KIM JONG UN "JUU", HASSAN ROUHAN "CHINI".

KIM JONG UN "JUU", HASSAN ROUHAN "CHINI".

Mwakamajoka

Senior Member
Joined
Nov 21, 2017
Posts
170
Reaction score
149
Utawala wa serikali ya Irani umekuwa ni moja ya tawala ambayo inaandamwa kila kukicha na Marekani na mshirika wake wa karibu kabisa pale mashariki ya kati(Israeli). Kipindi cha utawala wa Barack Obama aliyekabidhi kijiti cha uongozi kwa raisi wa sasa wa Marekani(Donald Trump) palitokea mzozo mkubwa kati ya Mataifa ya Magharibi wakiwa bega kwa bega na Israeli dhidi ya Utawala wa Irani ambao ulishutumiwa kwa kuwa na mpango wa nuclear. Mpango huu hakuna taifa lolote la Magharibi lilouamini hata kidogo kwasababu kulikuwa na mkanganyiko kuhusu uhalisia wa mpango wenyewe, wapo waliosema mpango unajikita kwenye matumizi ya nishati(Umeme) wapo walioamini kabisa kwamba mpango ule unahatari kubwa sana kwa maana ya kwamba ulijikita kwenye mpango wa silaha hatari za nyuklia.


14/7/2015,kikafanyika kikao huko VIENA AUSTRIA kilichojumuisha nchi kubwa Duniani kama China, Ufaransa, Urusi, Marekani, Uingereza, Ujerumani, Irani na Umoja wa Ulaya (Irani+P5+1+European Union), kikao hiki ndicho kilichokuja na kuundwa kwa mpango unaofahamika kama Joint Comprehensive Plan of action(JCPOA) au Iran Nuclear Deal. Mpango huu ulisainiwa na nchi zilizounda hii equation (Iran+P5+1+European Union=JCPOA). Ukiwa na madhumuni yafuatayo :-
1:Kupunguza kwa kiasi kikubwa mashine za kurutubishia uranium(Centrifuges).
2:Kupunguza bidhaa na malighafi za uranium kwa kiasi kikubwa(Stockpile) .
3:Na malighafi zote za uranium zilizobaki zisirutubishwe kwa kiwango ambacho kinaweza sababisha kupatikana kwa silaha za nyuklia nk.

FIKRA ZANGU.

Unapo ona hili mwenzio anaona lile. Irani kunauwezekano mkubwa kabisa baada ya kubanwa na Joint Comprehensive Plan of Action alitulia na kutafakali kwa kina ni vipi atakamilisha mpango wake wa silaha za nyuklia. Bila shaka karata yao ikaangukia kwa serikali ya Siria ili kukamilisha kiu yao kuu ya Silaha za Nyuklia. Kwa maana ya kwamba ili waweze kukamilisha mpango huo ni lazima zifanyike jitihada makini ambazo zitafanikiwa kwa ufasaha lakini nje ya ardhi/mipaka ya Taifa la Irani, hapa ndipo inapokuja kujulikana ni kwa nini Israeli asubuhi, mchana na usiku anashambulia military bases za Irani zilizopo nchini Siria. Maeneo yote nchini Siria ambayo yameandamwa na Israeli lazima Irani anahusishwa kwa namna mbali mbali. Leo J3, 1/5/2018 kuna taarifa imetolewa na kiongozi mkuu wa serikali ya Israeli(Benjamin Netanyahu) akisema Irani baada ya kubanwa kwenye JCPOA amekuwa na harakati tukutu za kuendeleza nuclear programs kwa siri.

MASWALI YA KUJIULIZA.

1:Irani anatekeleza mipango yake wapi?

2:Irani kama anatekeleza mipango yake ndani ya mipaka ya Irani kwa nini Israeli isishambulie maeneo hayo nchini Irani?

3:Kwa nini Israeli anashambulia military bases za Irani zilizopo ndani ya mipaka ya Siria?

4:Siku chache zilizopita Marekani, Uk na Ufaransa walilusha makombora na baadhi ya maeneo yaliyoshambuliwa ni scientific research center na chemical weapons storage facilities, je nani mmiliki wa hizo programs ni Siria au Irani?

5:Na leo kuna taarifa nzito zimetolewa na Benjamin Netanyahu zikimtuhumu Irani kudaganya Dunia kwamba alishikamana na JCPOA lakini kiuhalisia anadai ni uongo mtupu, je Irani ndiye hatari zaidi kwa Israeli kuliko Mataifa mengine?

NGOME YA KIM JONG UN.

Kim Jong Un ameushangaza ulimwengu kwa majaribio ya kustaajabisha hasa katika nyanja ya makombora ya masafa marefu kama vile Hwasong-15 na silaha korofi za nyuklia. Toka taifa kubwa Duniani la Marekani kumpata Raisi Mpya Donald Trump Mataifa mbali mbali tumekuwa tukishuhudia mtu mzima(Trump) na kijana(Kim Jong Un) wakishambuliana kwa maneno yasiyo na staha kwa walimwengu waliostaarabika. Tumeshuhudia ubabe wa kila aina ukifanyika katika Peninsula ya Korea, Trump akitoa vitisho na vikwazo na Kim Jong Un akiwachezesha Dundo zito.

Utawala wa Marekani ukagubikwa na kigugumizi nini cha kufanya, tukashuhudia viongozi wa ngazi za juu wa taifa la Marekani wakiweweseka na hatimaye kuondoshwa kwenye nyadhifa zao(Rex Tillerson) na hatimaye akateuliwa Mr. Jonh Bolton aka JoBo na mambo yote yakabadirika ghafla kwa mfano shambulizi la kemikali Duma-Siria na mashambulizi ya kibabe yakifanywa na Marekani, Uk na Ufaransa ambapo makombora 103 yakirushwa na makombora takribani 71 yakidunguliwa juu kwa juu na majeshi tiifu ya serikali ya Siria.

Mambo hayakuishia hapo, tukashuhudia uharaka wa vikao vikubwa na vya kihistoria kama ifuatavyo :-

1:Wajumbe China kukutana na wajumbe wa Korea Kaskazini.
2:Kim Jong Un alivyoingia kimya kimya nchini China na kuzungumza na Mr. Xi Jinping.
3:Wajumbe wa Korea Kusini walivyokutana na wajumbe wa Korea Kaskazini.
4:Kikao kisichoonekana kati ya Kim Jong-un na Mr. Mike Pompeo.
5:Kilichofatia ni kukutana viongozi wakuu wa Mataifa hasimu kabisa Duniani, ambapo Kim Jong Un na Mo Jae In walizungumza mambo mazito kiasi kwamba Mataifa mengi yanaona mwanga uliopotea kwa muda mrefu sana.

6:Mwezi huu wa tano tutegemee kushuhudia kikao cha kipekee kati ya Kim Jong Un na Raisi wa Marekani Donald Trump.

Kim Jong Un "JUU"Hassan Rouhan"CHINI" , kama tu Donald Trump atalidhika na matakwa ya Kim Jong Un. Nguvu iliyotumika kumdhibiti Korea Kaskazini (Kim Jong Un) itahamishiwa kwa Irani(Hassan Rouhan). Na kama deal ya peninsula ya korea itashindikana hakika mambo yatakuwa mabaya zaidi.
 
Utawala wa serikali ya Irani
.

Kim Jong Un "JUU"Hassan Rouhan"CHINI" , kama tu Donald Trump atalidhika na matakwa ya Kim Jong Un. Nguvu iliyotumika kumdhibiti Korea Kaskazini (Kim Jong Un) itahamishiwa kwa Irani(Hassan Rouhan). Na kama deal ya peninsula ya korea itashindikana hakika mambo yatakuwa mabaya zaidi.

Umefafanua vema. Marekani wamepunguza tatizo la jinsi ya kuikabili Iran. Patana na Korea Kusini tubaki na adui mmoja tu wa kushughulika naye.
 
Wakati wakubwa wako wanaomba SULUHISHO juu ya Iran Izrail anapiga kelele nyingi yaani hana raha, JAMAA WAMEAHIDI KUWA BOMU 1 LITAKAPOTUA ARDHI YA IRAN BASI ATAITOA IZRAIL KWENYE RAMANI YA DUNIA. Ukweli wa mambo ni kuwa wajemi hawa silaha za nyuklia wanazo na vinu vya nyuklia wanavyo pia, ni bora suluhu ipatikane ili huu mgogoro usije kuwa mkubwa
Screenshot_20180501-171512.jpg
 
Kitu pekee kinachowaumiza kichwa ni kwamba vile vinu vya nuklia vilivyopo iran, vimetengenezwa na Mrusi, washajaribu sana kuvishambulia ili waviharibu matokeo yake wameshindwa na mitambo iendayo kushambulia ama kuviharibu, huabirika yenyewe. In short vile vinu vinajirinda vyenyewe. Hilo ndo tatizo na wanaogopa piga direct pale wanajua kinachoweza wakuta, wale waajemi si watu wa mchozo, karata zao wamezichanga vizuri na zimechangika haswa.
 
Back
Top Bottom