Hyungnim
JF-Expert Member
- Sep 25, 2016
- 301
- 482
Kimbwanga; sehemu ya 1
Mtunzi: (Hyungnim)
Alifahamika kwa jina la Anko Mavi!jina hilo la mzaha alilipata kutokana na kazi yake ya kuchimba vyoo,kuvizibua vyoo vilivyojaa lakini pia kuyabeba 'mavi'ooh ashakum si matusi nilipaswa kuandika kinyesi kwenye toroli na kwenda kuyatupa mbali...jina hilo likawa maarufu kuzidi jinale Athumani Ngabhire alopewa na wazaziwe. Anko mavi likamkaa sawia,likamea na kukita mizizi huku Athumani likipotelea kuzani.
Kibarua hiki licha ya ugumu wake kilimtwalia kipato.Akapata faranga zilizopiga jeki familia! Mkono ukaenda kinywani lakini pia akamudu kumtunza mkewe mama Sayona.
Licha ya ufukara wake Anko Mavi alijaariwa kuwa na mke kipusa bwanaa!kwa rangi alikuwa mweusi tii mithili ya chungu cha mzee Matumbawe.Alijaaliwa kuwa na makalio makubwa hasa yaliyokuwa ya mviringo mithili ya pia.Umbile lake lilikuwa kama mwanamke maridhawa alofinyangwa akafinyangika.Kiuno cha kukata na shoka jimama la kidigo hilo.Uso wake ulichukiza kidogo kila jamali alomtazama usoni alikunja USO kwa ghadhabu ila alisawijika pindi machoye yaliponasa rasilimali ya makalio.uso wa mtazamaji unasawijika na kujaa nuru angavu.Hivyo mkewe akavuma kwa jina la mama pia kumaanisha mviringo wa rasilimali makalio ulofanana na pia.
Siku hii Anko Mavi kwa kufuata kaida yake alijitoma kibaruani,kayajaza mavi kwenye toroli na kuchanja mbuga akikata mitaa kuyapeleka yanakostahili.Alisukuma toroli uso kaushupaza na kuukaza kwa hasira na chuki.Ni wazi hakukihusudu kibarua hiki.Akawaza haraka na filamu ya kukera ikatambaa mawazoni mwake.Akajiona yupo afisi za benki.Akiwa ktk msururu mrefu wa watu anaulizwa na mtoa huduma ...
Meneja:jina lako,umri,mahali uishipo,kazi na shida yako..Fanya haraka.
Anko mavi: aaaah...umri wangu ni miaka 49 na jina langu ni anko mavi na kazi yangu ni kubeba mavi kutoka vyoo vilivyojaa na.....
Vicheko vinasikika kutoka kwa kina dada warembo,anaghadhibika na kurusha ngumi,anadhibitiwa na bawabu.
Alishtuka na kusononeka.Akashukuru kuona ukikuwa mzugo ombwe wa mafikara yake.Akazikaza hatua akiwa ndani ya masulupwete,miguu kaisopeka makobazi jasho likimchuruzika toka kwapani na kutengeneza michirizi yenye chumvichumvi ilozidi kuupausha uso.Maisha ya akina pangu pakavu tia mchuzi...
Ghafla kundi la watoto watoto linajitokeza na kuanza kumkebehi."Anko mavi huyooo katinga masulupwete huyooo.Jazba zinampanda na anajikuta akifura kwa hasira na kuanza kuwafukuza.Lengo lake awakamate na kuwatia henzirani,ili waadabike.
Haya sasa mtanange huo.Ni kukurukakara za Anko Mavi na watoto.Wanampiga chenga huku wakizomea,anafura zaidi,hakati tamaa anapagawa zaidi lakini haachii toroli.Anakimbia nalo na kupepesuka huku na huko,misuli ya mikono kaiimarisha.
Ghafla wanatokeza kwa Mzee Hamduni mkaanga mihogo akiwa na wateja tele.Anko mavi anaashindwa kuhimiri kukata kona na hivyo anakwenda kujitoma ktk kundi la wateja wa mihogo,wanamkwepa na toroli linabinuka na kwenda kufunika kalai la mihogo itokotayo motoni.Mavi yanatuama kwenye kalai na hivyo kufanya mseto wa mihogo,mavi na mafuta ya mawese.Mlio wa pyuuu unasikika,ishara ya mseto huo kutokota na kuwiva.Harufu nzuri ajabu inatawala anga lote na eneo jirani na kijiwe cha Hamduni mzee.
Mzee Hamduni anahamanika na kumkumba Anko mavi.Wanaanza kuzichapa na mkaanga mihogo anasokomezwa kwenye toroli na kupakazwa masalia ya mavi,wanunuzi pamoja na wale watoto waovu wanasukamana kwa Shari kugombea mihogo ilochanganywa na mavi na kutoa harufu nzuri.
Zogo linazidi kukua na watu wanaongezeka kugombea mihogo.Migambo na sungusungu wanajongea eneo la tukio kutuliza ghasia.Anko mavi anahamaki kuwaona migambo anagwaya na kulikamata toroli kikamilifu na kutimua mbio.Mzee Hamduni analia kwa uchungu biashara yake kuharibika anakamata kipande kidogo cha mhogo kilichopakazwa mavi na kukifumbata mdomoni na kukitafuna.Anaukunjua uso kwa tabasamu pana anapogundua mhogo ni mtamu.Fikara za kuimaisha biashara yake kwa kukaaanga mihogo kwa mavi zinamtawala.Anaondoka kurejea kwake,mkononi ana kalai na vipande viwili vya mhogo,ampelekee mkewe mama Safari.Mluzi haukauki mdomoni mwake.
Je,umeishia kwa kukenua meno?
Hyungnim...