Kinachofuata ni Mbowe kupewa mwaliko wa kwenda Magogoni ili picha zake na Bwana mkubwa zitumike katika kufanikisha damage control

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,014
144,372
Leo hii baada ya habari ya Msigwa kulipiwa na Magu kutoka,watu watakuwa wameshangaa ila mimi binafsi sijashangaa kwani nilijua kitafanyika kitu kama hiki na hakika kimetimia ndani ya masaa 24.

Wakati ACT-Wazalendo wakichangia shilingi milioni mbili,sitashangaa chama cha kijani nacho kikachangia ili kujisafisha na aibu hii ya kisiasa

Lengo kubwa la mada hii si kuongelea haya yanayoendelea,bali ni kuwatahadharisha CHADEMA hasa mwenyekiti Mbowe kuwa kitachofuata ni yeye kualikwa Magogoni kwa mazungumzono na Bwana yule alafu baadae watoke mbele ya waandishi wapige picha kuonyesha kuwa siasa si uadui na kwamba Bwana yule hana chuki na upinzani(usanii mtupu).

Hivyo,namtahadharisha Mbowe ikiwezekana mwaliko huo{kama utatolewa) aupotezee kabisa kwani utakuwa ni wa kujaribu kurekebisha makosa ya wao kuwekwa ndani na ukweli mwingine ni kuwa watachokubaliana kitakuwa ni geresha tu hivyo ni bora asijisumbue kukutana na Bwana yule.

Tambueni huyu Bwana amepania kuwashughulikia kadri awezavyo hivyo kuweni makini
 
Hahaha Kamwe akipewa mwaliko awezi kataa maana ni juzi tuu walikuwa wana lilia mualiko wa Ikulu ni vigumu kukataa...hahahaha hata ungekuwa wewe
 
Yule bwana nafasi ya kiki bado anayo atangaze msamaha au hata zuga ya kuwalipia waliobaki ili watoke hii itafunika ile aibu ya msigwa
 
We jamaa kuna wakati huwa unaona mbali ila tatizo lako unamtetea Mbowe ambae alishafel kuiongoza chadema

Sent using Jamii Forums mobile app

Bora Mbowe.... Wewe hicho chama na harakati zake ukipewa utakikabidhi kwa bashite au pole pole within 24 hours...!!
Bila kupepesa macho ama kuumauma maneno, Watanzania wengi wamejitambua kisiasa kupitia harakati za upinzani chini ya huyo huyo Mbowe...!!
Ameshapoteza na anaendelea kujitoa muhanga ili wewe na wengineo mjitambue...!!
You need him more than you can imagine!!
 
chadema_in_blood_B9Uq1Y-H-HM.jpeg
 
sure.
Mbowe aweke masharti yafuatayo kabla ya kukutana na JPM:

1. aafiki uundwaji wa tume huru (NEC)
2. aondoe zuio la mikutano na maandamano ya kisiasa
3. atoe guarantee ya usalama wa Tundu Lissu atakaporejea nchini

in my opinion...JPM akikubali kutekeleza masharti hayo 3, basi Mbowe aende ikulu na ku hug naye kabisa!
 
Wanakumbuka shuka asubuhi kuanzia kwa polepole jana unaona ni jinsi gani serikari na CCM inavyotumia nguvu kujisafisha wao hawana influence na maamuzi ya mahakama.

Isingekuwa CDM kujianzishia harambee yao; wangetumia propaganda gani kujisafisha.

Kama kuna vitu raisi na yeye anaona sio sahihi anatakiwa avipige stop kabla avijachafua nchi.
 
sure.
Mbowe aweke masharti yafuatayo kabla ya kukutana na JPM:

1. aafiki uundwaji wa tume huru (NEC)
2. aondoe zuio la mikutano na maandamano ya kisiasa
3. atoe guarantee ya usalama wa Tundu Lissu atakaporejea nchini

in my opinion...JPM akikubali kutekeleza masharti hayo 3, basi Mbowe aende ikulu na ku hug naye kabisa!
Na mapokezi ya Tundu Lissu yawe huru na ya amani
 
Bora Mbowe.... Wewe hicho chama na harakati zake ukipewa utakikabidhi kwa bashite au pole pole within 24 hours...!!
Bila kupepesa macho ama kuumauma maneno, Watanzania wengi wamejitambua kisiasa kupitia harakati za upinzani chini ya huyo huyo Mbowe...!!
Ameshapoteza na anaendelea kujitoa muhanga ili wewe na wengineo mjitambue...!!
You need him more than you can imagine!!
Ningeweza kukupa like Mia moja ningekupa mkuu. Waliotaka kuwa wenyeviti Kuna aliyebaki chadema? Wote wameshajipendekeza. Ni kama wafanyakazi wanaojipendekeza wanavyopendwa na wenye misimamo wanavyochukiwa. Chadema Kuna watu kadhaa huwezi kuwatingisha akiwemo Mbowe mwenyewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbowe hawezi kuingia kwenye huo mtego wa kijinga. He is a smart opposition leader ever happened in the East and Central African Region. Hajawahi kuongozwa na njaa bali akili iliyotukuka.
 
sure.
Mbowe aweke masharti yafuatayo kabla ya kukutana na JPM:

1. aafiki uundwaji wa tume huru (NEC)
2. aondoe zuio la mikutano na maandamano ya kisiasa
3. atoe guarantee ya usalama wa Tundu Lissu atakaporejea nchini

in my opinion...JPM akikubali kutekeleza masharti hayo 3, basi Mbowe aende ikulu na ku hug naye kabisa!

That is monkey business...
Huwezi kukutana nao kujadiliana chochote kikatekelezeka!!
Washapigwa upofu ili changes zitokee!!
Bado raia tu kutambua nguvu ya wingi wao!!
 
Back
Top Bottom