Kinacho endelea msako wa wahamiaji haramu

Kinacho endelea msako wa wahamiaji haramu

Mapolomoko

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2013
Posts
1,751
Reaction score
422
Kumekuwepo na ukiukwaji wa maagizo ya rais ktk zoezi hili, kwa sasa imegeuka biashara.Mfano mzuri ni Biharamulo, watanzania wenye asili ya kinyarwanda wamekamatwa na kubambikiwa kesi, MF. Mzee Budugu, huyu hajui kusoma wala kuandika hata kujaza voucher ya simu hajui.

Walienda kumpekua kwake kama anahifadhi wanyarwanda wenzie hawakukuta mtu zaidi ya watoto wake na mkamwana wake wakamwambia twende ukaandikishe maelezo kuwa hatujakuta mtu kwako na alipofika polisi wakamuweka ndani.

Wamembakizia kesi ya kufadhiri kundi la M23, inasikitisha sana kwa uonevu huu.
 
Mkuu, salaam!

Ungetulia kwanza, halafu ukaandika kwa ustadi juu ya tukio hilo ili tukusaidie njia sahihi. Kwa ulivyoeleza ni vigumu kukuelewa.

Hebu badala ya kuweka post #2 na #3 ungeihariri ile ya kwanza na ingejitosheleza mkuu wangu.

Ila pole sana kwa kuguswa, pia nawe Kiswahili chako si kizuri sana.

Pole!
 
kuna unyama unafanyika ktk zoezi hili..mtu anakamatwa njiani wanambeba anaacha nyumba na watoto peke yao baba hayupo mbaya zaidi wanachukuwa simu
 
Kuandikisha maelezo mdogowangu haihitaji mpaka ujue kuandika, cha muhimu ujue kuongea tu! Mzee atakua ameshindwa kuthibitisha kama watu walioko ndani ya nyumba yake ni watoto wake kweli!, Usihofu ataachiwa ukweli ukijulikana!

Ila sio vizuri mnagoma kwenda kwenu!,
 
harafu bado kuna watu watakuja kulalamika eti tunatengwa EAC.
kwa unyanyasaji huu tunaofanya kwa raia wa nchi majirani tutegemee kutengwa kimyakimya tu.

pia kuna watu watakuja kusema tujitoe EAC.

hizo bandari tukijenga bila kuwa na ujiran mwema na majiran tutaishia kupitisha unga tu wakina masogange.

wanaoshikwa wanafanyiwa mambo za kinyama sana. wengine ni watanzania wenzetu lakin wanalazimishwa kuwa raia wa nchi nyingine.

ukweli lazima usemwe
 
Wewe ni mnyarwanda rudi kwenyu utuachie Tanzania yetu.
 
tumewasitili muda mrefu warudi kwao ukizingatia nchi zao zimevunja ushirikiano nasi EAC wanaweza kutumwa vitu vibaya katika nchi yetu na tujifunze kuingiza watu tusiowajua
 
Inauma sana kwamba oparesheni hii imegeuzwa biashara kwa wanaoisimamia. Kuna member humu juzi kasema alipokuwa anasafiri toka Kigoma alipona baada ya kuombwa kitambulisho na kukuta jina lake kwenye leseni ya udereva ni la asili ya nyanda za juu kusini (Kina Mwa...). Angekutwa na jina la kiha au kihangaza yangemkuta makubwa.

Hata mzee Samuel Sitta ameeleza hofu yake juu ya uendeshwaji wa zoezi zima na mwisho kauliza, serikali ilikuwa wapi miaka yote hao wahamiaji haramu wakiwa humu nchini? Why today!
 
harafu bado kuna watu watakuja kulalamika eti tunatengwa EAC.
kwa unyanyasaji huu tunaofanya kwa raia wa nchi majirani tutegemee kutengwa kimyakimya tu.

pia kuna watu watakuja kusema tujitoe EAC.

hizo bandari tukijenga bila kuwa na ujiran mwema na majiran tutaishia kupitisha unga tu wakina masogange.

wanaoshikwa wanafanyiwa mambo za kinyama sana. wengine ni watanzania wenzetu lakin wanalazimishwa kuwa raia wa nchi nyingine.

ukweli lazima usemwe

Chuma ya LIGANGA peke yake inatosha kusababisha mafuriko ya mzigo hapo bandari ya bagamoyo.

Hujaweke bado kitu ya zambia na Congo.
 
Mengine yoooote nakusamehe, ila hili una uthibitisho gani kuwa si kweli? Wanyaru mnatusumbua!

Kuna uwezekano mkubwa huyo mhanga ni supporter wa m23. majority, if not all tutsis regardless wanaishi nchi gani they support m23...wengine wapo huku Dar. Wote waliokuwa wanawa support RPF miaka ya 90 kuna uwezekano mkubwa wanawa support m23 pia
 
Back
Top Bottom