Kimombo cha wazungu na changamoto zake

Wantazania someni novels za kingereza na kutizama movie za Hollywood pamoja na kisikiza BBC english. English lazima kupanda.
 
Mkuu umenivunja mbavu
 
Shukrani kwa ufafanuzi mkuu, umenifurahisha sana kugusia kimombo cha mnigeria ile ndo babu kubwa.
 


Daah mie nakumbuka naenda kuanza form I shule moja ya Catholic..tuna walimu mapadre na masista...
Dah...kuna mmoja alikuwa wa Biology..Ni muhindi ila kakaa sana Ulaya..pata picha..
V na W kuzielewa ni mziki..
Kuna wa Physics..Mmarekani..ni sheedah..Yaani the first six months..Nilimwambia bi mkubwa nahisi kama shule inanishinda.
Kuna wa Kiingereza..mmoja Mganda,mwingine Mkenya...matamshi ya a na o..
Ila inshallah after a year nilikuwa natiririka vizuri..
Kimbembe ukirudi home..mshua anakuja na migazeti yake mikubwa Daily News,Guardian,the East africcan.
Anachagua yale mavitabu ya Nyerere na columns ya kina Jenerali Ulimwengu,Onyango Obbo,Makwaia..et al..
Ananiambia nisome,niandike comprehension summary..Daah..Nguvu zilikuwa zinaisha.
Yeye he doesn't give a damn umefaulu history,maths au chemistry..so long you cant write or speak properly you don't understand..
Halafu hata hazisomi..sasa bhana mie nkawa najisahaulisha kumbe mzee ananilia timing..
Akauliza za wiki mbili ziko wapi..
I wont forget that day in my life...
Ila all in all..Nawashukuru wote kwa juhudi zao..Leo walau naeza ongea dakika 20 mbele ya umati..
Lakini tuna Language Crisis kwenye hii nchi.. Kiswahili hatukiju,cha Malkia ndo kabisa..
Tumebaki na Singeli tuu...
 
Mshua alichangia sana ktk lugha yako kwa kweli na hivyo ndio yatupasa tuwe twafatilia watoto wetu...Sio mzazi akomaa tu na ripoti za kila baada ya miezi 6!
 
Sisi waswahili ni shida Mkuu.
Anaekucheka nae hakijui lakini anakuwa wa kwanza kuwahadithia jamaa zake. Unafiki mtupu.

Mimi binafsi nilikuwa nikiwaambia hao jamaa wenye lugha yao kuwa mimi sijui kiingereza la wajifunze kiswahili lakini cha ajabu wao wanasema najua.
Nikiwauliza mbona wakati mwingine natumia nguvu nyingi ili kuhakikisha wananielewa, wao wanasema 'kwa kiwango chako unakifahamu kiingereza kwani hiyo sio lugha yako'.
Nilifarijika sana na ku-improve zaidi na zaidi.
 
Ha ha ha. mkuu uminikumbusha mbali kuna mmoja alikuwa anatufundisha A level aeleweki kabisa alafu mbaya zaidi alikuwa mkuda sana na mmbeya. Siku moja wakati anakata pindi akagongewa mlango kuufungua anakutana na nyoka kainua kichwa, alikusanya vitu vyake na kuondoka mojo kwa moja. ila jina simkumbuki
 
Me si mwalimu ila kazini kuna wazungu wa kwa malkia. Accent yao ngumu bora Americans! Akija offisin kuongea anavyoteleza ile lafudhi yao huelewi yani me ni pardon Pardon haziishi!

Mbona simpo kuwaelewa, akikubongea ung'eng'e wewe sema, Padoni sir au madamu hadi uelewe, mwisho wa siku atafunga spidi gavana mdomoni
 
Umenikumbusha ticha flani mzungu alikuwa anafundisha kemia. Copper Oxide anatamka koproksaidi. Ilikuwa balaa na vurugu kumwelewa! No wonder sikufaulu chemistry
 
Hawa ndugu kama wanakuongelesha unaeza kutamani uombe subtitles
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…