MWATANI
Member
- Feb 14, 2014
- 45
- 44
Watanzania wenzangu, tutambue kuwa kinachoendelea kwa sasa huko Dodoma katika Bunge Maalumu la Katiba (BMK), ni Uhaini, unafiki, utapeli, ufisadi na Uzandiki mkubwa (subversion) unaofanywa na chama tawala kinachojaribu kulazimisha kuandika katiba yenye matakwa yao na wala si wananchi,Uandaaji wa Katiba ni suala la muafaka na maridhiano kati ya pande mbili zinazo kinzana kifikra, lakini CCM kwa wingi wao uliopatikana kwa katiba mbovu na yenye viraka hawalioni ili kwa sasa, bali kuwa madikteta wa mchakato huu, Swali ni je? tunaharakisha nini kuandaa katiba itakayoendelea kulalamikiwa na na watanzania kuwa iliandaliwa na kundi lenye itikadi moja, kwa nini tusisubiri maridhiano kwanza ndo tukaendelea na mchakato huu muhimu kwa taifa, Kikwete rais wangu hachana na wapambe nuksi, tumia busara kwa hili, ili ustaafu kwa heshima na wala si kwa dharau na kebei, umeteleza kwenye ufunguzi wa bunge hili maalumu, lakini chukua hatua sasa maana bado ni mapema sana.