Kilio cha baba na kifo cha jumuia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kilio cha baba na kifo cha jumuia

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by INGI, Oct 24, 2012.

 1. I

  INGI Member

  #1
  Oct 24, 2012
  Joined: Jan 18, 2011
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hawezi kuniingia akilini kwa baba anayeomboleza tabia za watoto wake hali hachukui hatua. Kuanguka kwa Fredrick Sumaye kule Hanang kulinisaidia kujua kuwa kumbe sio tuhuma bali ni ukweli rushwa ndio mtaji wa wanasiasa wa CCM kufikia malengo. Ukweli huu umetekelezwa tena na jumuiya wa wanawake UWT, mchakato ni ule ule kubaki kwenye kiti au kukifikia kiti tarajiwa. Na sasa vijana, mambo yale yale. Wakati huo mwenyekiti anajaribu kuwaonya hao wanawe kuwa tabia hiyo inatangamiza familia yake. Swali langu ni kuwa Baba huyo (mwenyekiti) anavyo vyombo mahususi vya kushughulikia mambo hayo, kwa nini asiwaruhusu kutekeleza majukumu yao kama sheria inavyowataka. Mtandao wa rushwa haukuwa na sumu wakati wa kumwangusha Sumaye lakini sasa unaonekana umepenya sana kiasi cha kushtua baba wa familia. Sumu ikishaingia kwenye ini, figo na ubongo kuna ubonyaji? Uchafu wa mwili hauwezi hauwezi kuchunjwa na hata taarifa muhimu haziwezi kuchambuliwa na amri halali kutolewa maana viuongo muhimu vya mwili vimeathirika. Namsihi baba wa familia kuchukua hatua, haitoshi kulalamika.
   
 2. W

  Wizzard Wweed Senior Member

  #2
  Oct 24, 2012
  Joined: Oct 19, 2012
  Messages: 108
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Basi subiri mwanae mkuu aje zua kilio mjengoni?,ndo wana teketea hivyo.waache wajika ange.
   
Loading...