Ndio wengi.!
Mzee ameongea kishujaa sana, kaanza kwanza na kusema yale bwana yule anayotaka kuyasikia, ndani yake akachomekea suala muhim sana ambalo bwana yule akabaki ameduwaa hajui afanye nini mwishowe akazuga kwa kucheka.
.....View attachment 1002589
Hii ilikuwa uganda enzi za Idd Amini , naye aliitisha kikao cha majadiliano na watu wa dini , kwahiyo haya mambo hayajawahi kuleta nafuu popote pale .
We bwege nimekuelewa mpaka nimekuelewa tena.Hahahaha kuna mtu anataka "kutembelea Nyota" ya viongozi wa dini! Maana siku hizi kila shughuli yupo nao kama vile Gwajima, Kakobe, mara wapo Maaskofu etc
Anajua viongozi wa dini wakiwa upande wake , wakimzungumzia kwa uzuri basi na kondoo wao watakuwa sympathetic naye!
Kule kwa ndugu zetu Waislamu yeye ameridhika kujumuika na Sheikh Alhadi, lakini kwa Jinsi yule dada wa Marekani alivyokwishatoa tuhuma kali kwa huyo Sheikh keshachafuka sana, hakuna Muislamu anayemchukulia serious!!
Ngoja nimshauri njia nzuri ya kuleta umoja na mshikamano wa Kitaifa!
1. Mzee angalia TEUZI zako zimeegemea upande mmoja zaidi, watu wanalisema hili mtaani
2. Heshimu katiba ya nchi, hakuna haja ya kuminya haki ambayo makundi mengine yamepewa na katiba, haikufanyi kuonekana strong kwa kujaribu kuimply kwamba uko sahihi kuliko katiba
3. Kazi zako zilenge kupanua uhuru wa watu zaidi kuliko kuuminya. Hii miswada ya vyama vya siasa ambayo inakwenda kuminya vyama na kuvifanya viwe vyama visivyong'ata hailisaidii Taifa. Nyerere alidhani mwaka 1965 kuwa vyama vingi vinamchelewesha kuleta maendeleo lakini Nyerere huyohuyo miaka 25 baadae akagundua kuwa alifanya mistake kubwa, please usichukue njia hiyo ya kale kwa sababu kwanza Kizazi kijacho kitaifuta hiyo sheria unayotaka kuifunga, lakini utakuwa umeshawachelewesha kwenye kujenga Taifa lililokomaa kidemokrasia
4. Mzee, Mshikamano bila uchumi ni sawa na kiwiliwili bila mikono na miguu, hapawezi kuwepo na mshikamano wakati vyuma vimekaza, bila uchumi ndoa zitakufa, watu watashikana uchawi, vibaka wataongezeka, misongo ya mawazo itaongezeka na hatimaye kuzaa chuki baina ya wenye nacho na wasionacho, Mshikamano hautakuwepo!. Badili sera zako za uchumi sasa ili kustimulate biashara, Ikibidi kupunguza kodi punguza, nimeona leo kwenye taarifa ya habari kuwa uchumi wa china umeshuka na njia moja wanayoifanya sasa ni kupunguza kodi na kuinject mabilioni ya dola kwenye miradi inayogusa wananchi moja kwa moja ili kupunguza makali!. Ongea vizuri na wafanyabiashara wakubwa nchini, wafanyie wepesi kwenye mambo yao usiwakwaze, Matajiri ni mawakala wa Mungu kwenye kusambaza Rizki kwa waja wake duniani!, Wana upako wa hela hao, ukiwajaribu kuwashusha utashuka mwenyewe!, Ukijaribu kuwakwaza utajikwaza Mwenyewe, maana maandiko yanasema yule aliyepewa na Mungu hakuna mwanadamu anayeweza kumnyang'anya labda Mungu mwenyewe awe ameamua hivyo!!.
5. Mzee inabidi sasa uanze kuwa Stateman, Unahitajika sasa Kupandisha "Game" yako iwe international zaidi. Uwanja wa hapa nyumbani muachie Kassimu, sina shaka naye, ni kiungo mchezeshaji mzuri sana, nazikubali kazi zake. Sasa inabidi uende Ulaya uongee na akina Angela Merkel, akina Theresa May, Nenda Canada, Nenda hata hapo Australia kaongee na Investors waje, Shuka hata South hapo bondeni uangalie nini wataalamu wa madini hapo wanaweza kushare nasi katika hii sekta
6. Mzee, Maendeleo ya vitu bila Uhuru ni kazi bure!. Leo hii tunamkumbuka Nyerere siyo kwa sababu alijenga reli ya Tazara, na bomba la TAZAMA au Viwanda kedekede tunamkumbuka zaidi kwa sababu alitupa Uhuru kutoka kwa mkoloni!. Na wewe unayonafasi ya kutupa Uhuru mpana zaidi, hizi sheria za Habari na Takwimu hazitusaidii katika azma ya kuwa na watu wenye FIKRA HURU, Zinaweza kukusaidia kisiasa katika mwaka wako mmoja uliobaki au ukibahatika Sita iliyobaki lakini zina athari isiyomithilika kwa Usitawi wa Taifa. Zitakwenda kujenga Taifa la Watu Vipofu, Wasiohoji, Wenye kuamini Propaganda za Serikali inayotawala, Kiufupi zinakwenda kujenga Taifa la watu walio usingizini!. Je ungependa miaka 30 ijayo kuwa na TAIFA la watu bongolala?. Angalia miaka 50 ijayo mzee, usiangalie uchaguzi ujao
7. Mzee Korosho, Korosho, Korosho Mzee, Kangomba na Mkulima wa Korosho ni sawasawa na chungu na Kata, Mkulima anayetafuta hela ili amcheze mwanae Ngoma, Kangomba ndiye Mkombozi wake!. Huwezi kudhani Kangomba anamdhulumu mkulima, wakati Mahitaji ya Mkulima yanatimizwa na Kangomba!. Nyinyi watu wa Mjini mnadhani mahitaji yenu ya mjini ndo yaleyale ya mkulima!. Ni sawasawa na Mzungu atoke huko Ulaya akute mwalimu wa Msingi analipwa dola 300 ( shilingi laki sita) halafu aanze kudai eti Mwajiri anamdhulumu mwalimu!. WE NEED TO KNOW basic economics pribciples za NEEDS za watu na WANTS za watu!
LISSU kamalizwa na Stephen, asubiri kufa tuMzee anahangaika kumaliza kiki ya Lissu!
naunga mkono kupigwa marufuku biashara zote za bahati nasibu, betting na kamari.
Na ile gaming board ifutiliwe mbali kabisa.
Ushoga ndio kabisa Mungu atuepushie mbali usitokee kabisa
......Tunakonkludi kwamba viongozi wengi waliofika hapo ni wachumia tumbo hawajazitaja shida halisi za watanzania ,wakati kila Siku wako nao makanisani na misikitini.
Nasema zilizokuja ni Takataka! Potelea mbali. Hakuna kiongozi wa dini, ni takataka tu!Ni Kongamano la Kidini au ni la Kongoamano la Kujipendekeza, Kusifu na Kulia Njaa?
Tatizo mifumo yetu ya utawala haitaki watu waerevu ndyo maana wakina bashite wanatamba na matamko ya hovyoHuyo Mchungaji kijana mchumi anaitwa KIMARO amemwaga fact sana sana, HIVI WACHUMI MNASHINDWA KUWAZA KAMA ANAVYOWAZA HUYO MCHUNGAJI, AU MUENDE MKASWALI KANISANI KWAKE MUOMBE KIPINDI MAALUMU CHA UCHUMI.
HUYU MCHUNGAJI ANAONYESHA MADHARA KABISA YA WASOMI WETU KUKOSA EXPOSURE MAANA ANAJUA VITU VINGI AMBAVYO WATU KAMA WANGEKUWA WANAVIJUA NA KUVIAPPLY TUNGEKUWA MBALI SANA..