Kimbunga cha MELISSA chakaribia Jamaica, watatu wafariki

Kimbunga cha MELISSA chakaribia Jamaica, watatu wafariki

tonicimmobility

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2025
Posts
493
Reaction score
1,038
tracking_1761623588032_hpEmbed_2_20x11.jpg

Soma pia: Kimbunga Ragasa chafika China baada ya kuua watu 17 Taiwan

Kimbunga kikali kilichopewa jina la “Melissa” kinaripotiwa kuikaribia Jamaica kikiwa na kasi kubwa ya upepo na mvua nyingi. Wataalamu wa hali ya hewa wanasema kuwa kimbunga hicho ni dhoruba kali zaidi duniani mwaka huu, na huenda kikawa kimbunga kibaya zaidi kuwahi kuikumba Jamaica.

Kwa mujibu wa Kituo cha Habari Kimataifa cha #AlJazeera, leo Oktoba 28, 2025, Kituo cha Kitaifa cha Vimbunga cha Marekani (National Hurricane Center - NHC) kimesema kimbunga hicho ni dhoruba ya kiwango cha juu kabisa cha hatari, kikiwa na kasi ya upepo wa hadi kilomita 282 kwa saa.

Wataalamu wa kituo hicho wamesema kuwa kimbunga hicho kimeendelea kuongezeka nguvu kutokana na joto la juu la bahari katika eneo la Karibea, jambo lililochangia kuipa nguvu zaidi dhoruba hiyo.

kimbunga hicho kinaripotiwa kujongea kwa mwendo wa taratibu chini ya kilomita tano kwa saa, hali inayoashiria kuwa maeneo yatakayopitiwa yatakumbwa na mvua kubwa kwa muda mrefu, na hivyo kuongeza hatari ya mafuriko makubwa pamoja na maporomoko ya ardhi.

Mamlaka nchini Jamaica zimefunga viwanja vya ndege, shule, na huduma nyingine za umma. Vituo vya dharura na makazi ya muda vimefunguliwa kwa ajili ya kuwahifadhi wakazi waliolazimika kuondoka makwao. Inaelezwa kuwa serikali pia imetenga bajeti ya dharura kusaidia juhudi za uokoaji na utoaji wa misaada.

Kituo cha Kitaifa cha Vimbunga Marekani pia kimeonya kuwa mawimbi makubwa na hatari ya baharini yanaweza kufikia hadi futi 13 katika maeneo ya pwani ya kusini mwa Jamaica, hali inayotishia maisha ya wakazi wa maeneo ya karibu na bahari.

Ripoti zinaeleza kuwa watu wengi nchini Jamaica tayari wamehamishwa kutoka maeneo hatarishi, huku wengi wakiwa na wasiwasi kwa siku kadhaa wakisubiri kuona nini kitatokea baada ya dhoruba hiyo.

Hadi sasa, watu watatu wameripotiwa kupoteza maisha nchini Jamaica kutokana na kimbunga hicho, huku wengine wanne wakifariki dunia huko Haiti na Jamhuri ya Dominika.
 
Mellisa? Hii itakuwa ni kimbunga jike hiki, kile cha ukanda wetu kilichoitwa chenge kimeishia wapi?
 
Mwaka 2021 wakawa wanatuonesha hata kwenye rada zao kimbunga kikaliiii. Na video za AI na matukio ya kuungaunga wakosema ni mtwara. Wakazuia hata doria za majini.

Boooom🔥🔥🔥🔥 tani moja ya dawa za kulevya ikadakwa. Na habari ya kimbunga ikaishia hapo.
 
Back
Top Bottom