FirstLady1
JF-Expert Member
- Jul 29, 2009
- 16,792
- 5,375
Ndugu zangu:
· Mtoto anayeitwa Leonard Kipapi alizaliwa tarehe 05.11.2000 tukakabidhiwa tuishi naye akiwa na umri wa siku mbili (2) kufuatia kifo cha mama yake mzazi hapo tarehe 08.11.2000
· Mwezi January 2010 alipelekwa kwa baba yake mzazi huko Njombe kuendelea na shule akiwa darasa la pili
· Juzi tarehe 07.09.2010 nililetewa taarifa kwamba mtoto Leonard amelazwa katika hospitali ya Kibena (Njombe) hoi taabani baada ya kupokea kipigo toka kwa mama yake wa kambo
· Jana asubuhi (tarehe 08.09.2010) mishale ya saa moja (07:20 hours) na dakika ishirini mtoto Leonard alifariki dunia.
· Mazishi yake yanafanyika leo hii tarehe 09.09.2010 huko Njombe.
Nimewashirikisha taarifa hii ili kuonyesha hudhuni iliyonipata baada ya kupigania maisha ya kichanga Leonard hadi kufikia mwaka huu 2010 akiwa na umri wa miaka 10.
Halafu ametokea mtu Mkatili asiye na moyo wa upendo wala huruma akamponda mtoto bila sababu ya msingi hadi kufa.
Huyu ni mama wa Kambo.
Tunamwomba Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mtoto wetu mpendwa mahala pema peponi
FL1,
Dont tell me mambo haya yamekupata wewe!!
Huyo mama bado yuko huru mtaani?...Inatakiwa dunia isimame kwa muda kumhukumu huyu!
Huyo mama atakuwa hazai na hana kizazi!
Dina .......tunatembea kifua mbele vile vile. kama ukatili ni wake mwenyewe!
mwengine wanaomba waume wawe na watoto wasalimike kuzaa mwengine anapiga mpaka anaua! aggggrrr ...
Tatizo walimwengu wanatuunganisha wote humo humo, coz comment ya mtu mwingine itakuwa...'wanawake wana roho mbaya sana', tushaunganishwa wote hapo. Na kama ndio kuna huyo mtoto wa baba wa kujifunzia ndio kabisaaaa, unaonekana..ni wale wale tu!
haaa yaani hapo ndio alikuwanajifunza kumwaga mbegu? haaa! poleni sana, hapo sasa ndipo ninapowachoka baadhi ya wanawake, kwani mnalazimishwa kukaa nao kama mnaona mnawatesa hivyo?...kweli inatia huruma sana, mie napendaga tu wangu anione kama mama yake wa kumzaa kwa kweli uzazi wenyewe huu uje umfanyie mtoto wa mwenzio hayo?...RIP mtoto mzuri.....
haaa yaani hapo ndio alikuwanajifunza kumwaga mbegu? haaa! poleni sana, hapo sasa ndipo ninapowachoka baadhi ya wanawake, kwani mnalazimishwa kukaa nao kama mnaona mnawatesa hivyo?...kweli inatia huruma sana, mie napendaga tu wangu anione kama mama yake wa kumzaa kwa kweli uzazi wenyewe huu uje umfanyie mtoto wa mwenzio hayo?...RIP mtoto mzuri.....
Nafikiri ni hulka ya mtu, wakati mwingine hata mtoto huyo hakai naye na akalipiwa ada huko asomako yeye ananuna!
nina ndugu yangu nae ndio hivi kabisa,kabla ya kuolewa alikuwa anampenda kweli mtoto wa mchumba wake, alivyoolewa mambo yalibadilika, mpaka akawa ananiambia mie nakaa na mtoto wa mr vizuri kwa ajili nabembeleza ndoa, cjui hivi na vile, mie nilikuwa namuuliza kwani umeshikiwa bakora kukaa na huyo mtoto c umwambie ukweli tu babake afanye maarafi, mtoto aliondolewa hapo home kwa ajili ya matatizo kibao, yupo kwa bibi yake lakini huyu ndugu yangu akickia bibi amecal kusema mtoto anahitajika hiki na kile ananuna na ugomvi ndani, sasa unajiuliza baba mtoto alitakiwa amtelekeze mwanae kisa kaoa au nini jamani, wanawake hatutabiriki kabisa.