Nashukuru na ninafurahi sana kuona sasa CDM wameweka kambi Morogoro. Ilikuwa ni aibu kwa majimbo yote ya mkoa huu kuchukuliwa na CCM katika chaguzi zilizopita. Hii ni njia nzuri ya kuleta mabadilikohasa katika mikoa yote ambayo inaonekana ina mizizi ya CCM kama Moro, Lindi, Tanga, Pwani na Mtwara na Ruvuma.
Shughuli za kuhamasisha mageuzi ya kisiasa zifanyike sasa. Inapofikia wakati wa uchaguzi, inakuwa tia maji tia maji tu. Mara nyingi vyama vilijikita vikienda katika majimbo haya wakati wa uchaguzi, na kuonekana kuwa ni wageni...hata wanapoonekana kukubalika wakati wa uchaguzi inakuwa ni wakati wa mikutano tu...inapotokea kwenye kupiga kura na kulinda kura...wale wananchama wa CCM hutumika kurubuni mawakala na kuiba kura..na hivyo wapinzani kuanguka katika majimbo haya. Sasa hivi hilo la wizi halita wezekana, kwani chama kitakuwa na watu wake waliopikwa na wenye moyo wa kuona mageuzi yanafanikiwa...hawa wanaoondoka sasa kutoka kwenye chama hiki dhalimu na wale waliohamasika kujiunga nacho hasa vijana..ndio watakuwa walinzi wa kura za UKombozi.
Mungu Yabariki Mageuzi haya!!