Kinachoendelea Msumbiji ni matokeo ya zuio la Uraia Pacha

MkamaP

JF-Expert Member
Jan 27, 2007
8,143
3,222
Kinachoendelea msumbiji ni matokeo hasi kwa nchi ya Tanzania kuzuia wananchi wake kupata uraia wanakoishi ili wapate ku safeguard haki zao za msingi.

Choice has consequenses, ni chaguo tuliamua kufuata la kuwarithisha ndugu zetu wanaokosa fursa sawia ndani hapa nchini na kuamua kupanua zaidi uwanja wa kujitafutia riziki zao za kila siku. Lakini, ni jambo mhimu zaidi kuelewa ya kwamba unapotafuta riziki zako yakupasa kuzilinda kisheria, na kinyume chake ni kuwa, ukiamua kuziachia riziki zako kuwa vulnerable kwa kila mmoja basi umasikini kwako hauwezi kukoma.

Watanzania wanaolilia uraia pacha, si kweli kwamba wanaukana utanzania ama si kweli kwamba hawana uzalendo, bali wanataka kulinda mali zao kisheria, wanataka kuondokana na vulnerbility hizi kama zinazotokea Msumbiji.

Mie nafikiri ni unafiki wa kuwabeza wamsumbiji kuwatimua Watanzania kwa kigezo tu eti tuliwasaidia miaka ile. Sasa kama wewe ndugu yako uliyenaye mpaka leo anayesaidia watanzania wezake mpaka leo unamwekea pingamizi la ku safeguard malighafi ya Tanzania, unapata wapi moyo mweupe pee wa kuwasemea wa msumbiji mahitaji yao?

Hatutakiwi kuchukulia mambo for granted eti ni serikali rafiki ama tuliwasadia, badala yake tunatakiwa ku secure and safeguard watu na mambo yetu. Sasa hao wamerudishwa tuje tupigane nao vikumbo mtaani kutafuta ajira. Na wenda huko walikokuwa waliajiri watu wengineTanzania, na pia wengine walisaidia ndugu tegemezi. Kinyume chake sasa, wamekuwa tegemezi wao wenyewe,eti kwa kwasababu tu tulishindwa kuwalinda harafu leo tunajidai kutoa matamko kuhusu msumbiji.

Na huu unaweza kuwa mwanzo tu, wengine watatolewa huko USA, europe na kwingine ili waje tubanane humu bongo, maana Tanzania ni kisiwa ni nchi pekee inayokana malighafi watu wake.

Kuna nchi moja ya Kusadikika ktk kitabu cha kusadikika, ilikuwa masikini sana na ikaamua kutuma wajumbe nchi zingine kujifunza huko wanafanya je mambo yao kunyooka? wajumbe walivyorudi pamoja na kupata misukosuko toka kwa mfalme, bado walielezea wanachofanya nchi zingine, na baadae mfalme alipokubali ule ushauri basi Kusadikika iliendelea sana.

Tofauti na Tanzania na kusadikika, ni kuwa Tanzania inawatuma wajumbe harafu haitaki kabisa warudi eti siyo wazalendo. Kwa kukata story short, ni kwamba mtu huwezi endelea kwa kutumia mawazo na mbinu zilezile zilizowahi kushindwa.
 
Kwanini isiwe uhuru wa kutumia pass zetu kama wakazi wa SADC? Ulaya wanaitumia hiyo kwa wanachama wa jumuiya Yao. Kingine umaskini na njaa unatusumbua sana
 
sina hakika kama SADC tunaruhusiwa kufanya kazi nchi zingine bila kuwa na working permit. Na kingine ndugu yangu, watanzania hawako SADC tu wapo ulaya na Amerika na Asia.

Inatakiwa tulinde masilahi yao kwa kufanya hivyo unalinda masilahi ya nchi. Na kufanya hivyo unaanza kwa kitu kilicho ndani ya uwezo wako bila ku negotiate terms na mtu yeyote. Swala la uraia pacha ni swala la ambalo liko ndani ya uwezo wa Tanzania bila ku negotiate terms na nchi yoyote.
 
Kinachoendelea msumbiji ni matokeo hasi kwa nchi ya Tanzania kuzuia wananchi wake kupata uraia wanakoishi ili wapateku safeguard haki zao za msingi.

Choice has consequenses, ni chaguo tuliamua kufuatwa la kuwarithisha ndugu zetu wanaokosa fursa sawia ndani hapa nchini na kuamua kupanua zaidi uwanja wa kujitafutia riziki zao za kila siku. Lakini, ni jambo mhimu zaidi kuelewa ya kwamba unapotafuta riziki zako yakupasa kuzilinda kisheria, na kinyume chake ni kuwa, ukiamua kuziachia riziki zako kuwa vulnerable kwa kila mmoja basi umasikini kwako hauwezi kukoma.

Watanzania wanaolilia uraia pacha, si kweli kwamba wanaukana utanzania ama si kweli kwamba hawana uzalendo, bali wanataka kulinda mali zao kisheria, wanataka kuondokana na vulnerbility hizi kama zinazotokea Msumbiji.

Mie nafikiri ni unafiki wa kuwabeza wamsumbiji kuwatimua Watanzania kwa kigezo tu eti tuliwasaidia miaka ile. Sasa kama wewe ndugu yako uliyenaye mpaka leo anayesaidia watanzania wezake mpaka leo unamwekea pingamizi la ku safeguard malighafi ya Tanzania, unapata wapi moyo mweupe pee wa kuwasemea wa msumbiji mahitaji yao?

Hatutakiwi kuchukulia mambo for granted eti ni serikali rafiki ama tuliwasadia, badala yake tunatakiwa ku secure and safeguard watu na mambo yetu. Sasa hao wamerudishwa tuje tupigane nao vikumbo mtaani kutafuta ajira. Na wenda huko walikokuwa waliajiri watu wengineTanzania, na pia wengine walisaidia ndugu tegemezi. Kinyume chake sasa, wamekuwa tegemezi wao wenyewe,eti kwa kwasababu tu tulishindwa kuwalinda harafu leo tunajidai kutoa matamko kuhusu msumbiji.

Na huu unaweza kuwa mwanzo tu, wengine watatolewa huko USA, europe na kwingine ili waje tubanane humu bongo, maana Tanzania ni kisiwa ni nchi pekee inayokana malighafi watu wake.

Kuna nchi moja ya Kusadikika ktk kitabu cha kusadikika, ilikuwa masikini sana na ikaamua kutuma wajumbe nchi zingine kujifunza huko wanafanya je mambo yao kunyooka? wajumbe walivyorudi pamoja na kupata misukosuko toka kwa mfalme, bado walielezea wanachofanya nchi zingine, na baadae mfalme alipokubali ule ushauri basi Kusadikika iliendelea sana.

Tofauti na Tanzania na kusadikika, ni kuwa Tanzania inawatuma wajumbe harafu haitaki kabisa warudi eti siyo wazalendo. Kwa kukata story short, ni kwamba mtu huwezi endelea kwa kutumia mawazo na mbinu zilezile zilizowahi kushindwa.
Iko wazi kuwa siku zote unatakaga uraia wa nchi pacha
Kwa hiyo unachofanya sasa unatumia sakata la Msumbiji kuendeleza mapambano yako ya kudai uraia pacha

Na hii apa chini ni moja ya thread zako za kupigania uraia pacha

Rais Magufuli akitaka kufanikiwa aruhusu immigrants na Dual Citizenship
 
Watanzania tulio wengi tulishasema wakati wa kuchukua maoni ya katiba mpya kuwa hatutaki hilo dubwasha la uraia pacha
Hatutaki mamluki wazidi kujaa kupitia hilo dubwasha
 
hiyo ndo majibu sasa sawia kwanini hiyo thread uliyo quote bado ina hold water. Hiyo Msumbiji ni consequences za hicho ulichochagua. Hivyo tulia, usilalamikie wamsumbiji
Umefanya tafiti kujiridhisha kwanini Msumbiji wanahangaika n.a. watanzania? Njaa iliyopo kule ni balaa
 
Tunaweza sema njaa, lakini vuguvugu litakuja hata kutokea europe na US vile vile.
 
Suala la uraia pacha lisisahaulike katika mkakati mzima wa serikali ya viwanda.

Tanzania haitapata hasara kwa uraia pacha zaidi ya faida za kutumia vizuri raslimali watu.
 
Back
Top Bottom