimtesa Vendana kila eneo. Hata unyumba! Jamani! Vendana angemlilia Modize ampe haki yake ya ndoa. Modize angekuwa mkali. Vendana angebembeleleza, kipigo kingefuata. Ndio, Modize alimpiga Vendana mara nyingi. Vendana alilia na kumshukuru Mungu. Inaonekana Modize alipenda kumwona Vendana analia, maana kinachomtesa Modize leo ni kwamba ile siku ya mwisho, Vendana hakulia, alicheka.

Ipo siku Modize alirudi nyumbani mpole. Vendana alimhurumia, akamuuliza “cha mno” nini? Modize hakuwa na jibu. Modize alitoka kumfumania mwanamke wake wa nje. Yule mwenye makalio kama kichuguu chenye nyoka.

Siku hiyo, hata unyumba Vendana alipata. Japo hayakuwa mapenzi yenye mashamshamu kwa sababu fikra za Modize zilikuwa mbali. Walikuwa wawili chumbani kitandani, lakini kiakili Modize alikuwa maili nyingi akimuwaza mwanamke wake aliyemfumania. Pamoja na hivyo, Vendana alifurahi, kwani ilipita miezi mingi bila kuguswa na mumewe.

Siku mbili baadaye Modize akapata suluhu na mwanamke wake wa nje aliyemfumania. Akapotea wiki nzima bila kurudi nyumbani. Simu haikupokelewa na wakati mwingine ilikatwa. Kisha ilipokelewa na mwanamke aliyemwambia: “Wewe mbona king'ang'anizi? Mwanaume hakutaki, si utafute mwingine?” Vendana alilia.

Wiki moja ilipovuka, Vendana alihisi mabadiliko ya kimwili. Aliwashwa sehemu za siri, koo ikawa kavu na alipokwenda haja ndogo alihisi maumivu. Alipokwenda hospitali, alikutwa na kaswende. Maskini, miezi na miezi kavumilia, eti mara moja kukutana na mumewe ndio apate kaswende! Ilimuuma sana. Angefanya nini?

Vendana akiendelea na matibabu, kwa sindano na vidonge, Modize alimrudia na hasira. Modize alimpiga Vendana na kumtuhumu kumwambukiza kaswende. Hivi kweli Vendana wa kujikalia ndani angeitoa wapi hiyo kaswende? Alishindwa kulituhumu li mwanamke lake lenye makalio kama kichuguu chenye nyoka alilolifumania? Vendana alilia sana. Kwa maumivu ya kipigo na kusingiziwa.

Ni baada ya siku hiyo Vendana hakulia tena. Modize asingerudi nyumbani mwezi na Vendana asingemtafuta. Modize aliporudi nyumbani, Vendana hakuwa na habari naye. Mabadiliko hayo yalianza kumshughulisha Modize. Nini kimembadilisha?

Mawazo ya Modize yaliongezeka na kuongezeka. Alihisi Vendana kapata mwanaume mwingine. Akawa anamuwinda. Angerudi nyumbani ghafla na kukagua kila sehemu bila kukuta chochote chenye dalili ya mwanaume. Alichukua simu ya Vendana na kupekua. Alikuta bilabila!

Modize alipomtaka Vendana kimwili aligonga ukuta. Vendana alimwambia “labda mpaka tukishapima”. Modize alipotaka kutumia nguvu ikawa patashika. Vendana alishabadilika. Hakuwa tena mnyonge.

Modize alipomwambia “wewe una mwanaume ipo siku nitakukamata naye”, Vendana badala ya kukanusha, alicheka. Ni kicheko hicho kinamtesa Modize kipindi hiki Vendana yupo kaburini. Alizoea kumuona akilia, sasa kwa nini mwishoni acheke?

Usiku wao mwisho ulikuwa hivi; Modize alirudi nyumbani usiku unaopakana na alfajiri. Alikuwa amelewa. Vendana alimgundua alitoka kwa mwanamke. Kitandani, Vendana akajidai anamtaka kimapenzi mumewe. Modize akajibu “sijisikii” kisha aligeuka na kumpa mgongo. Kwa tendo hilo, Vendana alicheeeka! Kicheko cha Vendana kilimkera Modize.

Akafoka “nitakupiga wewe mwanamke, unanicheka mimi?” Vendana akamjibu: “Nisamehe mume wangu, Shetani wa kitandani ni mbaya sana, tumshinde.” Wakalala.

Asubuhi wakati kila mmoja akishika njia yake ya kwenda kibaruani kwake, Vendana alimuuliza Modize: “Utarudi mapema leo au ndio kama kawaida, kuondoka leo kurudi kesho?” Modize akajibu: “Ratiba zangu hazikuhusu.” Vendana alicheka. Alicheka sana. Hicho kikawa kicheko cha mwisho.

Modize alitaka kujua siri ya vicheko vya Vendana. Mapema alimtumia ujumbe kuwa angechelewa kurudi nyumbani. Vendana alijibu neno moja “sawa”. Kigiza cha Magharibi, ilikuwa inaelekea saa 1. Modize alifika nyumbani na kukuta giza.

Modize akajinong'oneza: “Nilijua, huyu mwanamke kuna mwanaume anamzuzua. Nimemdanganya nachelewa kurudi, muda huu hayupo nyumbani?” Akampigia simu, haikupokelewa. Akasema tena: “Naona ndio shughuli imekolea, simu zangu hazioni. Leo akirudi namtimua.” Akagundua geti liliegeshwa tu, mlango pia ulikuwa wazi.

Modize akasema: “Nilioa mwanamke taahira kweli, anajiondokea tu kwa wanaume zake bila kufunga milango.” Akawasha taa za nje, verandani, koridoni, akaingia chumbani. Alipowasha taa, Modize alimshuhudia Vendana amelala akiwa mtupu, bila nguo yoyote, Modize aliita. Angewezaje kuitika? Vendana alilala usingizi wa mauti.

Modize akaita polisi, mwili wa Vendana ulipofanyiwa uchunguzi, ripoti ya daktari ilisema kifo cha marehemu kilisababishwa na hali ya ukosefu wa oksijeni kwenye ubongo (asphyxia).

Nini sababu ya oksijeni kushindwa kufika kwenye ubongo? Daktari aliunganisha picha za tukio, namna mwili wa Vendana ulivyokutwa, mtupu bila nguo, mkono wa kulia ukiwa sehemu za siri.

Akasema: “Marehemu alikuwa anajichua kujiridhisha kimwili. Hali ya kulazimisha hisia kujifikisha kileleni, ilisababisha mishipa ivimbe na kuzuia oksijeni kufika kwenye ubongo. Kitaalamu tunaita autoerotic asphyxiation.” Modize akashituka!

Huo ndio ukweli, Vendana tangu alipopona kaswende aliyoambukizwa na Modize, alichagua kujipa raha mwenyewe. Hakujua kuwa kujichua kungesababisha kifo chake. Aliuzoea mchezo, akalemaa.

Modize akawaza: “Nilidhani ana wanaume kumbe alijichua!” Alijilaumu kidogo kuwa pengine angekuwa jirani na mkewe, yaliyotokea yasingetokea. Baada ya muda, safari na muziki. Akalichukua lile li mwanamke lake lenye makalio kama kichuguu cha nyoka. Akaliweka ndani. Eti wakawa mke na mume!

Unafanya mchezo? Lile li mwanamke likamperemba, likauza nyumba. Matumizi makubwa ya kulihudumia, yalisababisha mtaji wa biashara nao upepesuke. Na zama hizi za vyuma kukaza, Modize akajikuta yupo hoi kiuchumi, kimapenzi na kifamilia.

Anamkumbuka sana Vendana. Anajilaumu kwa kila alichomfanyia. Ule uzuri wa Vendana, ile sauti yake tamu masikioni, lile tabasamu na utiifu wake, vyote vinamjia kichwani Modize na kujikuta muda wote anamuwaza Vendana.

Zile huruma za Vendana, vile alivyomfariji nyakati ngumu. Ule urafiki wao na yale mapenzi yao, vyote vinamrudia Modize na kumtesa sana. Jinsi alivyombadilikia, namna alivyomtesa na kumfanya Vendana alie kila siku, ni taswira iliyotuama kwenye fikra za Modize.

Modize anajihukumu, anashindwa kujisamehe. Hakika, binadamu aliyekufa hutesa kuliko aliye hai. Hasa marehemu akiwa na kinyongo.

Ni kwa sababu Modize anajihukumu kwa matendo aliyomfanyia Vendana ndio maana akilala humuona anamcheka. Akiwaza, Vendana humtokea akimcheka. Na kubwa zaidi ni ile siku ya mwisho, Vendana hakulia, alicheka.

Namsaiadiaje Modize? Halali wala hapati utulivu. Akilala anaweweseka, akikaa peke yake haishiwi mishituko. Natamani nimwambie Modize kuwa Vendana hamtesi, alishapumzika zake, kinachomtesa yeye ni ile taswi ya siku ya mwisho, Vendana hakulia, alicheka.

Ndimi Luqman MALOTO
 
J

Jifunze kufupisha habari bro.
 
Back
Top Bottom