Kina mama tutafanya ukatili huu mpaka lini?? Inatisha na kusikitisha

Nafikiri tabu kubwa tunapata katika kuchora mstari kati ya upendo wa baba kwa mwanae na kwa mke! Hata baba mtoto akimpenda huyo mtoto kwa jinsi ya kujaza kontena futi 40 (kama upendo ungepimika), hauwezi hata siku moja kulinganishwa na upendo wa baba kwa mke! Kuikubali ndio inawawia watu ugumu, mtoto mpaka ananyimwa chakula, chakula kizuri kinaliwa na mama na wanae wa kuwazaa chumbani! Friji inahamishiwa chumbani, imagine watu wanataka kupika minyama inatokea chumbani, yaani kuna wanawake wamejaliwa roho, khaa...


sasa wa huyu ndugu yangu anatokea kumchukia kisa ni mtoto wa kiume na yeye kajaliwa wa3 wa kike, anazaa haraka haraka akitafuta mtoto wa kiume kisa mtoto wa kiume wa baba akikua baba atampa majukumu mengi kuliko wanangu(mali)....i was shocked kuckia mpaka leo watu bado wana hulka za kuchambua mtoto wa kike na wa kiume, sasa mie swali langu kubwa kwake ni kwanini hukai nae vizuri bac ili hizo mali unazozungumzia aje awashirikishe wanao(ndugu zake) vizuri huko mbeleni kuliko kutumia option ya kuzaa kuzaa....cmuelewegi kabisa.
 
Back
Top Bottom