Mi nazan wazungu wanajipamba zaidi kuliko sisi, msiseme tunawaiga no! Its natural. Muulizen Cleopatra na Malkia wa Sheba enzi za Mfalme Suleman. Wanawake wa kizungu wamezidi! Lakini haisemwi! Ni wanawake weusi tu ndio wanasakamwa wakati hiki kitu ni natural. Yaani hata kama mume sina, nikiamka asubuhi naanza kujipamba tu. Angalia kabinti kako au kadada kako kama huna kabinti ka ndugu yako au jirani, kakifikisha miaka 5 hadi 9 hivi utakaona kanahangaika kujipamba. Kakivunja ungo ndio kabisaaa! Na hii ni wanawake wote dunia nzima. Sasa labda useme tu kwamba, wewe binafsi hupendi mwanamke anayeweka makucha ya bandia, mawigi n.k. lakini nakwambia, hata wanawake wa kizungu wamezidi tena wamezidi haswaaaa, sie tuna unafuu maana urembo wa asili tunao. Ukiwa hupendi, tafuta asiyeyapenda hayo pia, hayo manyongeza nyongeza yaliyozidi kwa upande wako.