Kilombero sugar company kwafutuka mgogoro | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kilombero sugar company kwafutuka mgogoro

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Magane, Oct 23, 2012.

 1. M

  Magane Member

  #1
  Oct 23, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 99
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Wanajamii hali ni tete kampuni ya sukari kilombero baada ya malipo ya bonus kulipwa kwa wafanyakazi wake kiubaguzi. Wafanyakazi wa muda na wa msimu walikusanyika mbele ya ofisi kuu ya kampuni wakidai kwamba wamelipwa bonus kinyume na tangazo kwa wafanyakazi wote. Mbaya zaidi tukio hilo lilitokea wakati wa kikao cha board of directors ambao kwa kiasi kikubwa ndiyo wenye kufanya maamuzi juu ya masuala mbalimabali ya uendeshaji wa makampuni yao ya sukari. walipotoka nje walizomewa na vijana hawa nguvu kazi ya kampuni. Kana kwamba hiyo haitoshi nao mameneja wanahoji malipo haya kulipwa kwa misingi ya kibaguzi.Hali sasa katika kampuni ni tete wakuu wa idara wanajaribu kutumia theory ile ya british rule ya divide and rule kwa kuita moja moja kwenye ofisi za wakuu wa idara. Bahati mbaya kwao ni kwamba maneja wa sasa siyo wale wa miaka ya sabini na themanini.Mgogoro wa mameneja unakolezwa na hali tata ya muda mrefu ya kupuuzwa na kudharauliwa na sasa wanataka kujiunga na chama cha wafanyakazi ili wapate mahali pa kutolea matatizo yao ya msingi kwani kwa sasa chama kimeshikwa na junior employees ambapo senior management team siyo tu wanawaheshimu pia wanawaogopa na kuwatetemekea kiasi kwamba hawa jamaa wa chama cha wafanyakazi wanachoomba au kuhitaji wanapewa bila shaka yoyote. Chama cha wafanyakazi kimeshika mpini hapa kilombero. Matokeo yake heshima iko kwa chama na mameneja kuupuzwa.
   
 2. k

  kamkoda JF-Expert Member

  #2
  Oct 24, 2012
  Joined: Sep 20, 2012
  Messages: 396
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  hivi HR wenu si yule mzee alikuwaga ATE miaka ile mwenye maneno meeeengi! Lkini nijuavyo bonus sio statutory payment ni kipato kinachotokana na performance na huwezi fananisha kuli na Meneja hata siku moja eti mlipwe sawa ama uwiano wa tofauti usiwe mkubwa, heshima itashuka. Waagizeni vijana wawe na adabu vinginevyo watapigwa chini, huko kuitwa nijuavyo wanatafuta wanaharakati...watch out acheni ushabiki fanyeni kazi!
   
Loading...