Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,742
- 40,872
Sijui ni kina nani ambao hawakuwahi kuandika kuhusu utegemezi. Mimi si mmoja wao. Msimamo wangu kuhusu misaada ya kigeni haujaibuka sababu ya MCC kusitishwa kama baadhi ya watu wanataka tuamini. Kama kuandika juu ya hili nimeandika sana na tena wazi kabisa. Sijabadilika msimamo wangu. Na wengine wanalizungumzia hili la MCC leo wakati wengine tulilizungumzia miaka sita nyuma! Hili la MCC limenipa tu sababu ya kuendelea na msimamo huo huo niliokuwa nao. Ushahidi wangu upo hapa:
Niliandika hili - STOP FOREIGN AID TO TANZANIA CAMPAIGN - hili ilikuwa Nov 19, 2008. Nikimjibu Mwalimu Augustino kwenye mada hiyo nilihoji hivi "Mwalimu ni kitu gani ambacho sisi wenyewe tunaweza kukifanya kwa uwezo wetu na fedha zetu wenyewe. Unafikiri misaada ya kigeni??? imetusaidia kuendelea na kiwango cha maendeleo kinaakisi misaada tuliyopokea hadi sasa?"
Niliandika hili -ARE WE ADDICTED TO FOREIGN AID? - hii ilikuwa Feb 17, 2009. Nikaandika hivi mle "Alas! May the truth be told, as a nation we can only function at least semi-effectively as long as there is this constant flow of foreign through the veins and capillaries of Tanzania, without which we will collapse like pieces of cookies in a milk jar! We depend on this drug, we beg for it, we long for it, we sing with high pitched voices, screaming and rukarukaring like kids in a candy store. Whenever we are promised that there is some more coming we smile so wide and our eyes get teary with joy! Our desires are stirred like a man tempted by that midnight temptress in the fortress of passion! "
Katika mada iliyoanzishwa na Mzalendo Halisi Cutting Off Aid - A Condition to lift Africa from Poverty - ya Feb 24, 2009 nilichangia na kuhoji ifuatavyo: "najiulizana sana kwamba endapo misaada ya kigeni itasitishwa:
a. tutaendelea kuwa na NGOs nyingi hivi?
b. Je watanzania wanaweza kujitolea fedha zao kufanya kazi za kujitolea?
c. Itakuwaje kwenye misaada ya visima iliyoanzishwa na fedha za wahisani, tutamudu kuiendeleza?
d. Vipi kuhusu miradi mingine inayosapotiwa na wahisani nayo itakuwaje?"
Nikaandika mada nyingine WAFADHILI MMEIDEKEZA TANZANIA, BADO TUNATAKA NYONYO - hii ilikuwa ni mada ya Feb 26, 2009. Niliandika mle jambo hili "Ninachosema ni kuwa, wakati wa kutukatisha kunyonya umefika. Tayari tuna wasomi wa kutosha, tuna raslimali ya kutosha, tuna watu wa kutosha na tuna sababu za kutosha kujitegemea. Lakini zaidi ya yote tunaweza kujitegemea kwa kiasi kikubwa katika kujiletea maendeleo. Hadi hivi sasa ninachokiona ni importation of development ambapo kile tunachokiita "maendeleo" kwa kweli ni vitu tulivyocopy and paste kutoka ng'ambo! Juzi nilimsikia Waziri Mkuu akitaka watu wanunue vitunguu vya Tanzania!!! Yaani kwa maneno mengine Tanzania inaagiza hadi vitunguu kutoka ng'ambo ambayo wenyewe tunaviona ni 'bora'!" Na watu wananituhumu sijaandika kuhusu "kujitegemea"!
Niliandika tena muda si mrefu baadaye hili RAIS MWENYE MAWAZO YA KUOMBAOMBA - Hii ilikuwa Aprili 9, 2009 Nilikuwa nainukuu hotuba ya Rais na nilitanguliza kusema hivi kabla ya hotuba yenyewe "Sehemu ya hotuba ya Rais Kikwete inayothibitisha kuwa hana mawazo ya kuinua hali ya maisha ya watanzania bila ya kukinga mikono kwa nchi matajiri; asilimia 99 ya mambo anayotaka nchi matajiri zifanye kwa Afrika yanaweza kufanywa na Afrika wenyewe!"
Hiyo ni mifano tu ya nilichokisema na kukiandika humu kuhusu fikra zangu juu ya misaada ya Kigeni; kuna tofauti yoyote na nilichosema leo? Na nimeandika vingi vingine kwa mfano,
Niliandika hivi juu ya MCA ambayo ndio ilikuja mwanzo kabla ya kuwa MCC. Ni katika mada ya SYMBION POWER ACQUIRES DOWANS POWER PLANT
"tatizo liko toka mwanzo tulipokubali kuwa sehemu ya hii MCA. Wengi walifikiria kuwa MCA ina lengo la kutupa sisi uwezo na kujenga uwezo wetu wa ndani la hasha. Masharti ya MCA kama yalivyo masharti ya miradi mingine mingi tu ya Wamarekani ni kuwa fedha za walipa kodi wao ni lazima zinufaishe Marekani. Sasa mimi siwezi kuwalaumu kwa hili. Fikiria dola milioni 700 zinaweza kufanya nini Marekani? Kweli tulifikiria Wamarekani watatoa hizo milioni 700 kwa Tanzania bure tu? Kwa undugu gani?"
Na nikaongeza na kusema,
Hatuwezi kuwalaumu. Kama tungekuwa tunataka kweli iwe ni misaada ya kutunufaisha na sisi watawala wetu wangesema mapema kwenye masharti kuwa kwa kila dola moja inayopelekwa Marekani dola nyingine moja ibakie Tanzania. Lakini hatuna sera ya misaada ya kigeni Tanzania hivyo tunakuwa katika huruma ya wale wanaotoa misaada na hatuwezi kuwalaumu. Kwa wananchi wa kawaida kwa kweli hiyo haiwajalishi maana kama serikali yao imeshindwa kutatua tatizo la nishati na Wamarekani kwa kutumia fedha zao, na makampuni yao wanakuja kusaidia why not?
Sasa leo naambiwa ati sijawahi kuandika juu ya hili; na nina uhakika licha ya kuweka rekodi yangu wazi kuwa sijabadilika kama inavyodaiwa wapo wengine wanaweza wasikiri kuwa "kweli mwanakijiji msimamo wako haujabadilika juu ya misaada ya kigeni". Watajaribu kuuelezea kwa kunilazimisha nizungumzie masuala ya Zanzibar kwa mitazamo yao.
Mwaka 2003 - zingatia kuwa nimesema yale yale tangu 2008! niliandika mada iitwayo
Stop unscrupulous Foreign Aid to Tanzania campaign towards 2015. Niliandika hivi mle:
What would happen if we were to initiate such a campaign to demand that foreign aid ought to be halted until a new policy on solicitation of the same is put in place? Unafikiri CCM na serikali yake watafanya nini kampeni hiyo ikianza?
Je wrwe kama Mtanzania utaathirika vipi na usitwishaji wa misaada hiyo? Je kama kuna misaada kweli inahitajika ni ipi na kwa maeneo gani au kwa muda gani?
Unafikiri tunaweza kupiga hatua ya haraka ya maendeleo bila misaada ya kigeni?
Sasa ni kweli nimebadilika? Ni kweli sijazungumzia kuwa huru kutoka misaada ya kigeni? Ni kweli msimamo wangu wa leo unatokana na matukio ya juzi ya uchaguzi? Au ni msimamo unaotokana na kuthibitika katika kanuni ninazozisimamia. Mtu anayesoma anaweza kuamua mwenyewe bila kuongozwa na hisia za kisiasa au kisasi au kutotaka kuwa mkweli au kuogopa kusema "mwanakijiji yuko sahihi" kwa sababu ataonekana anakubaliana na mtu ambaye hakudandia mabadiliko yale feki!
Naendelea kuamini kusitishwa MCC iwe sababu tu ya kutaka kuondoka na misaada hii ya kitegemezi ya kigeni ambayo imetufanya tuwe watu tusiojiamini, wenye mawazo ya kubembeleza na ambao tuko tayari tufanywe lolote ili mradi dawa hii nzito ya kulevya iingie kwenye damu zetu!
Nitaendelea kupinga misaada ya kigeni ya aina ambayo tunapokea sasa hadi tutakapokuwa tayari kuwa na ushirikiano wa kigeni ambao msingi wake ni heshima, utu, kusaidiana na kuinuana. Na kabisa napinga misaada ya kigeni inayoingizwa kwenye bajeti ya nchi moja kwa moja au ile ambayo inakuja nje ya maeneo yale matatu niliyoyaanisha katika ile mada nyingine. Katika hili inawezekana nimebakia "mimi tu, mimi kuwaletea habari"
MMM