Sura siyo issue sana, kubwa ni je kapigwa kweli bila kuambiwa kosa lake? Pamoja na hayo Polisi hatakiwi kumpiga mtuhumiwa kama hajawafanyia fujo, na hata kama mtuhumiwa atawafanyia fujo wanatakiwa kwanza watumie ujuzi wao kumdhibiti, na si kuanza kutumia nguvu ya ziada. Matukio kama haya tusiweke ushabiki wa kichama kwani polisi haohao kesho watakuja kwako kama si kwa familia yako.