Kina mama tutafanya ukatili huu mpaka lini?? Inatisha na kusikitisha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kina mama tutafanya ukatili huu mpaka lini?? Inatisha na kusikitisha

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by FirstLady1, Sep 14, 2010.

 1. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #1
  Sep 14, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Ndugu zangu:

  · Mtoto anayeitwa Leonard Kipapi alizaliwa tarehe 05.11.2000 tukakabidhiwa tuishi naye akiwa na umri wa siku mbili (2) kufuatia kifo cha mama yake mzazi hapo tarehe 08.11.2000

  · Mwezi January 2010 alipelekwa kwa baba yake mzazi huko Njombe kuendelea na shule akiwa darasa la pili

  · Juzi tarehe 07.09.2010 nililetewa taarifa kwamba mtoto Leonard amelazwa katika hospitali ya Kibena (Njombe) hoi taabani baada ya kupokea kipigo toka kwa mama yake wa kambo

  · Jana asubuhi (tarehe 08.09.2010) mishale ya saa moja (07:20 hours) na dakika ishirini mtoto Leonard alifariki dunia.

  · Mazishi yake yanafanyika leo hii tarehe 09.09.2010 huko Njombe.

  Nimewashirikisha taarifa hii ili kuonyesha hudhuni iliyonipata baada ya kupigania maisha ya kichanga Leonard hadi kufikia mwaka huu 2010 akiwa na umri wa miaka 10.

  Halafu ametokea mtu Mkatili asiye na moyo wa upendo wala huruma akamponda mtoto bila sababu ya msingi hadi kufa.

  Huyu ni mama wa Kambo.

  Tunamwomba Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mtoto wetu mpendwa mahala pema peponi

  NB: wapendwa sio mie ..ila yamewatokea ndugu jamaa na rafiki.
   
 2. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #2
  Sep 14, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Pole sana FL1 inauma sana wakati wengine wanafuta watoto mpaka kwa waganga wengine wanaua, inasikitisha sana yaani Lakini kuna mama wa kambo safi sana
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Sep 14, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  FL1,
  Dont tell me mambo haya yamekupata wewe!!
  Huyo mama bado yuko huru mtaani?...Inatakiwa dunia isimame kwa muda kumhukumu huyu!
  Huyo mama atakuwa hazai na hana kizazi!
   
 4. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #4
  Sep 14, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  RIP the young Leonard
   
 5. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #5
  Sep 14, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Duh....FL poleni sana.


  mfungulieni mashtaka jamani liwe funzo kwa wengine.......umpige mtoto mpaka afe! :mad2:
   
 6. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #6
  Sep 14, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Pole madame. Idadi kubwa ya wanawake (si wote) wana roho mbaya sana kwa watoto wao wa kambo. Jambo hili linasikitisha sana.
   
 7. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #7
  Sep 14, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280

  PJ hayanipata mie ila ndo hayo ya kutokea yametokea ..nimeumia sana kwa kitendo hiki..mungu aendelee kutuokoa
   
 8. D

  Dina JF-Expert Member

  #8
  Sep 14, 2010
  Joined: Sep 18, 2008
  Messages: 2,824
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Kuna baadhi ya akina mama kweli wanatukosesha ujasiri wa kuweka vifua mbele!

  R.I.P Leonard.
   
 9. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #9
  Sep 14, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Dina .......tunatembea kifua mbele vile vile. kama ukatili ni wake mwenyewe!

  mwengine wanaomba waume wawe na watoto wasalimike kuzaa mwengine anapiga mpaka anaua! aggggrrr ...
   
 10. Askofu

  Askofu JF-Expert Member

  #10
  Sep 14, 2010
  Joined: Feb 14, 2009
  Messages: 1,668
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 133
  Huyo mama afungwe jiwe la kusagia shingoni akatupwe kwenye lindi la bahari... hafai kuishi...:mad2:
   
 11. NG'OTIMBEBEDZU

  NG'OTIMBEBEDZU JF-Expert Member

  #11
  Sep 14, 2010
  Joined: Aug 11, 2010
  Messages: 845
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  FL 1,pole sana na hongera kwa kazi nzuri ya awali,Mwenyezi Mungu ni mkarimu sana,ila binadamu tu wabaya sana. (Karibu huku Kibena tule muhopeledzo)
   
 12. D

  Dina JF-Expert Member

  #12
  Sep 14, 2010
  Joined: Sep 18, 2008
  Messages: 2,824
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Tatizo walimwengu wanatuunganisha wote humo humo, coz comment ya mtu mwingine itakuwa...'wanawake wana roho mbaya sana', tushaunganishwa wote hapo. Na kama ndio kuna huyo mtoto wa baba wa kujifunzia ndio kabisaaaa, unaonekana..ni wale wale tu!
   
 13. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #13
  Sep 14, 2010
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,543
  Likes Received: 2,252
  Trophy Points: 280
  It is sad news FL1 wanawake wanakuwa wakati pale wanapokuwa wantetea maslahi yake ukiingia kwenye kumi nanne umeisha!Mfano mdogo akiwa andrive yupo kwenye haki yake jaribu kumpita kwambele uone anavyokuwa wild!i hate them japo ni mama zangu!
   
 14. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #14
  Sep 14, 2010
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  haaa yaani hapo ndio alikuwanajifunza kumwaga mbegu? haaa! poleni sana, hapo sasa ndipo ninapowachoka baadhi ya wanawake, kwani mnalazimishwa kukaa nao kama mnaona mnawatesa hivyo?...kweli inatia huruma sana, mie napendaga tu wangu anione kama mama yake wa kumzaa kwa kweli uzazi wenyewe huu uje umfanyie mtoto wa mwenzio hayo?...RIP mtoto mzuri.....
   
 15. Dreamliner

  Dreamliner JF-Expert Member

  #15
  Sep 14, 2010
  Joined: Jan 17, 2010
  Messages: 2,034
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Na utakuta hilo li mama liko mtaani linakunywa bia! Njii hii?
   
 16. Dreamliner

  Dreamliner JF-Expert Member

  #16
  Sep 14, 2010
  Joined: Jan 17, 2010
  Messages: 2,034
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Hili nalo Neno Nyamayao!
   
 17. D

  Dina JF-Expert Member

  #17
  Sep 14, 2010
  Joined: Sep 18, 2008
  Messages: 2,824
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Nafikiri ni hulka ya mtu, wakati mwingine hata mtoto huyo hakai naye na akalipiwa ada huko asomako yeye ananuna!
   
 18. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #18
  Sep 14, 2010
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  nina ndugu yangu nae ndio hivi kabisa,kabla ya kuolewa alikuwa anampenda kweli mtoto wa mchumba wake, alivyoolewa mambo yalibadilika, mpaka akawa ananiambia mie nakaa na mtoto wa mr vizuri kwa ajili nabembeleza ndoa, cjui hivi na vile, mie nilikuwa namuuliza kwani umeshikiwa bakora kukaa na huyo mtoto c umwambie ukweli tu babake afanye maarafi, mtoto aliondolewa hapo home kwa ajili ya matatizo kibao, yupo kwa bibi yake lakini huyu ndugu yangu akickia bibi amecal kusema mtoto anahitajika hiki na kile ananuna na ugomvi ndani, sasa unajiuliza baba mtoto alitakiwa amtelekeze mwanae kisa kaoa au nini jamani, wanawake hatutabiriki kabisa.
   
 19. D

  Dina JF-Expert Member

  #19
  Sep 14, 2010
  Joined: Sep 18, 2008
  Messages: 2,824
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Nafikiri tabu kubwa tunapata katika kuchora mstari kati ya upendo wa baba kwa mwanae na kwa mke! Hata baba mtoto akimpenda huyo mtoto kwa jinsi ya kujaza kontena futi 40 (kama upendo ungepimika), hauwezi hata siku moja kulinganishwa na upendo wa baba kwa mke! Kuikubali ndio inawawia watu ugumu, mtoto mpaka ananyimwa chakula, chakula kizuri kinaliwa na mama na wanae wa kuwazaa chumbani! Friji inahamishiwa chumbani, imagine watu wanataka kupika minyama inatokea chumbani, yaani kuna wanawake wamejaliwa roho, khaa...
   
 20. Beauty

  Beauty JF-Expert Member

  #20
  Sep 14, 2010
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 540
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kwakweli huu ni ukatili wa kipekee, huyo mama anastahili shahada ya ukatili, ni vyema vyombo vya sheria vikifatilia hili suala kiundani na mhusika achukuliwe hatua za kisheria, ambayo itakuwa fundisho kwa wengine.
   
Loading...