Bondpost
JF-Expert Member
- Oct 16, 2011
- 6,587
- 9,324
Kama mtu hajapitia Chuo chochote cha Diplomasia halafu anatumwa kufanya kazi za ki-diplomasia kwenye nchi kama China ambayo inajulikana duniani kote unatarajia nini? Nafikiri wa kulaumiwa zaidi ni huyo aliyewateua!
Nadhani wizara ya mambo ya nje ndiyo inahusika zaidi hapa, unajua zamani ulikuwa unasikia mtu ni diplomat yani walikuwa wanaogopwa maana walikuwa ni watu wenye heshima kubwa sana kwenye jamii. Nadhani sasa kuna haja ya kuangalia upya ajira ya ubalozi maana asidhani kateuliwa kwenda kuomba misaada tu au kuiuza nchi kwa wawekezaji, ubalozi ni zaidi ya hapo, kuna mambo ya kijeshi, mawasiliano, elimu, biashara nk. Mtu anashindwa hata kuandaa students exchange program? Anashindwa kuandaa tour ya vijana kwenda kuangalia mambo mbalimbali ya uchumi na teknology? Hata kutoa tamko fulani hatusikii? Sasa hawa ni wanakuwa ni wanasiasa au ma-diplomats?