Ni katika kuendeleza ubabe wake na ulevi wa madaraka DC wa kilolo bw.Gerald John Guninita amemweka rock up ya mbigili police station mwenyekiti wa kijiji cha udekwa bila sababu ya msingi.
DC huyu alifika kijijini hapo kwaajili ya kuendesha mkutano wa kumng'oa mwenyekiti huyo wa kijiji (CHADEMA) ambapo fununu zilishavuja siku chache kuwa ujio wake utakuwa maalumu kwaajili ya kuja kumng'oa mwenyekiti huyu ambaye hana hatia yoyote zaidi ya kuwa mwanachama wa CHADEMA.
Lakini gafla alibadilisha mkutano na kuwa kikao cha ndani hali iliyowashangaza wengi na wakiwa ndani ya kikao alimuuliza mwenyekiti huyo kwanini anarekodi kikao kwa njia ya simu,ambapo mwenyekiti alijibu kuwa anarekodi kwa kumbukumbu hivyo DC akaamuru polisi walioongozana nao wamkamate mwenyekiti huyo ili akamtie adabu.
Hata hivyo mmoja ya askari waliomkamata amekiambia chanzo changu kuwa DC amewaamuru wamweke ndani kwa siku mbili na baadaye wamwachie kwa masharti ya kuripoti kituoni kila siku assubuhi kwa muda wa wiki moja
Ikumbukwe kuwa hoja ya DC kutaka kumng'oa mwenyekiti huyu ni baada ya wananchi wake kumzomea mbunge wa kilolo myezi kadhaa iliyopita pale alipoenda kijijini hapo kama mbunge huku akiambatana na makada wa ccm kwa lengo la kukinadi chama hali iliyomfanya m/kiti ahoji kama ziara ile ilikuwa kwa shughuli za chama au mbunge .......nitaendelea baadaye