Kimeo kipya cha JK China balozi aliyelala usingizi mpaka sasa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kimeo kipya cha JK China balozi aliyelala usingizi mpaka sasa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nderingosha, Jun 13, 2012.

 1. n

  nderingosha JF-Expert Member

  #1
  Jun 13, 2012
  Joined: Mar 20, 2011
  Messages: 3,546
  Likes Received: 1,327
  Trophy Points: 280
  • Kama tulivyotabiri baada ya uteuzi wa mchovu Philip Marmo kuwa balozi china….tayari dalili za udhaifu wake kama balozi wa TZ uchina zimeshaanza kujitokeza kwa kasi ya ajabu…..China..nchi yenye uchumi imara na wa kasi zaidi duniani….nchi yenye watu wajanja wajanja ambao wanatumia sana udhaifu wa wengine kujinufaisha…iwe kiuchumi kama nchi au hata kibinfsi…kila mtu kwa nafasi yake…Kwa muktadha huu…wengi walitegemea balozi wetu kule uchina awe mtu makini na aweze kulinda interests za TZ na watu wake kule uchina….jambo ambalo linaonekana kuwa bado ni kitendawili kwa muda mfupi tu huyu jamaa aliokaa kule china…Nasema hivi kwani watu makini lazima wafatilie nyendo za utendaji wa ubalozi wetu kule china….hasa ikizingatiwa kuwa kwasasa TZ imekuwa inafanya deals nyingi za kimagumashi kule china…rejea mikataba tata….manunuzi tata….biashara tata….etc etc ..Mambo (indicators) machache yanayonifanya nianze kuhoji utendaji wa huyu balozi kule uchina ni kama ifuatavyo……  • Tangu amefika uchina…balozi Marmo mpaka sasa hajakutana wala angalau na watanzania walioko uchina….wawe wanafunzi au wafanya biashara…..sasa huyu anamsubiri rais JK aende uchina ndio akutane na watanzania au vipi???...yeye balozi anawakilisha interests za nani uchina kama mpaka sasa ameshindwa hata angalau kuitisha mkutano na watanzania????....nina taarifa kuwa kuna jitihada za wanafunzi kule uchina za kukutana na balozi lakini hakuna initiative yoyote toka kwa balozi mwenyewe ya kukutana na wanafunzi…..haswa ikizingitiwa kuwa yeye ni mgeni china na labda kuna mengi ya msingi ya kuisaidia TZ na pia kusaidia utendaji wake angeweza kujifunza toka kwa wanfunzi ambao ndio msingi mkubwa wa maendeleo ya TZ…..China ina wanafunzi wengi saana watanzania kuliko sehemu yoyote duniani…..hawa ni nguvu kazi ya kuangalia sana…na ni hili ni jukumu la balozi……

  • Tayari kuna taarifa(hazijathibiishwa)kuwa kuna wafanyabiashara wamepigwa vibaya na wachina hivi majuzi kule Guanzhou…mji ambao watanzania wengi wafanyabiashara hushukia na kuchukua mzigo….biashara kubwa kule kariakoo hutoka uchina…haswa katika mji huu wa Guanzhou…..sasa kama kuna taarifa ya wafanyabiashara kupigwa kule hii si nzuri na tungetegemea kusikia tamko la ubalozi wa TZ kule uchina…lakini kinyume chake tunasikia habari hizi kwenye magazeti..tena ya udaku….wakati kuna uwezekano kweli kuwa watanzania hawa wemepigwa……..soma habari hii (pamoja na kuwa yaweza kuwa udaku): WABONGO WALA KICHAPO CHINA - Global Publishers

  • Kuna taarifa za wanafunzi wa kitanzania uchina kupata shida kubwa ku access mtandao wa bodi ya mikopo TZ..yaani OLAS….jambo lililopelekea wanafunzi kulalamika sana na hata kutuma habari bodi ya mikopo moja kwa moja….mpaka ikabidi wanafunzi wasaidiane wao kwa wao kwa kumtumia mwenzao ambaye ana direct contact na bodi ya mikopo…haya yoote yamefanyika wakati ubalozi wa TZ kule uchina upo….Sasa ubalozi wa TZ unawakilisha interests za nani???kama jambo kama hili nalo wanafunzi wameona ubalozi ni helpless mpaka wakachukua jukumu wenyewe (kwa contacts zao)kuweza kusaidiana!!.......Kama balozi angekuwa ameonana na wanafunzi jambo hili angekuwa ameabiwa na kulifanyia kazi kwa wakati…kwani halijatokea mara moja kwa wanafunzi hawa….na matokeo yake siku zote ni kwa wanafunzi hawa kucheleweshewa fedha zao za mikopo toka bodi…..

  Kwa hizi indicators chache nilizotaja…nashawishika kusema kuwa balozi Marmo bado amelala….na ni wakati sasa kwake kuamka na kuchapa kazi aliyotumwa..kwa kuanza na kushughulikia kero kadhaa zilizopo…pamoja na kulinda maslahi ya TZ na watanzania kule uchina…..vinginevyo…hatutamwamini kuwa anawakilisha interests za TZ uchina…..nawasilisha…
   
 2. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #2
  Jun 13, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Sasa kupigwa wafanya biashara kuna uhusiano upi na Marmo? Wachina hata hapa wanapiga watu, umesahau kuwa walintandika mpaka mkuu wa kituo cha polisi? Kama huna cha kuandika ondoa hii maji taka.
   
 3. Mkirua

  Mkirua JF-Expert Member

  #3
  Jun 13, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 5,667
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Vyeo vingine si vya kufutana machozi tu?? What do you expect out of a person like Marmo?? wala sishangai...
   
 4. BIG Banned

  BIG Banned JF-Expert Member

  #4
  Jun 13, 2012
  Joined: May 4, 2012
  Messages: 263
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Huyo jamaa angeenda pumzika tu achunge ng'ombe kule Mbulu. amechoka sana.
   
 5. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #5
  Jun 13, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Kama namuona mzee Marmo full kuchoka na ongea yake kama mchungaji!
  Unajua ivi vyeo sometimes ni kupeana ulaji tuu!
  Kabla sijaendelea ivi mpaka sasa ana mda gani uko China ili tuanze analyse
   
 6. Bondpost

  Bondpost JF-Expert Member

  #6
  Jun 13, 2012
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 1,981
  Likes Received: 508
  Trophy Points: 280
  We kweli unaendana na ID yako! Hayo yaliyotanabaishwa hapo juu ndiyo haswa mojawapo ya majukumu ya balozi.
   
 7. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #7
  Jun 13, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Bondpost, Kitu unachoshindwa kuelewa ni kuwa kupigwa kwa mfanya biashara ni matukio ambayo yanataka wafanya biashara waelimishwe na hususan chombo chao kinachowaunganisha na biashara za nje, mfano chamber of commerce. Utakuta hawa wafanya biashara hata chamber of commerce hawaijui ni nini. Utakuta hao wafanya biashara wanakwendaa China lakini hakuna anaekwenda ku ripoti ubalozini kuwa nipo hapa China na nipo sehemu fulani na nimekuja kwa biashara fulani ili apewe maelekezo na maafisa wa biashara waliopo hapo. Wao wanajiendea tu, halafu uje kumlaumu Balozi? Wafanya biashara wengi wa Kitanzania hususan hawa wenye vimtaji vidogo, huwa wanakwenda kukaa sehemu ambazo ni za rahisi na hazina hadhi ya kukaa wafanya biashara, mfano utoke hapa kwenda Nairobi akakae Kibira (Kibera), akipatwa na maafa umsakame Balozi? Pia kuna Watanzania wachache wanajihusisha na biashara haramu za madawa ya kulevya, na hizo biashra zina madhara yake, juzi juzi tumesikia Mtanzania kahukumiwa kifo na wapo ambao wapo jela kwa sasa wanangoja hukumu zao au wanatumikia vifungo kwa makosa mbali mbali, nayo utamlaumu Balozi? Kuna mchina aliuliwa hapa Tanzani juzi juzi, Jee, tumlaumu Balozi wa China? Wacheni kuwa wafinyu wa fikra, cha kufanywa ni kujuwa ubalozi unashghulikia vipi haya mambo na sio kuja na kuanza kumlaumu Rais na Marmo. Kuna Mtaliani juzi kalalamika hapa JF udhalim aliofanyiwa hapo Tanga, Tanzania, kapigwa, kawekwa jela, kafukuzwa nchini. Jee tumlaumu balozi wa Italia?
   
 8. m

  mabhuimerafulu Member

  #8
  Jun 13, 2012
  Joined: May 29, 2012
  Messages: 89
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  No, hamjamwelewa. Uteuzi wa wastaafu kuwa mabalozi haya ndo matokeo yake. Wengine huchukulia ubalozi kama sehemu ya likizo. Inawezekana kabisa Marmo hawezi kazi hii, tena China, China?
   
 9. Wingu

  Wingu JF-Expert Member

  #9
  Jun 13, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,326
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Watanzania mnapenda sana kulalamika mtu kateuliwa juzi tu tayari mmemshushia lawama.Kwani wewe hujui ofisi za ubalozi wa Tanzania uwende ukamweleze shida zako kuliko kusubiri uandaliwe mkutano?Saa nyingine chukua uamuzi mwenyewe sio kulalama tu mnachosha.
   
 10. Bondpost

  Bondpost JF-Expert Member

  #10
  Jun 13, 2012
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 1,981
  Likes Received: 508
  Trophy Points: 280
  Ndiyo maana narudia tena kukueleza kuwa hizo ndiyo kazi za balozi, watanzania wanapoenda china wakuwapa info ni hao uliowataja ila akiwepo na balozi. Ndio maana ubalozi wanatakiwa kuwapa maelekezo na misaada hata kama mtu alistole way as long ni mtanzania mnatakiwa kumsaidia. Ndiyo maana tunakuwa na military attaches, political attache na wengineo katika ubalozi. Nitakupa mfano ujue kazi ya balozi, kuna yule muingereza alishtakiwa hapa Tanzania lakini serikali ya uingereza kupitia balozi wao wakafanya diplomacy wakafanikiwa yule bwana akaenda kuhukumiwa kule uingereza. Yani kazi sio kwenda na kuwaambia wachina waje huku bali anatakiwa kusafeguard interests na security ya kila mtanzania. Ukitoa mfano wa muitaliano au yule mchina nadhani unasahau diplomacy iliyofanyika mpaka viongozi wa juu kwenda msibani, lazima ubalozi wao ulifanya correspondence na ikulu sio bure aisee.
   
 11. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #11
  Jun 13, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Bondpost Kwa hiyo unakubaliana na mimi kuwa balozi kazi yake ni diplomacy lakini sio kuzuwia madudu wanayofanya wenyewe Watanzania. Huwezi kumalumu balozi kwa kipigo alichopewa mtanzania hujui kwanini kapigwa. Pengine ana daiwa, pengine kapeleka unga mbovu, pengine kafumaniwa? Kama nilivyokueleza mwanzo, Watanzania wengi hata ubalozini hawa ripoti au hilo nalo ni la kubisha? Tuwe wa kweli na tusitetee kila kitu, hata kama makosa ni yetu. Sio Rais wala sio balozi wa kulaumiwa kwa vitendo vyetu. Ni kama mjombako akaie hakafu wewe uhukumiwe, utakubali hayo?
   
 12. Bondpost

  Bondpost JF-Expert Member

  #12
  Jun 13, 2012
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 1,981
  Likes Received: 508
  Trophy Points: 280
  Unajua mabalozi wengi hawafanyi kazi zao ipasavyo yani ni mzigo mwingine kwa taifa. Nakumbuka wakati nafanya masters degree Russia nilikuwa na mwanamke Sweden nikaendesha gari kutoka Russia pale ni karibu. Nilipata ajali Sweden wakati narudi chuo, nimepelekwa hospitali na wale wazungu wakanihudumia kila kitu, nilipopata nafuu wakajaribu kuwasiliana na ubalozi wa Tanzania kipindi hicho balozi alikuwa mume wa huyu Prof. Tibaijuka, yule mzee alikataa kutoa msaada wowote kwa kusema yeye hana taarifa na mimi hata kama ni mtanzania, akanitukana kuwa kama nimeenda Russia kusoma kwa nini nizurure sweden yani na masimango mpaka wale waswede wakanipa pesa ya matumizi na wakanipatia tiketi ya ndege first class nikarudi chuo. What am trying to say here ni kuwa balozi anatakiwa kuwa mtu wa diplomacy, anayejua diplomacy sio kusubiri ten percent za mikataba. Hata mtanzania anauawa marekani yule dada kachomwa kwenye gari, hata balozi kutoa tamko la kulaani hajahangaika zaidi nae anatoa majungu kuwa unajua vijana wanataka kuolewa na wazungu ili wapate uraia! Huyo ni diplomat kweli au ni mp.um.ba.vu? Hivi kama mtanzania anakamatwa china kuna mikataba mingapi tunayo baina yetu ya exchange of prisoners ambayo balozi anatakiwa kuifatilia? Mtanzania hata akikaa kibera hapo Nairobi kuna shida gani eti siku akipigwa then we balozi usihangaike kulaani mauaji ya mtanzania na kuitaka serikali husika kufanya upelelezi kisa eti akome kukaa kibera? Nadhani kuna watu hamjui kazi za balozi na majukumu yake ya day to day. In short ni kwamba ningekuwa kwenye laptop ningekutumieni topic fulani niliisoma wakati nafanya course ya International Diplomacy and Protocol, hayo yamo na pia ukisoma Public International Law, kuna topic ya international diplomacy na kwa bahati nzuri nimeyosoma hayo UD na Kurasini. So unapoongelea diplomatic relation haiishii kusema unasubiri mtanzania aje kujitambulisha kwako, imagine unatoka TZ unaenda Guangzhou, ubalozi upo Hongkong then una VISA ya wiki, umeenda kibiashara, ukaanze kuweka appointment na balozi na wanavyokuwa na maringo si visa itaexpire? After all kuna haja ya kwenda kwa balozi? Ndo maana kuna tourist info centres! I still believe that mzee ataleta politics kwenye mambo ya diplomacy, ninaweza kusema katika mabalozi unaoweza kuwaona kiurahisi ni Cisco Mtiro, sio hao wengine maana hawafanyi kazi, ukiwafuata hata kama umeishiwa ulaya sasa unaomba msaada wa kurudi nyumbani hawakusaidii, ukiwa unamatatizo hawakusaidii then kuna haja ya kupoteza kodi ya watanzania kumlipa huyo mtu?
   
 13. k

  kindafu JF-Expert Member

  #13
  Jun 13, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,114
  Likes Received: 866
  Trophy Points: 280
  Wakuu, naomba kujuzwa kidogo - hivi hawa wanaoteuliwa kwenye CV zao kuna popote inapoonyesha waliwahi kupitia Chuo chochote cha Diplomasia?? Na kama sio, uteuzi wao ulizingatia vigezo gani???
   
 14. Bondpost

  Bondpost JF-Expert Member

  #14
  Jun 13, 2012
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 1,981
  Likes Received: 508
  Trophy Points: 280
  Yani ni kwamba hata kama ulikuwa unadaiwa na hao wachina au walichukuliana mabibi, haitoshi balozi kukaa kimya na kuona ni sawa mtanzania kupiga na kudhalilishwa. Kumbuka hapa TZ yule mchina aliuawa na majambazi ila uliona diplomacy iliyofanyika? Hivi kuna watanzania wangapi wanapata tabu kwa kudhalilishwa huko ulaya na mabalozi wanaota mavitambi tu? Ukienda kuomba appointment mpaka mwezi uishe? Ninachofahamu ni kuwa balozi anatakiwa kwanza kabisa kuangalia maslahi ya taifa lake na wananchi wake then mengineyo yanafuata sasa iko wapi welfare ya watanzania? Kumbuka mleta mada anakuambia kuwa toka amefika hajawahi kuita watanzania waliopo china kuongea nao! Ajue changamoto wanazokutana nazo nk! Mtu anashindwa ku-access mkopo wa elimu ya juu wakati alichaguliwa na ubalozi haushughuliki! Sasa huyo balozi tumempeleka kufanya nini? Na huyo ni mmojawapo ila wengi hawakai kusafeguard the best interests za taifa, wanatanguliza matumbo tu!
   
 15. n

  nderingosha JF-Expert Member

  #15
  Jun 13, 2012
  Joined: Mar 20, 2011
  Messages: 3,546
  Likes Received: 1,327
  Trophy Points: 280
  eh eh you puto!!!!unamtetea nani hapa sasa????.....don't contribute to this thread if you have nothing to offer.....puto!!....you are there sitting in Dar and pretend to answer for the status quo!! puto!!!..who is gonna speak for Tanzanians if they have problems abroad???..if not their embassy?.......we unaijua diplomacy we puto!!.. durak!! cyka!!
   
 16. Bondpost

  Bondpost JF-Expert Member

  #16
  Jun 13, 2012
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 1,981
  Likes Received: 508
  Trophy Points: 280
  Kwa ukweli kwa TZ sina uhakika kama vigezo huzingatiwa lakini pamoja kuwa balozi anatakiwa kuwa mtu mwenye busara, anayeheshimika kwenye jamii na mengineyo, pia ni vizuri angekuwa na background ya masomo ya diplomacy, protocol au international law au international relations. Kinachoonekana siku hizi ubalozi ni kama vile wanakuwa hakuna pa kukuweka ule national cake ndo wanakupa huko ukakae ughaibuni, wakati balozi hatakiwi kuwa mhuni hata kuonekana kumbi za starehe, never! Sijui vigezo vya uteuzi, hapa labda mh. Rais ndo anajua.
   
 17. k

  kindafu JF-Expert Member

  #17
  Jun 13, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,114
  Likes Received: 866
  Trophy Points: 280
  Kama mtu hajapitia Chuo chochote cha Diplomasia halafu anatumwa kufanya kazi za ki-diplomasia kwenye nchi kama China ambayo inajulikana duniani kote unatarajia nini? Nafikiri wa kulaumiwa zaidi ni huyo aliyewateua!
   
 18. Bondpost

  Bondpost JF-Expert Member

  #18
  Jun 13, 2012
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 1,981
  Likes Received: 508
  Trophy Points: 280
  Nimemshangaa sana kuona anamtetea balozi anayekaa kimya kusema hao watanzania kama wamepigwa watakuwa walevi au walifumaniwa! What a shame mtu anateuliwa then mpaka leo hajazungumza na watanzania? Sasa wale si ndo alitakiwa kuzungumza nao ili aweze kujua nini cha kushughulikia? Unajua mtu ambaye hajawahi kupata kushuhudia jinsi watanzania wanavyopata tabu ughaibuni halafu hakuna pa kusemea hawezi jua lolote. Ila ninaamini mabalozi wengi ni ex politicians ndio maana maamuzi yao yanakuwa kisiasa zaidi badala ya kuwa kidiplomasia!
   
 19. k

  kindafu JF-Expert Member

  #19
  Jun 13, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,114
  Likes Received: 866
  Trophy Points: 280
  Mkuu, waliowaza kuanzisha Vyuo vya Diplomasia hawakuwa wajinga! Wajinga ni hao wanaoteua bila kuzingatia vigezo muhimu!! Tafakari!
   
 20. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #20
  Jun 13, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Nderingosha, You simply do not understand what diplomacy is, I feel pity for you. A diplomat can only facilitate and advose you on the best ways to conduct your business in China if you register to him and go with particular requests, A diplomat can never come and rescue you when you are not even known to exist in China. You simply do not know what diplomacy is. You screw up in China you pay for it not the Ambassador nor The President. Bu diplomasinin ne olduğunu bilmek çalışmasını durdurmak
   
Loading...