Kinachojiri Bungeni Dodoma kipindi cha maswali na majibu leo tar 27/ 04/2016

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,253
SwaBunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kikao cha 6, mkutano wa 3

Kipindi cha maswali na majibu

Swali: Ni kwa namna gani serikali inatumia utafiti kubaini changamoto zilizoainishwa?

Majibu:
Taarifa na tafiti zinatumika katika nyanja zifuatazo;
1.Programu ya kukuza ujuzi kwa vijana.
2.Mfuko wa kujiajiri kwa vijana.
3.Baraza la uwekezaji kwa vijana.

Swali: Je, Serikali kupitia REA ina mikakati gani ya kupeleka umeme kwenye jimbo la Bukene?

Majibu: Mkandarasi kutoka China ameshinda tenda; ametakiwa kuharakisha ukamilishaji wa mradi. Mradi umekamilika kwa asilimia 82.
Kazi ya ufungaji umeme na transfoma bado inaendelea kwa baadhi ya vijiji.

Swali: Ni lini Serikali itafuta tangazo namba 28 linalotaka wananchi wanaokaa karibu na hifadhi kuondoka?

Majibu: Serikali inafanya kila jitihada kutatua mgogoro huo. Inapitia upya mipaka iliyoweka. Pia Inahakikiki fidia kwa wananchi.
Aidha Eneo la hilo linalindwa kisheria, na badiliko lolote linatakiwa kufuata sheria
Zoezi hilo litakamilika kwa kipindi cha mwezi mmoja.

Swali: Ni lini Serikali itakamilisha barabara inayounganisha vijiji vya Wilaya ya Rorya?

Majibu: Serikali imeshaanza kuijenga kwa awamu 2010/2011. Mpaka sasa ujenzi unaendelea na itaendelea kadri ya upatikanaji wa fedha.
Wataalamu wa sekta ya ujenzi wanaangalia uwezekano kuijumuisha barabara hiyo, kipaumbele kwa bajeti ya mwaka 2016/2017 ni kukamilisha miradi ya muda mrefu ili kuondokana na gharama za wakandarasi.

Swali: Je, ni lini Serikali itajenga kwa kiwango cha lami barabara ya Ifakara ili kurahisisha usafirishaji wa mazao?

Majibu: Serikali imeanza upembuzi wa kujenga kwa kiwango cha lami kilomita 24, utakamilika june 2016. Na sehemu nyingine inayobaki itajengwa na manispaa.
Ahadi zote zilizowekwa na serikali 2015/2020 zitakamilishwa.

Swali: Je serikali ina kauli gani kwa shamba namba 112 lilipo Nduruma ambalo?
Majibu: Hekari 80 zimerudishwa kwa wananchi na zimekabidhiwa kwa halmashauri.
Wizara bado inashughulikia migogoro yote ya ardhi nchini.

Swali: Ni lini kituo cha polisi kata ya Loya kitafunguliwa?

Majibu: Kituo hakijamilika sehemu ya silaha na choo. Pindi vikikamilika kituo kitafunguliwa.
Serikali inajipanga kununua magari mengi ya polisi kuhakikisha vituo vinapata magari.

Swali: Je, Tume ya Haki za Binadamu imefanikiwa vipi toka 2010 hadi 2016?

Majibu: Malalamiko yaliyoripotiwa ni 13,709 kati ya hayo, 6169 yalishulikiwa.

Kuhusu uchaguzi Zanzibar na mshekhe kulawitiwa,
Malalamiko hayajaripotiwa na kama kuna wenye ushahidi wa kulawitiwa mashekhe wapeleke kwenye tume ili yashughulikiwe.

Swali: Serikali ina mpango gani ya kufanyia marekebisho sheria ya ndoa na kuunda sheria ya mirathi?
Majibu: Serikali inapanga kufanya marekebisho sheria ya ndoa na ipo kwenye mchakato wa kuunda sheria ya mirathi.
 
Leo ni Bajeti ya Ofisi ya Rais TAMISEMI na Utawala Bora
 
MASH.jpg
 
Back
Top Bottom