Kilosa leo: Hii ni sawa na kusema bomu lililolengwa kwa adui limeangukia uraiani kwa mrusha bomu!

Nimecheka sana yaani mshikaji akabidi abadili gia angani tena juu kwa juu
 
Hiyo ndiyo safi sana wacha wafanye hivyo maana mwanzo wa Hesabu ni moja
 
.
Nashangaa wapinzani wa kweli kujiandaa kushiriki uchaguzi ambao ni dhahiri shairi ccm haiko tayari kukubali kupoteza. Ilipaswa kelele iwe ni tume huru ya uchaguzi, mpaka wanaojiandaa kuchezea uchaguzi wajue hali ni mbaya.
Tatizo lako ndio hilo kukariri mambo yasiyo ya msingi. Kama tume sio huru mbona mlikuwa mnapata wabunge?
Mbona kila chama kinaweka wakala na anajaza fomu za matokeo na matokeo yanabandikwa nje kila kituo na kila hatua husika? Na mawakala wanasindikiza hayo maboksi ya kura?
Acha kuwa na visingizio ambavyo havina kichwa wala miguuu.
 
Kampen zimeanza kumbe?
 
Lakini pia ni ukweli, siyo rahisi DED akubali kuuawa na wananchi kwa kuogopa kufukuzwa kazi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Kwa taarifa yako hata jangwani huwa mvua inanyesha japo mara chache. Tulikuwa tunatapa wabunge wakati demokrasia ikiwa na afadhali, kabla ya awamu hii kuingia madarakani. Hata hivyo bado malalamiko yalikuwepo kuwa tume si huru.

Baada ya kuingia awamu hii udhaifu wa tume umekuwa wazi sana. Nimeona kwa macho yangu mawakala wa upinzani wakigomewa kuapishwa, na kupata usumbufu wa wazi. Nimeona mawakala wakilazimishwa kusaini fomu za matokeo zisizo halali, tena kwa uratibu wa jeshi la polisi. Wakala gani anasindikiza matokeo, au unadhani wananchi hawaoni kinachotokea? Narudia tena, sina chembe ya shaka ya ninachosema. Tume hii ya uchaguzi sio huru na imejigeuza kuwa mawakala wa kunajisi uchaguzi, na ni mwendawazimu tu atakubali kushiriki uchaguzi chini ya tume hii.
 
Hapo ndipo tukisikia "... inategemea nimeamkaje!!"
Kampeni zimeshaanza...
 

Kampeni zilianza toka 2016. Sasa wanamalizia malizia tu!
 
Mnapeleka mawakala ambao hata barua ya utambulisho toka mwenyekiti wa mtaa hawana. Hapo mnatarajia nini? Habari ya tume kunajisi matokeo ni uongo maama taratibu na sheria huwa zinafuatwa. Jambo ambalo gumu kwako ni kukubali kuwa Ccm inakubalika kwa wananchi maana inatekeleza ilani yake inavyotakiwa.
 
walimuua binti yetu Aquiline masikini, lakini hakuna mwananchi hata mmoja aliyesema fyoko!

Woga umekuwa utamaduni wa ‘wadanganyika’ wa Tanzania, ambo ndo walio wengi. Hata hivyo, maumivu yakiendelea kwa muda mrefu, uvumilivu na woga hatima vitafikia mwisho na hakuna askari au risasi zitakazotosha kudhibiti nguvu ya umma uliochoka!
 
Upo sahihi sana mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…