Kimeumana!! Sio bungeni tu hata mtaani

Kimeumana!! Sio bungeni tu hata mtaani

Standards Person

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2021
Posts
668
Reaction score
861
Kimeumana ndani na nje ya bunge. Baada ya siku moja Rais kuwaambia wabunge wawakosoe Mawaziri na serikali, jana mapema bungeni wabunge Gambo na Gwajima wameibuka na hoja nzito. Gambo amehoji kutopandishwa madaraja kwa watumishi pamoja na waliokua watumishi hewa kutopewa mafao yao. Tuendelee kufuatilia tutasikia mengi.

Gwajima ameelezea namna ambavyo wafanyabiashara wameumizwa na watumishi wasiokua waadilifu. Watu kibao wametishiwa na wengine kuwekwa ndani kwa uonevu. Kuhusu wastaafu kusumbuliwa naibu spika nae akatia neno. Akauliza kama mtu unachukua michango yake inakuaje mwisho wa siku unamwambia akuletee barua ya ajira? Kama humjui mbona ulikua unachukua hela zake?

Hapo akaibuka Jenista Mhagama akadai kweli wastaafu wanasumbuliwa. Huyu nae bora angetuliatu ila naona wanajitetea maana wanaogopa kuzinguliwa. Tena atulie maana sasa watakosolewa, ahsante Rais wetu. Ila kilizidi kuumana pale ambapo Jeska Kishoa alikiri kufukuzwa CHADEMA lakini naibu spika akamwambia afute kauli kwani ofisi ya spika haina taarifa hiyo, yaaaaani pale kiliumana maana mkosaji kakubali kosa lakini msuluhishi au hakimu anasema hapana usikubali kihivyo bali futa kauli lengo nikwenda na katiba aisee kimeumana.

Huku mtaani nako nipiga nikupige. Ukisikia ya Songwe kwamba DC,RC, mbunge na mwenyekiti wa CCM hakuna picha angavu kwakuwa mkuu wa wilaya ni mbabe,utajua kimeumana. Kama mbunge anafanyiwa ubabe vipi mwananchi wa kawaida au huyo mnaiyemuita mnyonge? Sasa ukisikia ya Sengerema utajua mh.Rais kazi anayo ya kuisuka nchi upya.

Eti katibu wa mbunge anaambiwa na DC asizungumzie kero za wananchi kuhusu ardhi. DC amemtishia katibu huyo kumuweka ndani bali katibu alikomaa hadi mwisho. Kama wenyewe wanaotumia maviieghty wanagombana vipi wakikutana na waendesha baiskeli na wasukuma mkokoteni kwa punda?

Mh. Rais wawakilishi wako mikoani na wilayani baadhi nivivuruge na viburi. Hawapo kwaajili ya wananchi bali kwa ajili ya matumbo yao. Kwa tanga mjini hata lukuvi alizongwa akashindwa kufanya maamuzi sahihi. Mh Rais wasaidie watanzania wanamatumaini makubwa kwako
 
Nchi yetu shida ni kubwa,sijajua ni mifumo yetu,viongozi wetu au siasa zetu!Mama tuna imani kubwa nae tena mno ila changamoto ni hivyo vitu 3 hapo!na sio mama tu hata yoyote atakaeingia hapo kama ana nia ya dhati ya kuleta mabadiliko chanya hivyo vitu 3 vinaweza kumkwamisha big time
Pamoja na yote Mungu amtunze na kumpa afya njema mama yetu!
 
Hii mivurugano ndiyo itaturudisha ktk reli.. Mama hataki kutenda yeye kama yeye Bali anataka ashauriwe then achukue hatua .. Karuhusu bunge limpe wepesi wa maamuzi
Nchi yetu shida ni kubwa,sijajua ni mifumo yetu,viongozi wetu au siasa zetu!Mama tuna imani kubwa nae tena mno ila changamoto ni hivyo vitu 3 hapo!na sio mama tu hata yoyote atakaeingia hapo kama ana nia ya dhati ya kuleta mabadiliko chanya hivyo vitu 3 vinaweza kumkwamisha big time
Pamoja na yote Mungu amtunze na kumpa afya njema mama yetu!
Tatizo kubwa ni aina ya viongozi. Wakiwa kwa wananchi muda wa kampeni nitofauti na wapokua wanawatumikia. Kuna wizara mbona kero zimepungua kama vile nishati na madini,miundombinu lakini ardhi bado lukuvi hajamaliza na huyo naibu wake duh......kweli kuna watu wanabahati
 
Nchi yetu shida ni kubwa,sijajua ni mifumo yetu,viongozi wetu au siasa zetu!Mama tuna imani kubwa nae tena mno ila changamoto ni hivyo vitu 3 hapo!na sio mama tu hata yoyote atakaeingia hapo kama ana nia ya dhati ya kuleta mabadiliko chanya hivyo vitu 3 vinaweza kumkwamisha big time
Pamoja na yote Mungu amtunze na kumpa afya njema mama yetu!
Pia unafiki ni tatizo kubwa. Mtu anaweza akamshabikia Rais leo kwakua ni waziri lakini akiondolewa anamponda Rais
 
Me nikiona wanayatenda tena kwa haraka hayo wanayo yaona saizi ndo nitawaona wamepevuka, lakin nikiona bado wanademka ili kutafuta huruma ya Rais.....wakwende huko.

Ila uongo mbaya jamani Jiwe asingekufa haya tusinge yasikia kabisa ni bora kaenda zake.
 
Kama taifa tusipofata sheria zetu hatuwezi kwenda popote ndomana utaona hata mambo ambayo yakuangalia sheria ama katiba inasemaje watu tunataka mkuu wa nchi aseme .msaada kwamama ni bunge bila bunge hawezi kufanya anayotarajia
 
Kimeumana ndani na nje ya bunge. Baada ya siku moja Rais kuwaambia wabunge wawakosoe Mawaziri na serikali, jana mapema bungeni wabunge Gambo na Gwajima wameibuka na hoja nzito. Gambo amehoji kutopandishwa madaraja kwa watumishi pamoja na waliokua watumishi hewa kutopewa mafao yao. Tuendelee kufuatilia tutasikia mengi.

Gwajima ameelezea namna ambavyo wafanyabiashara wameumizwa na watumishi wasiokua waadilifu. Watu kibao wametishiwa na wengine kuwekwa ndani kwa uonevu. Kuhusu wastaafu kusumbuliwa naibu spika nae akatia neno. Akauliza kama mtu unachukua michango yake inakuaje mwisho wa siku unamwambia akuletee barua ya ajira? Kama humjui mbona ulikua unachukua hela zake?

Hapo akaibuka Jenista Mhagama akadai kweli wastaafu wanasumbuliwa. Huyu nae bora angetuliatu ila naona wanajitetea maana wanaogopa kuzinguliwa. Tena atulie maana sasa watakosolewa, ahsante Rais wetu. Ila kilizidi kuumana pale ambapo Jeska Kishoa alikiri kufukuzwa CHADEMA lakini naibu spika akamwambia afute kauli kwani ofisi ya spika haina taarifa hiyo, yaaaaani pale kiliumana maana mkosaji kakubali kosa lakini msuluhishi au hakimu anasema hapana usikubali kihivyo bali futa kauli lengo nikwenda na katiba aisee kimeumana.

Huku mtaani nako nipiga nikupige. Ukisikia ya Songwe kwamba DC,RC, mbunge na mwenyekiti wa CCM hakuna picha angavu kwakuwa mkuu wa wilaya ni mbabe,utajua kimeumana. Kama mbunge anafanyiwa ubabe vipi mwananchi wa kawaida au huyo mnaiyemuita mnyonge? Sasa ukisikia ya Sengerema utajua mh.Rais kazi anayo ya kuisuka nchi upya.

Eti katibu wa mbunge anaambiwa na DC asizungumzie kero za wananchi kuhusu ardhi. DC amemtishia katibu huyo kumuweka ndani bali katibu alikomaa hadi mwisho. Kama wenyewe wanaotumia maviieghty wanagombana vipi wakikutana na waendesha baiskeli na wasukuma mkokoteni kwa punda?

Mh. Rais wawakilishi wako mikoani na wilayani baadhi nivivuruge na viburi. Hawapo kwaajili ya wananchi bali kwa ajili ya matumbo yao. Kwa tanga mjini hata lukuvi alizongwa akashindwa kufanya maamuzi sahihi. Mh Rais wasaidie watanzania wanamatumaini makubwa kwako
Hili la wastaafu wanapodai mafao yao ni la-kuangaliwa na kufanyiwa mabadiliko. Ni kweli kabisa haingii akilini kuwa mtu mafao yanapelekwa, akitaka statement anapewa bila usumbu wa kuambiwa arudi kwa mwajiri, cheki namba anayo, kitambulisho cha taifa anacho N.K..... halafu wakati wa kudai analetewa mizengwe na usumbufu usio na sababu za MSINGI. Hili Serikali inabidi kuliangalia na kuja na mfumo ambao ni flexible na usikokuwa na makandokando. Otherwise achaneni na mafao na mishahara iwe ya viwango.
 
Wabunge wetu comedy sana,

Sasa huyo Kishoa anavyokiri kuwa Kafukuzwa anaendelea kufanya nini Bungeni si ajiuzulu Ubunge.

Yaani unakiri kufukuzwa halafu unazungumzia hayo ndani ya Bunge.

Toka ukazungumzie kwenye press tuone unamaanisha na sio kutupiga kiswahili cha kisanii as if katekwa??
 
Kwani aliyemwapisha hajui kuwa huyu si mwanachama wa chama chochote kwa sasa?
 
Haamini kama mpaka sasa mama amewaacha
 
Kwani aliyemwapisha hajui kuwa huyu si mwanachama wa chama chochote kwa sasa?
Kwani huwa anapohudhuria Bunge wanafanya kumteka??

Si huwa anajipeleka mwenyewe Bungeni??

Nini kinamzuia kujiuzulu??
 
Huyo binti anajijua rohoni kuwa alitenda kosa kwa kukisaliti chama chake, hivyo anaweweseka.Aibu na iwe kwake na wenzake 18
 
Back
Top Bottom