Kim na Rouhani wametuonyesha kuwa USA si lolote wala chochote, hawa ndio viongozi walionikosha tangu 2017

Pale US alipo Iraq anaweza kupata tarifa zote za kijasusi toka Iran, walijua jamaa wanajiandaa kushambulia na watashambulia wapi. Walichofanya ni kuondoa vinavyohamishika(mapema) na personnel wao. US ndiyo waliofahamu mwanzo kwamba Iran kaidungua ndege ya abiria ya Ukraine, japo Irani walibisha. Jamaa wako vizuri kwa intelligence, ndo maana Iran anafanya kila njia US aondoke ubavuni kwake. Anayekuzidi hukuzidi hata choo chake mkuu(hapo choo siyo jengo).

Sent using Jamii Forums mobile app
Imefahamika Jana you re great thinker br

Sent using Jamii Forums mobile app
 
KWAHIYO ZILE KAMBI WALIKUWA WANAFUAGIA PANYA SIYO?
Inabidi MTU kujitoa ufahamu ili akubali kuwa makombora zaidi ya kumi yanaweza kutua kwenye kambi ya kijeshi yenye maelfu ya askari halafu kusitokee madhara au vifo kwa askari!!
Kuna taarifa kwenye Uzi huu ikionesha .awasiliano rasmi ambayo wamarekani wanapeana taarifa za siri kuhusu madhara yaliyotokea na inataja askari waliokufa ni 146, na wengine wengi tu wamejeruhiwa na ndege kadhaa za kivita kuharibiwa! Wanavyosema wamempiga za USO hawatanii!!
Je uliiona sura ya Trump wakati anatoa taarifa ya tukio hilo?
Anayeweza kutuwekea tena taaria hiyo ya maafa sfanye hivyo tena! Ila iko kwa kiingereza na wamarekani wengi was bongo hilo ni tatizo!
 
Hivi we acha ujinga iliyoharibiwa ni sehemu ndogo sana ya kambi.Kama hujui tu ni kuwa roketi haishambulii na kuharibu eneo kubwa.Roketi 1 haiwezi hata kubomoa nyumba 2 za kawaida.Kwa hiyo kama unafananisha shambulio la roketi na mabomu basib utakuwa hujui unachoongea.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe ndio haujui! Roketi ni usafiri tu wa kusafirisha Bomu! Inategemea ni Bomu LA aina gani linasafirisha! Roketi pia zinapishana uwezo wa kubeba mzigo! Roketi yaani missile zinaweza kusafirisha hata mamia ya tani za mabomu! Inategemea kusudio la mhusika! Zinaweza kusafirisha hata mabomu ya nyuklia, inategemea mtumiaji anaitumia kusafirisha Bomu gani la uzito upi.
Kuna post kwenye Uzi huu inaonesha kiasi cha mauaji na madhara yaliyotokea! Itafute ukitaka!
 
Ungekuwa unajua vitu hata usingeandika upupu hapa.Hivi Kim Jong Un amefanya nini cha kumtingisha USA?Kipindi cha Obama na Trump ni kipi ambacho Kim ameonesha ubabe?Mara ya mwisho N.korea kurusha makombora bahari ya Japan ni Lini? Lini N.korea wamekorofisha S.Korea.Ukiangalia sasaivi Kiduku kaufyata.Adabu imekuwepo.Halafu kiduku alikuwa na utoto,saiz amepata ukubwa hana ujinga ujinga.

Kuhusu Iran ningekuona wa akili kama angalau angeuwa wanajeshi 5 tu wa marekani.Kushambulia kambi halafu usiue hata panyabuku huo nao ni ubabe?...wababe walikuwepo Cuba huko ,Urusi na Sio huko unakosema Iran wala wapi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Soma post namba 57 kuna ushahidi wa vifo vya askari wa Marekani na uharibifu mkubwa wa helkopta za kivita nk.
 
Wewe ndio haujui! Roketi ni usafiri tu wa kusafirisha Bomu! Inategemea ni Bomu LA aina gani linasafirisha! Roketi pia zinapishana uwezo wa kubeba mzigo! Roketi yaani missile zinaweza kusafirisha hata mamia ya tani za mabomu! Inategemea kusudio la mhusika! Zinaweza kusafirisha hata mabomu ya nyuklia, inategemea mtumiaji anaitumia kusafirisha Bomu gani la uzito upi.
Kuna post kwenye Uzi huu inaonesha kiasi cha mauaji na madhara yaliyotokea! Itafute ukitaka!x
Hii umejibu kitaalamu zaidi
 
Inahitaji kujitoa akili ili kudogesha teknolojia ya mtu anayeweza kutengeneza na kurusha kombora la balistiki ambapo nchi nyingi za Afrika hazijafikia hatua hiyo.
 
Back
Top Bottom