Kilimo Kwanza; Sauti ya Yakobo, Mikono ya Esau..... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kilimo Kwanza; Sauti ya Yakobo, Mikono ya Esau.....

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Amavubi, Mar 2, 2012.

 1. Amavubi

  Amavubi JF-Expert Member

  #1
  Mar 2, 2012
  Joined: Dec 9, 2010
  Messages: 29,473
  Likes Received: 4,752
  Trophy Points: 280
  Napata tabu sana kupata utashi wa dhati wa viongozi wetu katika suala la kinachoitwa kilimo kwanza. Ukisikiliza sana kauli zao na kuangalia kinachofanyika katika hali halisi utaona kabisa kwamba ni aina fulani ya mtaji wa kura kwa kucheza na mindset za Watanzania. Nimemsikiliza Mkuu wa nchi jana (01032012) na kuona kwamba bado tunayo safari ndefu ya kufikia azma ya ukombozi wa kiuchumi kupitia kilimo.....Hebu angalia kwanza kauli yenyewe kilimo kwanza....ukisikiliza utadhani ndio kipaumbele cha nchi katika sera, mipango na bajeti lakini kiuhalisia kilimo kwanza hakina tija kwa mkulima masikini wa Tanzania bali kwa wawekezaji wakubwa hususan wa kigeni hasa katika kukidhi matakwa ya nchi za ughaibuni. Ona kwa mfano jinsi ambavyo mashamba makubwa yalivyokuwa yanailisha nchi hii kama vile Mbarali, Kapunga, Rufiji nk yalivyogawiwa kwa wawekezaji ili kupanda mazao ya nishati uoto kama vile mbono kaburi (jatrofa) ambao kwa hakika ni kwa ajili ya kupata mafuta ya magari ya huko.....hivi kweli tuna dhamiri ya dhati ya kufanya kilimo kiondoe njaa Tanzania?

  Sijui wadau mnasemaje...
  .
   
 2. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #2
  Mar 2, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160


  Mrisho Mpoto, swali
  Kilimo kwanza ni kaulimbiu au mpango Wa kumaliza njaa Tanzania, karne ya 21 bado Chakula ni issue Ndiyo nipo kwenye gate la ukaguzi IKULU kumueleza Mjomba kuwa tuna taka utekelezaji Wa mengi tuliyokubaliana kabla ya kumpa Funguo ya jengo jeupe


  Ndimara Tegambwage,jibu


  Mpoto ndugu yangu!
  Kilimo kwanza ni wao
  Na kilichopo ni chao
  Si chako, si changu
  Hata kaulimbiu ni yao
  Wewe na mimi kalagabao!
  Yetu yawe makofi - pwa! pwa! pwa!


  Ndoto wamepandikiza
  Vichwani mwa hohehahe
  Eti watakula
  Eti watashiba
  Hata kuvimbiwa
  Eti watasaza
  Hata kuuza nje
  Eti neema yaja
  Yetu yawe makofi - pwa! pwa! pwa!


  Si changu si chako
  Kilimo Kwanza ni chao
  Tunda la mbongo zao
  Wenye mipango lukuki
  Wenye wenyeji ikulu
  Na katika vyake viunga
  Wenye "kontakti" nje
  Na ndani kusaka manamba
  Yetu yawe makofi - pwa! pwa! pwa!


  Wamekaa Marekani
  Hata nyumanju ya ikulu
  Wazawa na wakuja
  Kunguru ni kunguru tu!
  Wamevikuna vipara
  Na kilimo wakatua:
  Ndio lango, ndio shibe
  Mwafaka wa wanga.
  Yetu yawe makofi - pwa! pwa! pwa!


  Ili wapate ardhi, wameimba:
  Kilimo Kwanza
  Ili wapewe mikopo, wameimba:
  Kilimo Kwanza
  Ili wapewe kipaumbele, wameimba:
  Kilimo Kwanza
  Ili wale, wanywe ikulu, wameimba
  Kilimo Kwanza
  Waite unavyotaka:
  Wawekezaji au wawekezwaji?
  Yetu yawe makofi - pwa! pwa! pwa!


  Wanatafuta miliki
  Ya ardhi na mazao
  Wanahemea mapato
  Kwa migongo ya wazawa
  Wanatafuta fadhila
  Kwa ikulu na kwingineko
  Wale, washibe, wasaze
  Yetu yawe makofi - pwa! pwa! pwa!


  Kilimo Kwanza mpango
  Wa wakubwa kuvimbiwa
  Kilimo kwao kutaja
  Hilo hasa ni kudandia
  Waonekane wanajali
  Njaa kuikong'ota
  Kumbe njaa yao faida, ziada
  Nasi yetu makofi: pwa! pwa! pwa!


  Sikiliza wa Mpoto
  Na umri wako rejea
  Kilimo kwanza ije leo
  Jana ulikulani?
  Mkolezo una jambo
  Ni shinikizo babukubwa
  Wanasiasa waimbe
  Wafike kukushawishi
  Wanamipango wanene
  Eti huo "ukombozi"
  Ili uone sasa utapona:
  Kumbe tai anashuka
  Chako kitakuwa chao
  Na chao kitabaki chao
  Nasi yetu makofi: pwa! pwa! pwa!


  Wanayo yao madai
  Kilimo kikubwa wataleta
  Kilimo kikubwa ni ardhi kubwa
  Hata yangu na yako kumezwa
  Hata ya mkulima wa jembe,
  Yule aliyetulisha hadi jana
  Hadi leo na hadi kesho wavunapo
  Chwai! Itakwenda
  Nasi tutabaki na makofi: pwa! pwa! pwa!


  Kilimo kikubwa mitambo
  Walokuwa wakulima
  Sasa wawe manokoa;
  Wale wa kurandwa mijeredi
  Mithili ya utumwa wa babu.
  Kutumika watatumika
  Kutumiwa watatumiwa
  Kuchakaa watachakaa
  Mafao yao ni hapa
  Kwani wao watumishi
  Kwa soko lile la nje
  Lile la wawekezaji
  Au sema wawekezwaji
  Nasi yetu makofi: pwa! pwa! pwa!


  Kilimo kikubwa mbegu
  Mbegu nyingi kutumika
  Mbegu zao za viwanda
  Wanaziita za kisasa.
  Za asili zitapotea, pwe!
  Sote tule vikakara
  Vyenye ladha masimango
  Tubaki tukiimba
  "Maendeleo, maendeleo!"
  Makofi kuwapigia: pwa! pwa! pwa!


  Kilimo kikubwa mbolea
  Ile ya kwao viwandani
  Ardhi hii kunajisi.
  Baada ya miaka mitatu, minne
  Nayo kuwa kikakara
  Hakimei kisichochao
  Hakikui wasichotaka
  Hakipandwi wasichoruhusu
  Sote hatufurukuti
  Tunalinda soko la "bwana!"
  Tunaendelea: pwa! pwa! pwa!


  Kitu gani hatuwezi
  Wewe na mimi,
  Pale madarakani tukikaa?
  Hata hayo tungefanya
  Kwa mipango, kwa haki.
  Sasa wafanye kunguru
  Wasiothamini utu?
  Wasiothamini asili yako?
  Watumikiao soko la nje
  Kwa kutufanya manokoa?
  Kwa mwavuli wa Kilimo Kwanza?
  Nasi tuendelee kuwapongeza
  Kwa makofi: pwa! pwa! pwa!


  Kilimo Kwanza ni wao
  Wao hawa watafutaji
  Kama mipango ni yao
  Na kaulimbiu ni yao
  Sisi twabaki na njaa yetu
  Njaa ya kualika
  Njaa ya kusukumiziwa;
  Na kwa sauti zilizonyauka
  Macho yaliyoenda kengeza;


  Kwa uchovu
  Miili iliyofinyazwa kwa viboko;
  Vile viboko vya watawala
  Na wawekezwaji.
  Halafu tupige makofi
  Pwa! pwa! pwa!


  Afadhali "Kilimo Mwisho"
  Kuliko Kilimo Kwanza
  Kilimo Kwanza si chako
  Kilimo Kwanza si changu
  Acha watu na dili zao
  Wewe na mimi tufumbuke
  Tuache kupiga makofi
  Mwisho wa pwa! pwa! pwa!
  Ndio mwanzo wa kufikiri.  Chanzo. Mabadiliko
   
 3. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #3
  Mar 2, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Haya bana nikupe hongera kwa shairi lako zuri linaloongelea ukweli mtupu ktk hii kauli mbiu ya kilimo kwanza
   
 4. Amavubi

  Amavubi JF-Expert Member

  #4
  Mar 2, 2012
  Joined: Dec 9, 2010
  Messages: 29,473
  Likes Received: 4,752
  Trophy Points: 280
  Allaaaahhh!!!!! kumbe ni KAULI TU ehhee!!!! ...kwetu huku walalahoi sio?
   
 5. Goodrich

  Goodrich JF-Expert Member

  #5
  Mar 2, 2012
  Joined: Jan 29, 2012
  Messages: 2,050
  Likes Received: 632
  Trophy Points: 280
  Kilimo kwanza ni chao, Maisha bora ni yao, hata kauli mbiu ni yao. Sisi yetu makofi pwa pwa pwa !
   
 6. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #6
  Mar 2, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,798
  Likes Received: 3,884
  Trophy Points: 280
  Kilimo kwanza ni slogan au propaganda ya kisiasa iliyoanzishwa na wanasiasa kwa lengo la kupata mvuto kutoka kwa wapiga kura.Ili kilimo kwanza kifanikiwe na kiwe endelevu kilipaswa kushirikisha wataalamu mbalimbali wa kilimo ili waunde sera na kusimamia utekelezaji wake,.Lakini leo hii ni ajenda ya wanasiasa ambao hawajui kilimo chetu kimekwama wapi??Tunahitaji mbegu bora, tunahitaji umwagiliaji, tunahitaji zana (machinery), tunahitaji viwanda vya kusindika, tunahitaji watalaam hadi ngazi za vijiji, tunahitaji masoko ya bidhaa za kilimo, tunahitaji pembejeo nyingine kama mbolea madawa, tunahitaji watafiti, wagani, nk. Hayo yote yanahiji pesa, je ni kiasi gani kimetengwa kwa wizara ya kilimo kutekeleza mkakati huu??na uko wapi mpango kazi wa serikali kutekeleza hiki kilimo kwanza??Je evaluation inafanyikaje na baada ya muda gani??Serikali ifanye siasa lakini mambo ya kitaalam wawaachie wataalam, otherwise tutaendelea kupiga hatua moja mbele na tano nyuma!!!
   
 7. m

  mzambia JF-Expert Member

  #7
  Mar 2, 2012
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 885
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Itakuwaje kilimp kwanza wakati hata wakulima wakiuza mazao yao zambia au malawi serikari inakimbilia kufunga mpaka afu yenyewe haiyanunui mpaka yanaoza mikononi mwa wakulima.
   
 8. c

  collezione JF-Expert Member

  #8
  Mar 2, 2012
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 360
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Kilimo kwanza ni usanii tu.

  Utasemaje kilimo kwanza hamna barabara? Hayo mazoa si yataoza shambani.

  Utasemaje kilimo kwanza hamna umeme. Utahifadhi kivipi hayo mazao.

  Utasemaje kilimo kwanza elimu ya waTZ ni hoi. Si ndo mwanzo wa kukata mikono albino ili wabutue ela kirahisi.

  Kilimo kwanza ni cha JK na familia ake. Full stop
   
 9. Amavubi

  Amavubi JF-Expert Member

  #9
  Mar 2, 2012
  Joined: Dec 9, 2010
  Messages: 29,473
  Likes Received: 4,752
  Trophy Points: 280
  Tanzania itajengwa na wenye moyo na kuliwa na wenye meno..
   
 10. Amavubi

  Amavubi JF-Expert Member

  #10
  Mar 2, 2012
  Joined: Dec 9, 2010
  Messages: 29,473
  Likes Received: 4,752
  Trophy Points: 280
  ..kabla ya full stop...na wawekezaji kisha fool stop
   
 11. Amavubi

  Amavubi JF-Expert Member

  #11
  Mar 2, 2012
  Joined: Dec 9, 2010
  Messages: 29,473
  Likes Received: 4,752
  Trophy Points: 280
  wanafunga mipaka ili wauze yao kwanza
   
 12. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #12
  Mar 2, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Hebu fanya kiunganishi kati ya mada na metaphor uliyotumia
   
 13. Amavubi

  Amavubi JF-Expert Member

  #13
  Mar 2, 2012
  Joined: Dec 9, 2010
  Messages: 29,473
  Likes Received: 4,752
  Trophy Points: 280
  hicho ni kisa cha mtoto aliyempateli baba yake kwa kuwa alikua ni kipofu......alichofanya alijivika ngoZi ili afanane na kaka yake hatimaye apewe baraka ya kuwa mrithi halali wa mali......alipeleka nyama iliyonona kwa baba yake na kumuomba ampe mbaraka wa kurithi mali pindi atakapotoweka duniani...baba alipomshika mkono akadhani ni mtoto wake wa kwanza ( Esau) lakini aliposikiliza sauti akaona ni ya mtoto wa pili na kusema sauti ni ya yakobo hali mikono ni ya esau.....kiunganishi katika kilimo kwanza viongozi wana mikono tofauti na sauti zao, wakiwa jukwaani wanahubiri kilimo kwanza tofauti na matendo halisi yanayofanyika kwenye say utengwaji wa bajeti etc (they preach what they dont practise and they practise what they dont preach) ie they say what they dont do and they do what they dont say...sasa soma kianzio cha mada
   
 14. c

  collezione JF-Expert Member

  #14
  Mar 2, 2012
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 360
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  inaelekea raisi wetu hajui maana ya kipaumbele. Ebu tujadili iko "kilimo kwanza".

  Tuangalie Je, wataalamu wetu waomaliza vyuo wote wanaenda kulima? Hata kama sio wote, tuseme 80%.

  Kilimo kwanza kina-ajili watu wangapi hapa Tanzania? Na kinaingiza pato la taifa kiasi gani?

  Kama hizo factor are not satisfied, then kilimo kwanza as a mojor sector is "usanii"

  Waziri mkuu mstaafu wa Malaysia alishawahi kusema. "Kiongozi shuvapu na jasiri ni yule anayeweza badili uchumi wa nchi yake kutoka kwenye kilimo mpaka kwenye viwanda".

  China, India, Singapore, Malaysia wameweza. Viongozi wao wamekuwa wajasiri na shupavu. Leo wanatengeneza magari hawa jamaa.
  Sisi hata toothpick tuna-import.

  Shame kwa viongozi wanaotumia mwanya wa waTanzania ambao hawana uelewa...
   
 15. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #15
  Mar 2, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Unashangaa ya kilimo kwanza wakati hadi leo hii wafanyakazi wa serikali hawaajlipwa mishahara??????
  eti hazina hakuna umeme kwa siku ya 3, hivi hili linakuingia akilini?
  Are we serious?
  Umewabana wafanyakazi na wafanyabishara wadogo wadogo wenye viduka kodi hadi wengine wanafungua maduka usiku kwa kuogopa maofisa wa TRA. wanaojibana kuleta magari ndio hivyo tena, wanalipa kodi za kufa mtu, leave alone kodi kwneye petrol na mengine.
  Leo unashindwa kuwalipa mishahara?

  This is Tanzania.
   
 16. Kashaijabutege

  Kashaijabutege JF-Expert Member

  #16
  Mar 2, 2012
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 2,699
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  KAULI MBIU MNAISEMA NUSU TU. KAULI MBIU KAMILI INASEMA

  "Kilimo kwanza, malalamiko baadaye". Haina maana ya kuwa kilimo ni kipaumbele. Wakulima wanahimizwa walime badala ya kulalamika..oh hatuna pembejeo, oh bei ya mazao iko chini, oh mazao hayana soko..n.k
   
Loading...