Aliyekuwa Katibu Mwenezi wa CCM kata ya Muhonda akieleza jinsi alivyokunwa na sera za CHADEMA zilizoelezwa na katibu Mkuu wa BAVICHA katika mkutano wa hadhara katika kijiji cha Kichangani.
Katibu Mkuu wa BAVICHA Deogratias Munishi akikabidhiwa kadi na sare za CCM kutoka kwa katibu mwenezi wa kata ya Muhonda Jimbo la Mvomero, Mzee Ngoya.
Katibu Mkuu wa BAVICHA Deogratias Munishi akimkabidhi kadi ya CHADEMA aliyekuwa mwenyekiti wa serikali ya kitongoji cha Kododo jimbo la Mvomero, bwana Charles Kiwaga. Wengine ni wanachama wapya wa CHADEMA tawi la Kododo Mvomero.
Katibu Mkuu wa BAVICHA Deogratias Munishi akikagua majengo ya shule ya msingi Kododo kata ya Luale jimbo la Mvomero. Shule hii ina wanafunzi 652 na mwalimu mmoja tu.
Mwenye shati la rangi ya udongo na suruali nyeusi-ndiye Mwalimu Mkuu na mwalimu pekee katika shule nzima ya Kododo iliyopo kata ya Luale, mwenye kombati,Katibu Mkuu wa BAVICHA Deogratias Munishi alipokuwa akionyeshwa hali halisi ya maendeleo kielimu katika kijiji cha Kadoda. Jengo lililopo nyuma ni moja ya madarasa ya shule hiyo.Picha na Habari na CHADEMA
--
Hali halisi ya Elimu Mvomero: Shule ya Msingi Kododa,Mwalimu mmoja wanafunzi 652
Operesheni Sangara inayoendelea kwa upande wa Katibu Mkuu wa Baraza la Vijana la CHADEMA (BAVICHA), Bwana Deogratias Munishi amezidi naye kupasua vijiji ndani ya Mvomero, Morogoro. Pia wanavijiji walimuonyesha hali halisi ya maendeleo katika kata yao ya Luale kwa kipindi kirefu walichokuwa chini ya CCM tangu miaka 50 iliyopita mpaka sasa na wakiwa wamekata shauri kujiunga na CHADEMA kama chachu ya mabadiliko